Maoni yangu katika rasimu ya katiba 2013: viongozi na waliokuwa viongozi wa dini wasiwe wagombea

mkuu, waache viongozi wa kiroho wamtumikie Mungu na wanasiasa wafanye siasa
Mbona kilio chenyewe tunakisikia sasa hivi ambapo viongozi wa Kiislamu nao kutokana na rasimu mpya wanaweza kuingia bungeni kama wagombea binafsi?!

Ulikuwa wapi wakati kina Msigwa,Lwakatare na wengineo wakiingia bungeni?
 

Basi pendekeza wapagani tu ndio wagombeee uongozi nchi hii.Elewa udini ni hulka na inaweza kuingizwa na yeyote mwenye mrengo huo, ukitaka kuelewa zaidi msikilize shehe mkuu wa Dar mitazamo yake kunapotokea mikanganyiko ya kidini husimamia ukweli na haki.Viongozi type hiyo wanaweza kuongoza jamii mchanganyiko na kutoa haki bila upendeleo kwa dini yake.Suala lililopo nchini ni product ya mambo mengi ikiwepo kutowajibika,kutofuata sheria na taratibu,kulindana n.k yote hayo kwa ujumla wake yameleta hicho unachokiogopa.Tungekuwa ma uwajibikaji yeyote anaeleta hiyo migawanyiko sheria ingenyoosha.Na watu wangfuata dira ya taifa,sasa kila mtu anafanya lake kutokana na mfano unaooneshwa na viongozi.
 

nani kakwambia? Kwakua amepita mtakatifu nyerere sasa unataka aje na mtakatifu padri slaa? Hapana haiwezekani.
 

Dini si muhimili wa nne wa dola hivi kuipa mamlaka ya kutoingilia mihimili mingine. Na pia kila mmoja ni kiongozi katika dini yake maana kwa maisha ya dini unawaongoza wengine ili waige mfano wako na ukiweza unawashawishi ili waingie dini yako...ni kiongozi mwenye majukumu hayo. Dini zitabaki lakini mwenye misimamo ya dini zake asituletee fujo sisi tusiokuwa wa dini yake. Hao ndiyo viongozi tunaowataka. Tayari tumewaona baadhi ya viongozi waliotulazimisha kuvaa hijabu maofisini eti ndiyo kuwa waungwana...na hadi dressing code ikaundwa haraka haraka. Wapo waliotenga vyumba vya wizara kuwa nyumba yao ya ibada, wapo waliochukua fedha za serikali na kupelleka kwenye nyumba zao za ibada...hawa ndo tuwakatae lakini ukipata kiongozi asiyewadini yako na akakuheshimu kwa staili ya Ruksa juu ya nguruwe...kama alivyowahisema mzee Mwinyi...anayetoa tamko la kula nguruwe ni ruksa...! Kiongoziasiyetetea dini yake kwa vile ni wa dini hiyon n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…