Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Haya mabenki sijui WB na IMF hayakundwa kutatua kero zetu bali yaliundwa kututumia sisi ili kutatua kero za nchi zao
 
Ndiyo maana ushauri wa haya mabenki haujawahi kutusaidia bali umesafishia njia makampuni ya nchi zao kuzishika njia kuu za uchumi
 
Hebu tungalie kijuujuu tu sera nzima ya ubinafsishaji ambayo matutusa ndani ya CCM hujivunia ni ilani yao ya uchaguzi
 
Sera hii ilizaa lukuki ya sheria za uwekezaji ambao makampuni ya nje yametajirika na kutuacha sisi umesikika kuongezeka
 
Pamoja na kuwa na sheria za uwekezaji na kuwamilikisha mamluki njia kuu za uchumi bado serikali chanzo chake kikuu cha mapato ni raia badala ya kuwa ni wawekezaji!!!!!!
 
Sasa kama wawekezaji hawana mchango wowote kwenye ujenzi wa nchi tuna msukumo upi wa kuendelea kuwa nao?
 
Kigugumizi cha kuzifuta sheria za upendeleo kwa wawekezaji kinatoka wapi kama siyo hongo wanazopewa watawala?
 
Tungependa kuangazia upungufu mkubwa wa taarifa ya CAG
 
Taarifa zote za CAG zina dosari moja kubwa zinafukuzana na matukio badala ya kubainisha vyanzo vya hayo matukio
 
Taarifa za CAG zote alizowahi kututaarifu hazina mashiko kwa sababu hazitaji ufisadi unachochewa na nini!
 
Taarifa za CAG kama hazina mamlaka au uwezo wa kuchangia vyanzo vya ufisadi sasa vina msaada upi kama lengo lake ninkutupasha habari ya jinsi nchi ilivyogubikwa na wezi, wabadhirifu na wala rushwa kubwa kubwa
 
Taarifa za CAG zilipaswa kuanisha mfumo ndiyo chanzo kikuu cha ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka ya umma na wizi
 
Taarifa za CAG zilipaswa kubainisha mfumo huu unazalisha uwakilishi haramu na kuleta m'mom'monyoko wa uwajibikaji
 
Taarifa za CAG zilipaswa zibainishe katiba irekebishwe hususani maeneo ya tume ya uchaguzi
 
Taarifa za CAG zingesema sheria za uchaguzi zinachochea uwakilishi haramu
 
Bila ya kuufuta uwakilishi haramu hatutaweza kupambana na ufisadi
 
Jukumu la kupambana na maovu kwenye jamii huanza na mchakato wa kuwachagua viongozi bora
 
Sasa kama wakati wa uchaguzi wagombea wanajigamba wataunda serikali hata kama hatutawachagua ujue lengo lao kuwepo serikalini ni kwenda kuiba mali ya umma hawana jipya. Sasa hawawezi kukemea maovu kama Sokoine tunda la uwakilishi halali
 
Back
Top Bottom