Juice world
JF-Expert Member
- Jun 7, 2022
- 1,982
- 2,706
Katika hii nchi ukitoa Rais, watu wanaofuata kupigiwa magoti ni askari na hawa jamaa huwa wanafanya walitakalo na hii imethibitika katika vitu vingi sana.
Yaani kiufupi hao jamaa waliotuhumiwa kubaka na kulawiti hawatofungwa na wataishi maisha ya uraiani na kazi hawatofukuzwa sababu ni watu muhimu sana.
Sasa naona wabongo wanadanganyana sana eti watafungwa hivi si mliambiwa kesi ni siku tano haya mpaka leo siku tano si zimeshaisha Jana eti Kuna wakili kajitokeza kufungua kesi dhidi ya mawakili wanaowatetea MAAFANDE imepelekea kesi kusogezwa mbele mpaka kesi ya mawakili isikilizwe.
Hivi watanzania Kwa akili ya kawaida tu hamuoni kama hapo hamna kesi ya MAAFANDE yaani kesi imetoka Kwa maaafande imehamia kwa mawakili.
Cha kushauri tu mkae mkijua MAAFANDE watarudi uaraiani hii sio Tanzania ya magufuli na kesi hamna ipo hivyo yaani na majamaa yanadharau kweli kama yenyewe ndio wanaume pekee Tanzania.
Pia soma>> Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani