OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Wakubwa wenzangu tuache kujadili ulimbukeni wa jamaa zetu kwenye mashindano ya CAF, tujadili mambo ya msingi.
Clatous Chama amekuwa akipangwa winga huku Saido Ntibazonkiza akitumika kama kiungo wa kushambulia nyuma ya mshambuliaji wa kati.
Chama amekuwa akionyesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho (assists) kulinganisha na Saido ambaye ameonyesha uwezo wa kufumania nyavu pindi anapopata fursa.
Kitendo cha kumpanga Chama pembeni kinaonekana kuipunguzia Simba idadi ya pasi za mwisho jambo linaloonekana kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa kati ambao wamekuwa wakipangwa, hivyo pengine Robertinho angejaribu kumtumia Saido winga na kumrudisha Chama acheze namba 10.
Maoni yangu ya kitaalamu ni hayo kuelekea Jumamosi kwenye fainali yetu. Wewe maoni yako ni yapi.