Maoni ya Mtanzania anayeishi UK kuhusu kupanda kwa kodi za majengo

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Haya ni maoni ya Mtanzania ambaye kwa akili yangu nimemuona kama hajielewi na hajui jinsi vile hizi kodi na tozo zinavyotafunwa Kifisadi hapa Tanzania πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Hii kodi ni ndogo sana...kwa mwezi...

Nyumba ya kawaida ilitakiwa ilipie kodi ya jengo walau 5000/ kwa mwezi

Waafrika tunadhalilishwa kwa kulazimishiwa hadi u GAY kwasababu hatutaki kabisa kulipa kodi.....tunapenda sana serikali zetu ziwe omba omba

Hivi kweli jamani NYUMBA ya chini kulipa kodi 2000/= nalo ni la kulalamika?????

Tulalamikie hela zikiliwa lakini kodi ya majengo ni chini sana.

UK kodi ya jengo kwa mwezi kwa nyumba ya chumba kimoja tu ni Β£100 kwa mwezi sawa na shs 361,000/= ndio maana wanatujengea hadi mashimo ya vyoo kwa wanafunzi wetu sisi ambao hata shs 2000/= tu tunahamasishana kugomeaπŸ€·πŸΏβ€β™€οΈπŸ€·πŸΏβ€β™€οΈπŸ€·πŸΏβ€β™€οΈπŸ€·πŸΏβ€β™€οΈ

Kama kweli tunataka kuwa HURU basi tuanzie kwenye kuwa na independent budget yetu wenyewe na kweli TUFUNGE MIKANDA KULIPA KODI ZA SERIKALI NA ZA MAJIJI NA MANISPAA
 
Haya ni maoni ya Mtanzania ambaye kwa akili yangu nimemuona kama hajielewi na hajui jinsi vile hizi kodi na tozo zinavyotafunwa Kifisadi hapa Tanzania...
Hizo hela zisingekuwa zinatafunwa na watu wachache bila kuchukuliwa hatua yeyote labda hoja yake ingekuwa na mashiko na wananchi wangeelewa maana kinachofanyika kinaonekana...hauweji kujenga nchi huku unafuja hela
 
Hizo hela zisingekuwa zinatafunwa na watu wachache bila kuchukuliwa hatua yeyote labda hoja yake ingekuwa na mashiko na wananchi wangeelewa maana kinachofanyika kinaonekana...hauweji kujenga nchi huku unafuja hela
Nilianzisha uzi mwingine kama majibu yangu kwake na kashindwa kunijibu

 
Nimeona tangazo la Tanesco likikanusha kupanda Kodi hiyo na wanadai wanakusanya madeni ya wale waliolipia 1000- baada ya kuanzia kwa 1500-
 
Hizo hela zisingekuwa zinatafunwa na watu wachache bila kuchukuliwa hatua yeyote labda hoja yake ingekuwa na mashiko na wananchi wangeelewa maana kinachofanyika kinaonekana...hauweji kujenga nchi huku unafuja hela
Nisha ongea sana humu bila watu kulipa kodi haitakuja kamwe mtanzania Kujielewa. Angalia sisi wafanyabiashara tulivyo na msimamo nantunavyoweza kutetea maslahi yetu, kulipa kodi kunauma hivyo unadai haki yako.

Kila mtu akilipa kodi ni rahisi kuiwajibisha serikali, mtu anayelipa kodi ukiwambia aandamane ataandamana tu sababu hela yake inamuuma, ila kama hela yako yote we unakwepa kodi ndio inazalisha taifa kama letu.
 
😑
 
Mambo mengine ni kweli yanashangaza!! Unakuta uanaambiwa changia Hela tununue kifaa cha kumsaidia mkeo wakati anajifungua mtu anakataa na wakati huo huo anaendelea kumtia mimba !! Hizo ni akili kweli au matope
 
Najua Watu wengi sana hapa mtampinga japokuwa amesema ukweli mchungu sana. Tatizo lililopo Tanzania ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi wa nchi hii, kwa hiyo hata kama Kodi ya pango la Ardhi itaongezwa kwa 2000% bado haitasaidia kitu kwani mafisadi waliopo Serikalini watazifanyia ufisadi fedha zote kabisa na Wala malengo tuliyojiwekea hayatatimia.
 
binafsi, hiyo kodi ya nyumba sioni kama kubwa, ni ndogo sana na inatakiwa kuongezwa kama ingekuwa inaenda kufikia kwenye mikono salama. jaribu kufikiria, kwa siku unatumia bando la bei gani, unakunywa mipombe bei gani, n.k kwanini hiyo hela usipeleke kujenga nchi yako? kama hazitafikia kwa wezi?
 
HUYU HAJIELEWI, AMESHA SHIBA MUTTON, TUMSAMEHE, UCHUMI WAO NI MKUBWA, SASA HATAMBUI HILO!
 
Baada ya kuona malalamiko ya hii kodi ya 2000/- nikakumbuka council tax UK ni kama alivyosema huyo mTz wa UK ni kama Β£1300 hivi kwa mwaka kwa nyumba za kawaida kabisa. Ila Tz na UK ni tofauti kila nyanja.
Baada ya kusema hayo niseme tu 2000/- kwa mlipa kodi sio nyingi labda kama wengi wasemavyo matumizi yake ndio yanawafanya wajisikie vibaya kulipa kodi. Sasa ni wakati muafaka tuiwajibishe serikali na matumizi ya hela zetu.
 
Mwambie aje huku ajue bei ya dagaa mpaka sukari kama hatarudi tanzania
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…