Maoni yangu kuhusu mijadala ya masuala ya dini

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Kumekuwa na mijadala mingi isiyokuwa na Afya kwa masuala ya Dini humu majukwaani. Tatizo la hiyo mijadala ni watu kuleta mada ambazo ni porojo bila ushahidi wowote huku wakiaminisha watu kuwa ni mafundisho ya dini fulani.

NASHAURI: Ili jukwaa lionekane lina wachangiaji wenye maarifa (wasio wajinga); tuchangie mada za dini zile zenye ushahidi kutoka kitabu husika (Biblia au Quran). Mtu akija na porojo zake sijui hadithi imesimuliwa na nani au sijui tamthilia nk nk tumpuuze!

Kwa kufanya hivyo tutaliheshimisha jukwaa kwa kulifanya lionekane lina watu wenye maarifa.,,,namaanisha watu wanaotaka kuujua ukweli na sio WATU WAJINGA WANAO AMINI KILA WANACHOSIKIA!

Kumbuka: Mtandao umefikia watu wengi kwa haraka sana huku ulimwengu wa tatu, hata wale ambao wangehitaji muda kidogo wa kujifunza namna ya kwenda nao hawakupata hiyo fursa.....tuwasaidie!
 
TUMIA AKILI HATA ZA MKE WAKO

Tetesi kivipi?
 
Amini vitabu vyote ila sio kurani,mana mule kumejaa hadithi za sungura na fisi.
 
Hata kwenye Biblia kuna porojo kama za uumbaji. Adam na Eva ni hadithi tu za sungura.
 
Maisha yalivyo magumu niache kutafuta pesa nianze kubishania dini za kigeni? Nitakua mjinga wa mwisho aiseee
 
Mkuu we hujakaa vijiwen. Unafkr kwann story za vijiwez znanoga sana. N kwsbb hazina quotation na mistari. Mf mpige story halafu jamaa aanze zile "mfano warumi sura ya 4 mstari wa22 " vp utaendelea kumsikiliza?
Sema kamba ndo zipunguzwe na tuongee cha uhakika ikiwezekana na vifungu

Japo kuna wengine watasema kifungu na kupindisha tafsiri vile vile
 
Mkuu we hujakaa vijiwen. Unafkr kwann story za vijiwez znanoga sana. N kwsbb hazina quotation na mistari. Mf mpige story halafu jamaa aanze zile "mfano warumi sura ya 4 mstari wa22 " vp utaendelea kumsikiliza?
Sema kamba ndo zipunguzwe na tuongee cha uhakika ikiwezekana na vifungu

Japo kuna wengine watasema kifungu na kupindisha tafsiri vile vile
 
Kwanini isiwe “kila mtu aamini kile anaamini bila kujadili ya mwenzake”?

Maana shida inaanzia hapa mtu siyo Muislam anataka afundishe uislam mtu siyo Mkristo anataka afundishe Ukristo,simple tu amini unachoamini vingine waachie wanaoviamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…