Israel kitu anachokitaka ni kuwa siku moja naye awe Superpower, hivyo katika mikakati yake ni pamoja na kujitanua kijiografia, na kuwaondosha wale waliyokuwa tishio kwa usalama wake kuwa karibu naye na kuhakikisha huwa hana kigugumizi katika kujiendeleza kiuchumi, miongoni mwa miradi yake mikubwa ambayo anataka kutengeneza ni Ben Gurion Canal ambayo itakuwa mshindani wa Suez Canal. Egypt anaonekana kama mkatili kwa kuwazuia wakazi wa Gaza wasiingie kwake ni kujua kuwa ikiwa Israel watafanikiwa kuichukua Gaza basi Suez Canal inakwenda kufa na uchumi wa Egypt unakwenda kuathirika pakubwa tu.Israel bhana wana majivuno. Sasa wanawaamuru wapalestina 1.1 Mill waondoke Gaza.
Swali la kujiuliza wao ni akina nani?
Gaza sasa ni sehemu ya Israel au nako huko wanataka kuanza ujenzi wa makaazi haramu kama kule West Bank?
Hivi vita vya Palestine watu wengi wanadhani ni vita vya kidini, kama wanavyoaminishwa na wengi lakini ni vita vya kiuchumi zaidi.