MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
BIASHARA YA KUAGIZA CHINA
Leo nimeona nitumie haki yangu ya kikatiba chini ya ibara ya 18 kifungu cha kwanza kuhusu uhuru wa kutoa maoni. Nitazungumzia kuhusu hii biashara ya kuagiza vitu China na kuviuza Tanzania. Maoni yangu haya yanatokana na uzoefu wangu kwenye aina hii ya biashara. Pia nimeona ni wakati sahihi wa kutoa haya maoni baada ya kusikitishwa na wimbi kubwa la matapeli wanaowaliza watu hasa wanawake.
Kwanza kabisa tukubaliane hii biashara ni nzuri inalipa kwasababu nchi zetu hazina viwanda hivyo kila kitu kinatoka nje hasa China. Ni biashara ambayo ukiifanya kwa makini itakutoa kirahisi zaidi. Tanzania pamoja na changamoto zake za tozo na mambo mengine ila bado kibiashara ni sehemu nzuri kwasababu ya wingi wa watu. Watu zaidi ya milioni 60 ni wengi hivyo huwezi kosa kabisa wateja. Cha muhimu cheza na BEI pamoja na UBORA wa vitu unavyoagiza.
Baada ya wajanja kugundua Tanzania panalipa ndo kukatokea watu wanaowaagizia bidhaa wenzao kutoka China huku wao wakifaidika na "cha juu" wanachoongezea. Ni kitu kizuri na ninawapongeza. Ila kuna wahuni wachache nao wamejitokeza na kuanza kutapeli watu pesa zao walizopata kwa shida. Mitandaoni ni kilio kila kona. Wanawake wakiwa wahanga wakuu wa hawa matapeli. Poleni sana. Binafsi ninajua maumivu ya kutapeliwa. Nilishawahi tapeliwa na mbongo mwenzangu simu aina ya Iphone. Inauma sana kuona ndugu yako anakutapeli LIVE. Kibaya ni kwamba utakuta mtu anatapeli watu kibao na kuwa na kiburi cha hali ya juu. Na wengi wa waanaoagizia watu mizigo hujifanya miungu watu.
Nini maoni yangu ili mtu asitapeliwe au kupunguza hatari ya kutapeliwa? Binafsi baada ya kupata vipigo mara kadhaa kupitia matapeli niliamua kujivika mabomu na kuanza kuagiza mwenyewe. Ingawa haimaanishi kwamba ukiagiza mwenyewe ndo hutakutana na matapeli wa kichina... la hasha. Kuna wachina matapeli pia ila ni wachache kulinganisha na watanzania wenzetu.
Nilichofanya ni ku-install app ya Alibaba kwenye simu yangu kisha kuanza kutafuta vitu mbalimbali nilivyokuwa navitaka. Baada ya kupata na kukubaliana bei basi huwa ninalipia direct kwa mchina kisha nampa address ya msafirishaji ambapo mara nyingi natumia Silent Ocean Ltd. Baada ya hapo mchina hupeleka mzigo kwa msafirishaji na kunitumia picha ya delivery note kuonyesha kwamba mzigo sasa uko Silent Ocean Ltd. Zamani mizigo ilikuwa inafika mapema sana. Ndani ya mwezi na wiki moja unakuwa ushapata mzigo ila baada ya corona hadi leo mizigo kuipata haipungui miezi miwili (siku 60). Ila matapeli wengi watakuambia haizidi siku 45.
Faida na hasara za kutumia huu utaratibu wangu zipo. Unapoagiza online inabidi umakini sana kwasababu pichani kitu ni kizuri lakini kikikufikia ni ovyo. Pia kwenye Alibaba kuna matapeli pia wa kichina hasa upande wa nguo. Unaweza lipia asikutumie mzigo au akatuma vitu vya ovyo. Faida ya huu utaratibu wangu ni kupata vitu kwa bei chini ambayo itakuja kukupa faida kubwa. Kwa mfano hizi pochi zinazouzwa 6000 hadi 8000 kule China huwa ni 2000 hadi 3000. Faida nyingine unakuwa na uhakika wa mzigo kuja kwa jina lako na sio dalali hivyo unajikuta umeokoa gharama za usafirishaji. Kiukweli kuagiza mwenyewe ni bora zaidi. Kuhusu matapeli wa kichina huwa ni nadra sana kutokea. Pia kuna jinsi ya kuwagundua kabla hata hujaagiza.
Mimi nashauri muwe na hiyo App mjiagizie wenyewe. Kama huelewi omba hata mtu wako wa karibu akusaidie. Isitoshe waagizaji wengi nao huingia tu Alibaba na kuwaagizia watu. UOGA WAKO NDO UMASKINI WAKO.