Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Hatuwezi kuwakwamua masikini kwa kukalia utajiri wa nchi - Mpango.

Maoni yetu.

Hakuelezea madini na ubinafsishaji wote tangia tupate uhuru kwanini haujatukwamua kutoka umasikini wa kutupwa
 
Jambo kubwa la kitaifa ni lazima watoe maoni yao na serikali kuwa sikivu - Mpango
 
Mikataba mitatu inayosainiwa leo imezingatia maoni ya wananchi kwa kiwango kikubwa- Mpango
 
Serikali inatekelezq ilani ya uchaguzi ya CCM inayoelekeza ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kuharakisha maendeleo ya nchi - SSH
 
Mikataba 3 iliyosainiwa imezaliwa kutokana na mkataba mama uliyoleta maneno mengi - SSH
 
Alishukuru bunge na baraza la mawaziri kwa ushauri wao na kuupitisha mkataba huu- SSH
 
Ampongeza Mwanasheria mkuu, uongozi wa bandari, Falme za Kiarabu, DP WORLD - SSH
 
Bandari ya Dar ni lango la biashara, utajiri wetu na ni huduma kwa majirani yetu - SSH
 
Upo ushindani Mombasa, Beira n.k wateja wanayo haki ya kuchagua huduma bora SSH
 
Wapo wanaona sisi wenyewe tunao uwezo wa kuziendesha lakini tutachelewa sana - SSH
 
Maoni yetu.

Hii mikataba 3 tunalishwa maneno ya kuwa maoni yetu yamezingatiwa ukiondoa swala la kulinda ajira hakuna lililotajwa ya kuwa limezingatiwa
 
Maoni yetu.

Bila ya hiyo mikataba 3 kuwekwa hadharani hatuna namna ya kujua geti na 3-7 nini kitaendelea.

Hatujui uwekezaji wa WB wa zaidi ya $420 Mill tutafidiwa vipi na huyu mwekezaji hasa ukizingatia huu siyo ubia
 
Mwekezaji kulipa kodi na ipo haki ya kuvunjwa mkataba lakini hatujui ni kwenye mazingira yapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…