Maoni yangu kitalaamu kuelekea "fainali" dhidi ya Horoya

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wakubwa wenzangu tuache kujadili ulimbukeni wa jamaa zetu kwenye mashindano ya CAF, tujadili mambo ya msingi.

Clatous Chama amekuwa akipangwa winga huku Saido Ntibazonkiza akitumika kama kiungo wa kushambulia nyuma ya mshambuliaji wa kati.

Chama amekuwa akionyesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho (assists) kulinganisha na Saido ambaye ameonyesha uwezo wa kufumania nyavu pindi anapopata fursa.

Kitendo cha kumpanga Chama pembeni kinaonekana kuipunguzia Simba idadi ya pasi za mwisho jambo linaloonekana kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa kati ambao wamekuwa wakipangwa, hivyo pengine Robertinho angejaribu kumtumia Saido winga na kumrudisha Chama acheze namba 10.

Maoni yangu ya kitaalamu ni hayo kuelekea Jumamosi kwenye fainali yetu. Wewe maoni yako ni yapi.
 
Horoya niliwaona ile game ya kwao, hawakuwa na makali ya kutisha, tukiwashambulia mfululizo watalegea, magoli yapo, siombei nao waokolewe na kipa wao kama Vipers.

Chama sio winger, kuna wakati naona afadhali kocha atumie mfumo wa 4-3-3 huu, ndio mfumo Simba Sc waliouzoea kuleta matokeo na timu kucheza kwa kushambulia.

Inawezekana kocha akawa na mbinu zake kichwani, lakini kumchezesha Chama asiye na nguvu na spidi ya kutosha kama winger kunapunguza mashambulizi ya timu, amrudishe Chama nyuma ya Phiri, peleka Saido pembeni, timu itaamka.
 
Umesema vyema

Sent from my Infinix X689C using JamiiForums mobile app
 
Mimi ushauri wangu tumlete yule mganga wetu kutoka Pemba, na pia yule mama mganga wa Moro mwenye titi Moja tumlipe Ile Hela yake tuliyomzurumu ili magoli yarudi pale Kwa Mkapa. Tusipofanya hivyo haki ya Mungu hatutoboi.
Simba ngufu moya[emoji123][emoji123]
 
Inawezekana kocha akawa na mbinu zake kichwani, lakini kumchezesha Chama asiye na nguvu na spidi ya kutosha kama winger kunapunguza mashambulizi ya timu, amrudishe Chama nyuma ya Phiri, peleka Saido pembeni, timu itaamka.
Hili mimi linanishangaza, naona kama kocha anatukwamisha
 
Ww una utaalam upi!!?? Hujawahi kukochi hata timu za chandimu. Punguzeni midomo yenu mirefu na dharau. Tz sasa hv kuna timu moja tu Jangwani. Na kwa taarifa yako huu ni mwanzo tu.
Mleta mada amesema tujadili kitaalamu wewe unamshambulia mleta mada,hii ni haki kweli au hujaelewa uzi unataka nini?
Amesema ni maoni yake,wewe maoni yako ni yapi?
 
Ukabaji WA chama na ntibanzokinza ikoje!?..na Kasi yao ya ku-react mpira ukipotea!?..nachojua chama ni konokono
 
Mi naona Chama aende Azam tu maana Simba imebaki jina na kujaza wazee kina Boko na Onyango, pale anaua kipaji chake tu na Yanga atakaaa benchi Hana kiwango tunachotaka . Chama Yuko slow sana na hakabi! utopoloni Hatuna falsafa ya slow slow na tunakaba timu nzima kama ugomvi!

Hilo la kudiscuss mchezaji Gani apangwe Namba ngapi ni kupoteza muda tu Simba ni mgonjwa mahututi hachagui dawa yoyote Wala daktari Wala kitanda Wala sindano adungwe wapi na nani saa ngapi iwekwe dawa Gani Ili iwe Nini na Kwa faida Gani!
 
Ww una utaalam upi!!?? Hujawahi kukochi hata timu za chandimu. Punguzeni midomo yenu mirefu na dharau. Tz sasa hv kuna timu moja tu Jangwani. Na kwa taarifa yako huu ni mwanzo tu.
Hawa viumbe ndiyo maana wanaitwa mbumbumbu.

Ujuaji tu umewajaa. Kajitu kamekula ugali wake na maharage! Baada ya kushiba, kanajiona kameshakuwa na kenyewe ni kakocha ka viwango vya Robertino!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…