Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,577
- Thread starter
- #201
Nina Hamu ya kusikia majibu ya CCM Kuhusu mambo yaliyoibuliwa kwenye wasilisho hili ambalo kwangu ndio bora kabisa katika mchakato wa katiba .......
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba watu waache kuingia katika propaganda za CCM za kutumia 'wengi na wachache'' Huu ni uopotoshaji mkubwa. Shamsi Nahodha hana 2/3 katika kamati yake, anapata wapi wengi na wachache''MAONI YA WENGI, MAONI YA WACHACHE''
MBINU CHAFU ZA UPOTOSHAJI
Katika bunge la katiba linaloendelea, kamati mbali mbali zinatoa maoni kuhusu mitazamo yao.
Hadi majuzi ni kamati mbili tu zilizokuwa zimepata muafaka wa 2/3 kutoka pande zote.
Ni pande zote kwasababu Tanganyika haina mwakilishi, inawakilishwa na Tanzania ambayo znz ipo, huku Zanzibar ikiwa na uwakilishi wake.
Kwa mtazamo huo tu utaona jinsi ambavyo Watanganyika hawana mahali pa kushika au utetezi.
Muhimu hapa ni kuwa pamoja na mazingaombwe hayo 2/3 haikupatikana.
Kutopatikana kwa 2/3 kuna maana moja, suala la vifungu 'cha kwanza na sita' hayana ufumbuzi'
Katika kuliendesha bunge kibubusa busa Mh Sitta ameamua kamati zianze kuwakilisha maoni yao.
Kuna jambo watu wengi hawalioni kama upotoshaji. Kila anayesimama na kuwakilisha mawazo husema ''maoni ya wengi au maoni ya wachache'
Hii ni hila na mbinu ya CCM kuwalaghai wananchi kuwa kuna majority na minority.
Kwa taratibu za upigaji wa kura huwezi kusema maoni ya wengi ikiwa huna 2/3 kutoka pande zote. Kamati ambazo hazina 2/3 ya pande zote hazifai kabisa kusema kuna maoni ya wengi. Utakuwaje na maoni ya wengi wakati huna 2/3?
Mfano kama wajumbe wa 'Tanzania' wakiwa 30 na wakapiga kura na kupata 2/3 hiyo maana yake ni 20 kati ya 30.
Hawa hawatoshi kupitisha vifungu hadi wajumbe wa znz waridhie kwa 2/3.
Kama wajumbe wa znz ni 24, 2/3 yao ni 16 na hao lazima wapatikane ili kusema 'wengi'.
Hata kama wajumbe wote wa 'Tanzania wakikubali kwa ''3/3'' idadi yao ambayo ni 30 haiwezi kupitisha vifungu hivyo endapo ile ya znz ni 15 au chini ya hapo.
Kwa muonekano wa haraka 2/3 ya Tanzania inaweza kuwa nyingi, hiyo haifanyi 2/3 ya znz kuwa wachache.
Kinachoangaliwa ni 2/3, hata kama wznz katika kamati ni 9, 2/3 yao ni 6.
Hao wznz 6 wanaweza kukwamisha vifungu vilivyopitishwa na 3/3 ya 'Tanzania' ambao ni 30.
Siyo sahihi na ni upotoshaji wa makusudi kabisa wa kutumia lugha kwa kusema maoni ya wengi na maoni ya wachache.
Mkakati huu umelenga kuvunja nguvu za kisheria za 2/3 kwa neno 'wengi na wachache'.
Wananchi na wabunge wakatae hila hizo.
Kinachopaswa kusemwa ni hivi ' maoni ya kundi moja yanasema ABCD, maoni ya kundi la pili yanasema ABCD'
Nashangaa sana hata wale wenye hoja wanakubali kuitwa wachache wakati hakuna uchache.
Kwa kwamisha vifungu kwa 2/3 ni nguvu na wingi.
Narudia hata kama wachache wapo 6, 2/3 yao ni 4, hao ni sawa na 100 ambayo 2/3 yao ni 66. Hatuwezi kudharau hao 4 kwasababu kanuni zinasema lazima kupatikane 2/3 ya pande zote.
Hata katiba na ndani ya bunge la JMT, wznz ni 81 na 'Watanzania' ni takribani 240.
Sheria na kanuni zinasema, jambo la muungano lazima lipate 2/3 ya pande zote.
Haisemi wengi au wachache.
Sitta akiwa Spika hakuwahi kutumia neno wachache kwa wazanzibar ndani ya bunge la JMT, leo anaanzia wapi kama si ulaghai na hila zake akitumiwa na CCM.
Huu ni mtego wa kuonyesha umma kuna wengi na wachache wakati ukweli si hivyo.
Wajumbe kuweni macho.
Mkuu duh,upo macho kweli.....
....Naunga mkono hoja ubeberu na ukabaila wa tibii haukubaliki
Mkuu duh,upo macho kweli..
NI PM email yako basi.
I am truly enjoying this. Kwa miaka mingi 'wapinzani' walitaka Hati ya Muungano iwe sheria mama hata juu ya Katiba. Sasa wanasema ni batili, na CCM Ndio watetezi wake sasa. Tume na Warioba inatambua Hati hiyo kama chimbuko la serikali tatu na msingi wa Katiba; Lissu: mara ni batili, mara ndiyo msingi wa kutaka Tanganyika sasa maana Hati iliipa uhai. Mara Hati haikusainiwa na yaliyomo hayajulikani, huku anataja mambo yake 11 ya Muungano, na mara Jumbe anathibitisha kuwa Nyerere alisafiri Z'bar na Wawili wale wakasaini huko. I agree it is brilliant, like glass; and just as brittle.MAONI YA WAJUMBE WALIO WA WACHACHE KATIKA KAMATI NAMBA NNE KUHUSU SURA YA KWANZA NA SURA YA SITA YA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
[Kanuni ya 32(4) ya Kanuni za Bunge Maalum, 2014]