Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Lakini yaelekea nchi ya viwanda huishia kwenye majukwaa tu
 
Kama tungekuwa makini ya kujenga nchi ya viwanda kodi zote ziwe VAT, REA na EWURA tungelizifuta na kupunguza bei ya umeme
 
EWURA haina umuhimu wowote ule na jukumu lao kubwa huwa ni kutubebesha zigo la gharama za maisha
 
Kuongeza bei ya kiwese ndiyo jukumu wanalolifanya. Sasa kwanini warudi kutukamua tena kwenye kodi za umeme na maji ili walipane mishahara minono na marupurupu kibao
 
Kuna anayejua kwanini mishahara na marupurupu ya EWURA yatungiwe sheria ya kodi?
 
Kuna anayejua kwanini tusifute EWURA na majukumu yao kufanywa na TPDC?
 
Mbali ya kukosa ubunifu wa kupunguza gharama za nishati na maji na hivyo kuwa mzigo kwa wazalishaji na kupunguza ajira za vijana EWURA pia wanao ufisadi mkubwa wanaoufanya kwenye uagizaji wa kiwese kwa kuleta ukiritimba wa BULK SUPPLIERS ambao wamekuwa monopoly na kupanga bei iliyo juu ya bei ya soko la dunia
 
Wamiliki wa bulk suppliers ni wahindi ambao wanaagiza kiwese kutoka India ambako hawazalishi kiwese na kuongeza gharama za mafuta kwetu
 
Sasa kinachoendelea tunalipa ufisadi wa EWURA na kuipatia India soko la mafuta ambayo hayazalishwi kwao bali huagizwa kutoka Urusi tena kwa punguzo la dola za kimarekani 30 kwa kila pipa na hiyo nafuu hata sumni sisi hatupewi
 
Uongozi mzima wa EWURA hauna sifa ni fadhila za kisiasa tu kwa gharama zetu
 
Tumekuwa tukiwauliza EWURA wanakwama wapi kuagiza mafuta moja kwa moja kutoka Urusi?

Kwanini hawatujibu?
 
Kesho tutaiangaza Bodi ya mikopo ambayo nayo tutashauri ifutwe ni mzigo kwa taifa
 
Sheria ya mafao ya wenza wa viongozi wa kitaifa ni ya kifisadi na inakuika katiba kwa kufuta usawa miongoni mwa jamii na kutanua mafao tajwa isivyo halali na kinyume cha sheria!
 
Huwezi kumlipa mafao ya ustaafu mtu ambaye hujamwajiri!
 
Msingi wa mafao ya kustaafu ni mshahara sasa kama hana mshahara aliostaafu nao unatumia vigezo vipi kutumia mshahara wa mwajiriwa kumlipa mafao asiye mwajiriwa na kwanini unaleta ubaguzi kwenye utumishi wa umma?
 
Tunachoona hii sheria ya mafao ya wenza wa viongozi wa kitaifa itachochea misuguano kwenye jamii
 
Pia tunaona kasi ya ajabu ya kutunga sheria za kuwakamua wananchi kodi
 
Back
Top Bottom