Maoni yangu kwa serikali juu ya magonjwa yasiyoambukiza

Maoni yangu kwa serikali juu ya magonjwa yasiyoambukiza

MAMDALI

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2015
Posts
221
Reaction score
439
Ningependa nitoe maoni yangu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza nikilenga magonjwa aina mbili kisukari na shinikizo la juu la damu. Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la magonjwa haya hususani kipindi hiki ambapo utandawazi unakwenda kwa kasi. Nimeguswa kuleta huu uzi baada ya kutembelea hospitali x (ya wilaya) na kukuta zaidi ya nusu ya wagonjwa kwenye wodi ni wa kisukari vs hypertension. Nikajauliza kama hali hii ipo huku pembezoni huko mijini hali ipoje? Kwa maana haya magonjwa yanaendana na life style.

Nini kifanyike
1. Serikali iweke mkazo kwenye kutoa elimu afya kupitia media mbalimbali kwa maana ni heri kinga kuliko tiba. Gharama ambayo serikali itakuja kuagiza madawa kutibu magonjwa haya ndani ya maika 30 ijayo in bora ikawekeza kwenye kinga.
2. Ni vyema na sisi wenyewe tukabadirisha mfumo wetu wa maisha kwa maana ya ulaji wa vyakula vya nafaka halisi, kuepuka vinywaji vyenye kemikali, kufanya mazoeza mara kwa mara na pia kujenga mazoea ya kupima afya zetu mara kwa mara
 
Hayo magonjwa kwa sasa si vyakula tu, ila ni maisha magumu na msongo wa mawazo is a big problem. Labda uongelee kansa..
 
Hayo magonjwa kwa sasa yanaletwa na hali mbaya ki uchumi na sio vyakula tu..
 
Back
Top Bottom