Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Kamati ya uteuzi siyo sahihi kuundwa na Majaji, wanasheria na wateule wengine wa Rais kwa sababu uchaguzi siyo kesi inayotakiwa kuamuliwa
 
Kwa huu, mfumo wanaojaribu kuujenga baada ya uchaguzi ikawa kesi utarudi kwa hawa hawa waliovuruga uchaguzi kukusuluhisha?
 
Maana ugomvi huanzia kwenye uteuzi wa makamishina walitoka CCM sasa jaji mkuu aliyeratibu zoezi la kuwaajiri makamishina ataamua kesi yake mwenyewe?
 
Tunashindwa kuelewa mapungufu ya rasimu ya marekebisho ya katiba iliyopendekezwa na Warioba bado mnayakumbatia kama walikuwa sahihi mna matatizo gani?
 
Kila chama cha siasa kimchague mwakilishi wake ambaye atachaguliwa na mkutano mkuu wa chama chake kwa minajili hiyo tu na asiwe mwajiriwa serikalini au ana wadhifa wowote ndani ya chama cha siasa
 
Sasa tukiisha wapata hawa wajumbe wakae wamchague Mwenyekiti wao na wataajiri secretariat yao na kujiundia kanuni za kuwaajiri makamishina wa tume ya uchaguzi na jinsi ya kuendesha uchaguzi huru na haki kwa wapigakura
 
Tume huru ya uchaguzi kamwe haiwezi kuundwa na wateule wa Rais maana kwanza hawatawajibika kwa wapigakura bali watawajibika kwa Rais aliyewateua
 
Rais awe anateua makamishina wa Tume ya uchaguzi kutokana na mapendekezo ya kamati ya kusaili inayoundwa na wawakilishi wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa
 
 
Back
Top Bottom