Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #701
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli kiwese cha urusi kinahitaji kuchakatwa kabla ya kutumika. Lakini tunachoamini EWURA kama wangekuwa hawabebwi leo uwezo wetu wa kuchakata mafuta ungelikuwa mkubwa na tungeachana na uagizaji wa mafuta yaliyochakatuliwa kutoka India.Nilisikia Urusi wanatoa crude oil na hapa kwetu hakuna uwezo wa kuyachakata mkuu naomba nipate elimu hapa..
Hii Nchi ni ngumu sanaa... sijui lini wezi watakomaNi kweli kiwese cha urusi kinahitaji kuchakatwa kabla ya kutumika. Lakini tunachoamini EWURA kama wangekuwa hawabebwi leo uwezo wetu wa kuchakata mafuta ungelikuwa mkubwa na tungeachana na uagizaji wa mafuta yaliyochakatuliwa kutoka India.
Bulk supplies ni utaratibu wa kifisadi na EWURA wanauendeleza kwa sababu baadhi yao wako kwenye payroll na kwa vile wao hawaathiriki hawana msukumo wa kubadilisha.
Hivyo kutokana na huu udadavuaji ni dhahiri EWURA wanyimwe kodi utaona sera zitakavyobadilika na kuwa chombo cha usimamizi chenye kujitegemea.
Tunakiri upo uwekezaji umeanza wa kuchakata lakini ni mdogo na hauwezi kupunguza mzigo wa kuibeba EWURA na kupunguza bei ya kiwese kwa walaji kwa sababu unategemea wawekezaji kutoka nje eneo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu.
Kwa nchi inayojenga uchumi wa viwanda ungelitegemea uwezo wa kuchakata kiwese upo mikononi mwa umma kuondoa bei za kupangwa ambazo zitakwamisha nia ya serikali ya uchumi wa viwanda.
Bila bei poa ya nishati zote uchumi wa viwanda ni vuvuzela la majukwaani tu.
USHAURI
Warusi wako tayari kuisaidia Tanzania kujenga uwezo wa kuchakata mafuta tatizo au kikwazo chetu uwezo huo utamaliza ufisadi wa bulk suppliers ambao unawatajirisha watendaji ndani ya EWURA na Wizara ya nishati.
Sasa tuamue ama zao au zetu.
Ugumu wa kutatua hii kero ni ukosefu wa utashi wa kisiasa tu kwa sababu vyeo serikalini hutolewa kama fadhila tu siyo wenye uwezo wa kutatua kero!
Ukiona wanaiba kura ujue hawatakoma kuiba hiyo ndiyo laana yaoHii Nchi ni ngumu sanaa... sijui lini wezi watakoma