Maoni yangu kuhusu Sakata la DP World kama mtu niliyewahi kufanya kazi kwenye Bandari ya Dar es Salaam

Gharama ni kubwa mno zaidi ya 70T,tsh
 
Safi
 
Na wengi wetu tunalalamikia vipengele vinavyotufunga kwenye mkataba pamoja na ukomo wake. hakuna mtu anaekataa mwekezaji, shida ni masharti magumu na hakuna mlango wa kutokea kama kazi yao itakuwa chini ya kiwango
 
Mdau maelezo mazuri sana .Mungu akubariki.

Hzo changamoto ni common kwa namna yeyote ile aje huyo Dp world au mwingine kama watakuwa na ufanisi angalau matatizo yatapungua.

Yeyote yule akija fresh ishu ni ufanisi kuna storage ni balaa unalipa pesa bila kujielewa unaweza kufikria agent wako anakupiga kumbe kweli,kuna demurrage hizi kutokana na meli kutopakua mzigo ndani ya mda uliopangwa na zinahesabu pesa ndefu haswa ukute berth hamna nafasi kwa vile zingine zinapakua
 
Umeandika vizuri tu, ila kutokana na sensitivity ya Bandari kiuchumi na kiusalama ni vizuri kwanza tukaunda timu ya wabobezi itushauri namna ya kuongeza ufanisi bandarini huku uchumi na usalama ukiwa top priority.

Pia tusitoe mandate ya muwekezaji au port management kuzifikia bandari zingine bila utaratibu utaozingatia terms of reference zitakazowekwa na wataalam wetu.

Ni vizuri strategic planning za rasilimali zetu tuzipange kwa mpango wa muda mrefu at least 20 yrs bila interference yoyote.
 
Mitanzania siyo mizalendo ht uisomeshe mbinguni itaharibu kazi tu!!
 
Na ndege nazo tutakuja kuwapa wageni kama ilivyokuwa hapo mwanzo na mambo yatakuwa mabaya na watu hawataamini.
Yaani ATCL ndiyo ilipaswa kubinafsishwa kwanza kabla ya bandari. Ukitaka kujua sababu yangu linganisha kipindi cha Fast Jet kwenye punctuality na nauli halafu iniambie kama kuwa na ATCL kina tija kwa mwananchi.

Ila kama hujawahi kusafiri kwa ndege huwezi kunielewa, utashangilia tu kuwa na ATCL
 
Inatakiwa mifumo ipigwe bomu ife kabisa ianze upya.
 
DP world kama anafaa hiyo ni sawa, ila vipengele vya kuiuza Tanganyika milele viondolewe
 

unafikiri ni rahisi kiivo mkuu?

Na pia tatizo kuu la nchi yetu ni nidhamu ya kazi na sio elimu.
 
Kama tunashindwa kuendesha bandari basi hatuna serikali , Sawa huenda tumeamua kumweka mwekezaji lakini kama tunaingia mikataba ya namna Ile basi hii nchi imelaaaniwa
Hivi nikitu gani tumewahi kuendesha kwa ufanisi nataka uweke shirika moja la tu, hakuna kazi rahisi kama Bima lakini tumelimaliza. Issue sio serikali sisi wa Tz tunashida katika uadilifu wa kazi sio serikalini tu hata private sector tunashida kubwa. Wewe ukiajiri mtu ujue tu kubali kupigwa. Bandari kuna usumbufu pale utasema unaomba kazi wafanyakazi wanatembea kwa maringo na vitambulisho vyao utasema wameshushwa toka mbinguni. Angalizo tu hakuna serikali yoyote wanaweza ila mifumo ndio inaweza kuwabana au kupunguza urasimu. Sasa issue ya mikataba inasomaje hayo ndio yajadiliwe na lipatikane suluhu, lakini kusema eti tuendeshe wenyewe tutalia. Tulikuwa na UDA ma bus wakepewa wao tu ndio wafanye kazi lakini ufanisi zero wakauwa kila kitu zero profit.
 
unafikiri ni rahisi kiivo mkuu?

Na pia tatizo kuu la nchi yetu ni nidhamu ya kazi na sio elimu.
Mkuu, Nini kinashindikana wakati miaka ya nyuma hasa awamu ya kwanza iliwezekana?
Mbona baada ya uhuru, walitumwa watanzania uingereza kusomea udaktari na waliporudi miaka ya 70, ndio waliokuja kuendeiendesha Muhimbili?
Madaktari 10 wa mwanzo wa taifa kwenye hospitali ya taifa Muhimbili walitumwa kusoma kwa ajili ya taifa!.
Mifano ipo: Dr Chiduo, Dr Kasambala, Dr Kumpuni, Dr Kombe na kina Prof Salungi na wengineo.
 
Sasa hapo tatizo si mifumo ya tra
 
Sasa hapo tatizo si mifumo ya tra
Kote kuna changamoto mkuu, kuanzia TRA mpaka huko TPA .

Na ndiyo maana tunasema wakirekebisha mfumo wa TPA wasisahau wa TRA, TBS , ATMIS na mifumo mingine.

Maana TPA wanaweza wakashusha meli nzima kwa masaa sita TRA wakaja kukukwamisha au TBS

Na mwisho tunasema hatukatai mwekezaji ila pande zote mbili zinufaike
 
Umesema vizuri. Huduma nyingi ni mbovu sana. Na watu wamegeuka miungu watu na kuwa na ukiritimba na urasimu usio na maana bado hatuajaweza kutoa huduma zinazoridhisha.

Sio maji, sio umeme, sio huduma za simu, sio za internet, na mifumo ya hospitali haiwezi kutoa huduma kwa kiwango cha kuridhisha.

Hivyo faida tutakayopata wenye uwezo wakiwekeza kwetu ni pamoja na huduma kutolewa vyema. Kuhusu mkataba hilo sizungumzii leo.
 
Sisi shida yetu ni mkataba mbovu! Ni bora tuendelee kupata huduma mbovu kuliko kusaini mkataba wa hovyo.
 
Cartels za TEC ndo zinanufaika na haya mambo na wezi wachache wanaotaka kutumiq udhaifu huu kuendelea kuiibia nchi yetu fedha na mapato mengi.
 
Sisi shida yetu ni mkataba mbovu! Ni bora tuendelee kupata huduma mbovu kuliko kusaini mkataba wa hovyo.
Mkataba una u hovyo gani? Mnaonesha jinsi gani mnavyotaka nchi hii iendelee kuwa nyuma ili mjinufaishe hapo Bandarini. Mmeula vya chuya. Serikali imeshafanya maamuzi na hakuna kurudi nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…