Hii ni Iringa na baridi lazima ufunge milango na madirisha. Sasa hawa usiku huo waliamua kujifungia na kugalagalazana sakafuni. Hawakujua jiko la mkaa linatumia hewa na oksijeni na kuachia carbon monoxide ambayo haina harufu na inaua. Waliendelea na starehe yao hadi mauti ikawakuta. Asubuhi wateja walishangaa mbona hafungui. Wakachungulia wakawaona wako watupu wamelala. Wakaita polisi ambao walivunja mlango wakawakuta wamekufa kwa kuvuta carbon monoxide ambayo hawakajua inatokana na makaa yaliyokuwa yakiwapasha joto. Wote ndoa zao waliziweka kando siku hiyo. Sina uhalika kabla ya mauti walipanga kulala hapo hadi asubuhi. Ninahisi ilikuwa chapuchapu waishie.