Maoni ya Mbunge Neema Lugangira kuhusu Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika, CAADPBR

Maoni ya Mbunge Neema Lugangira kuhusu Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika, CAADPBR

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum CCM - Kagera Mhe. Neema Kichiki Lugangira, Anaandika;

Namshukuru Mhe. David Kihenzile, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kwa kunipa fursa ya kuwasilisha Mada kuhusu Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika CAADPBR kwa Tanzania ambapo nilianisha:

Mipango ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza Kilimo na Sekta zote za Uzalishaji na namna ambavyo ameibeba Ajenda ya Kilimo kama moja ya maeneo ya kipaumbele kwake na Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza kwa Umahiri Mkubwa

Matokeo ya Tathmini ya Tanzania iliyofanywa na Umoja wa Afrika AU katika Utekelezaji wa CAADP: Mwaka 2018 = 3.08/10, Mwaka 2020 = 5.08/10 na Mwaka 2022 = 6.14/10

Ongezeko kubwa la Bajeti ya Kilimo kutoka TZS 294B/USD 126M (2021/22) hadi TZS 954B/USD 408M (2022/23)

Nilielezea pia kwa kina jitihada za Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan za kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi katika Sekta ya Kilimo na Sekta zingine za Uzalishaji Tanzania 🇹🇿

Aidha, kupitia Mkutano huu wa African Union wa Wabunge kujadili Maendeleo ya Kilimo Afrika. CAADPBR, nimepata uelewa mpana zaidi katika eneo la kuongeza uwekezaji kutoka sekta binafsi ya nje ya nchi hivyo hii inakwenda kuwa moja ya Ajenda zangu katika Bunge la Bajeti 2023 kwa lengo la kuchangia Utekelezaji wa Maono ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika eneo hili la Diplomasia Ya Kiuchumi

Kipekee, nampongeza Mhe. Mwenyekiti wetu Kihenzile kwa Uwasilishaji wa Mada juu ya Maeneo ambayo Bara la Afrika linahitaji kuyachukua ili kuiwezesha Afrika kuwa wazalishaji wakubwa wa Mazao muhimu duniani.

Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Kihenzile amewasilisha kuwa katika nchi 10 duniani zinazoongoza kwa uzalishaji wa Chai ni nchi moja tu ya Kenya kutoka Afrika imeshika nafasi ya 3 mwaka 2022 kwa kuzalisha Tani laki 4 tu huku nchi ya kwanza duniani ikiwa ni China inayozalisha Tani 2.4m ikifuatiwa na India inayozalisha Tani milioni moja.

Tujiulize, kwanini iwe hivyo? Nini kifanyike? Kwa umoja wetu kama Wabunge tumejipanga kuishauri vyema Serikali.

FqULKGEXoB4dMWS.jpg
FqUJDttXgAAwGxP.jpg
WhatsApp Image 2023-03-05 at 07.51.54(1).jpeg
 
Back
Top Bottom