Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Uchimbaji wa makaa ya mawe umebuma mwekezaji anataka aondoke nayo bila kutuachia hata sumni.

Na hawa mazezeta wetu wako bize wanajadili mgao wao
 
Uchimbaji wa simenti Tanga umekwama kisa mwekezaji hataki kuchangia uchumi wa nchi hii
 
Na watawala wanaona ganda la muwa la jana ni fursa ya kukata kidali chao
 
Sheria za kuwabagua wawekezaji kutoka nje wasilipe kodi zinalenga kutoa mwanya wa watawala kudai hongo
 
Huwa tunauliza mtupe takwimu tangia Orthello apewe Loliondo mchango wake kwenye bajeti ya serikali kila mwaka uko wapi?
 
Huwa tunauliza mchango wa wachimbaji wakubwa wa madini kwenye bajeti ya serikali uko wapi?
 
Tunachoona ni kasi ya kukopa madeni ambayo kila mmoja wetu anajua hayalipiki
 
Tunachoona ni vuvuzela la wataalamu kudai mzigo wa madeni unabebeka lakini hawatuelezi wametumia vigezo vipi kuhitimisha hivyo
 
Tunachoona majukumu ya serikali kama afya, elimu na miundombinu tunabebeshwa sisi tusiyo na hatia
 
Tunachoona watawala kila kukicha wanatunga sheria za mafao ya kuboresha hali zao huku kikotoo cha wanyonge kikiendelea kubinywa
 
Tunachoona watawala kila kukicha wanajipandishia kimya kimya mishahara na marupurupu huku ya watu baki inaendelea kudumaa
 
Tunasema sheria zimetumika visivyo na kujenga matabaka ya matajiri na masikini
 
Tozo, mifuko ya bima ya afya na bodi za mikopo ya elimu ni ushahidi watawala kazi imewashinda
 
Sheria za kodi, masilahi ya watawala, wawekezaji, Bima ya afya, Miundombinu na bodi ya mikopo ya elimu kwa pamoja zinajenga tanuru za vita vya wenyewe kwa wenyewe
 
Back
Top Bottom