Maoni yangu kwenye mechi ya Yanga na USM Alger

Watafungwa tu. Maana Yanga wanacheza mpira wa chini zaidi.
 
Yanga ihakikishe Diarra, Nondo, Baka, Mayele, Musonda na Mudathir wanaanza kazi imekwisha, wengine wajazie tu ifike wachezaji 11!

Huwa sikosei kwenye kuchagua list ya Yanga maana Boli la Yanga nimeanza kulifuatilia nikiwa nasoma vidudu Nyerere akija mkoa mji mzima tunaenda stadium kumpigia makofi na kusema " zidumu fikra za mwenyekiti" , enzi hizo Dunia nzima wasomi Nyerere na Mao tu!
 
Backline ya Yanga iwe makini sana wasipoteze concentration kwani kuna wakati wanapoteza sana umakini kiasi kwamba kama washambuliaji wa timu pinzani wakiwa makini kutumia fursa ni goli tu.

Niliona kwenye mechi yao na Gallants iliyochezwa Dar jinsi mabeki walivyokuwa wakipoteana nyakati fulani lakini washambuliaji wa Marumo Gallants hawakuwa sharp.
 
Kinachofanya kazi ni mbinu. Unacheza mpira mzuri wakati shots on target ni 4-6
Kucheza mpira mzuri haina maana yoyote kama umefungwa
 
Nina wasiwasi sana na nafasi ya Aucho, tuwaombelee Yanga watembee bahati/nyota/upepo wabebe ubingwa wa CAFCCL 2023 na kuiheshimisha TZ.

Mungu ibariki Young Africans, Mungu ibariki Tanzania.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Kwani timu ilocheza na Mazembe ikawapiga nje ndani si ipo? chezesheni hiyoyo mkuu, mkiambiwa mlikutana na mlolongo wa mitimu mibovu hamuelewi, wale ni nusu tu sasa ya wale top 5 wa kule champions league.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…