Maoni yangu juu ya rasimu ya mitaala na Sera ya elimu 2023

Wilson Gamba

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2013
Posts
808
Reaction score
878
Kama mtanzania nimepitia na kuisoma kwa umakini kujua nini kimo maana elimu ndo Kila kitu katika taifa lolote maana ndo jiko la wataamu wenye chachu ya kuleta maendeleo ya nchi.

Nawapongeza Ila maoni yangu ni Kama ifuatavyo;
1. Kwenye Sela ya elimu lugha ya kujufunzia ni Kiswahili kwa shule za awali na msingi kwa zile za serikali na kiingereza kwa zile zinazotumia mfumo wa kiingereza. Maoni yangu apa ni bora lugha ingekuwa moja kwa shule zote yaani kiingereza ndo kitumike na Kiswahili lifunzwe tu kama somo ili kuepuka kuendelea kuwachanganya watoto kwani wakifika sekondari kwa mjibu wa Sera hii ya elimu pendekezwa mtoto ataitaji kutumia kiingereza katika kujifunza kwa masomo yote isipokuwa Kiswahili na historia ya tanzania.

2. Kuhusu masomo ya darasa la kwanza/ awali ningependekeza mtoto aweze tu kumudu stadi tatu tu yaani kuhesabu, kusoma na kuandika ili kumwezesha kumudu vizuri zaidi lugha na atumie pia kiingereza Kama nilivyoshauri apo juu, pia Kama Kuna ulazima Sana anaweza pia kusoma science ya mazingira yake.

3. Na ili hili liweze kufanikiwa nashauri walimu waendane na ratio ya watoto ili kuwamdu vuzuri yaani mwalimu awe na watoto wachache ili awamudu sasa hapa kwa darasa la awali na la kwanza.

Ushauri wangu ni huu kwa mtizamo wangu. Kwa ujumla kama ikisimamia vizuri ni nzuri sana.

Zaidi, soma: Rasimu ya Mitaala Nchini: Umri wa kuanza darasa la kwanza ni miaka 6, elimu ya msingi mwisho darasa la 6
 
Naileta kwenu kama nilivyopokea.

MAPENDEKEZO YA RASIMU YA RIPOTI YA KAMATI YA KITAIFA YA MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU* .

Na Baltazari Luhanga.

1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.

31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

32. Walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa Wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada
(cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.

33. Vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.

34. Kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe
na umahiri zaidi. Kisha walimu watapata leseni.

35. Mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.

36. Kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.

37. Bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.

38. Utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. Hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwasababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. Utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.
 
Watafanya yote wakisahau Walimu watarudi tena square one.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom