(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii na sheria za nchi;
(b) ni mwenye akili timamu;
(c) angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa
Jamhuri ya Muungano;
(d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini;
(e) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii;
(f) anayo angalau shahada ya kwanza ya chuo kikuu
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;
(g) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha
siasa au mgombea huru;
(h) sera zake au sera za chama chake si za mrengo wa kuligawa
Taifa kwa misingi ya ukabila, udini, rangi au jinsia;
(i) ni mwadilifu na anafuata maadili ya Taifa;
(j) mwenendo wake binafsi hautiliwi shaka na jamii;
(k) hajatiwa hatiani kwa kosa lolote la jinailinalohusu kukosa
uaminifu; na
(l) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi
Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa
kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
HAPO PENYE RED KUHUSU IBARA YA 75 RASIMU YA KATIBA JUU YA SIFA ZA MGOMBEA URAIS NDO NDO HASA MAKUSUDI YA THREAD YANGU MAANA SIJUI KWA HAWA WAGOMBEA AMBAO NI VIONGOZI WA KIROHO WATAJITETEA VIPI KWA HILO