Maoni yangu: Mbwana Samatta ndiyo basi tena

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
4,830
Reaction score
4,729
Siku nilivyosikia ndugu yetu anaenda Aston Villa FC nikajua ana wakati mgumu sana kwasababu kubwa mbili:

1. Muda ulikuwa umesonga sana, angeenda mwanzo wa msimu angeweza kuonesha makali yake hata timu ingeshuka yeye kama mchezaji huenda angeonekana na kusajiliwa na timu nyingine za ligi kuu.

2. Timu aliyoangukia inashuka daraja; sasa kwa mechi alizocheza sidhani kama kuna timu ya ligi kuu itamhitaji, Aston Villa FC isingeshuka pengine angekuwa na muda wa kuonesha makali msimu ujao na huenda ingekuwa njia ya kupanda zaidi.

Yoye kwa yote nampongeza kwa hapo alipofikia, akaze buti katika mechi zilizo salia huenda akaonekana dakika za lala salama ila kwa hali ya kawaida nahisi ndo imetoka hiyo.
 
Alivyokuwa Genk alisema msimfikirie sana yeye, kuna wanaoweza kuja wakafika mbali zaidi yake.

Kwangu kikubwa naona kaonyesha kuwa inawezekana na kwa kiasi pia tumekuwa kwenye ramani ya soka. Simdai hapo inatosha sana.
Kachukua ubingwa ubelgiji akiwa na mchango mkubwa 23 goals, kacheza ueropa na kafunga goal za kutosha, kacheza uefa kaifunga team kubwa Liverpool. Kacheza epl na kafunga goal moja. Kacheza final carabao Wembley kaifunga goal team bora Man city chini ya Pep.
 
Alivyokuwa Genk alisema msimfikirie sana yeye, kuna wanaoweza kuja wakafika mbali zaidi yake.

Kwangu kikubwa naona kaonyesha kuwa inawezekana na kwa kiasi pia tumekuwa kwenye ramani ya soka. Simdai hapo inatosha sana.
Sema hicho ni muhimu na tunashukuru awamu hii tunang'aa kila sehemu. Hiki ndo kishindo cha awamu ya 5
 
Unaona sasa unataka kuchafua Uzi wako wewe kambale wa kijani
Mkuu usiwe mbishi kama shabiki wa Simba, wewe hujaona maendeleo awamu hii? Mfugale, Ubungo, Reli yakisasa, Laizer kupata Tanzanite, Ndege mpya 11, Hospital mpya, vituo vya Afya, Zahanati, Bandari zote kuboreshwa, Viwanja vya ndege, Kuhamia Dodoma, Mradi wa umeme wa Nyerere, Hifadhi ya Burigi Chato, Meli mpya na vivuko, Maboresho ya miji, Mbwana Samatta, Timu ya Taifa kufuzu AFCON, Tanzania kuingia nchi ya uchumi wa kati, Vidole vimechoka ku type yako mengi.
 
Malizia kabisa kuwa Tanzania imepata yesu mpya
 
Sisi wa huku mpitimbi tunapitwa na mengi aisee ndege zilishafika 11? Magu noma, zikifika 15 tujuze tena
 
Kwenye Afya kuna hospitali 67 na vituo vya Afya 330+ vipya.
Shula kongwe zote zimerudishiwa upya wake
Fly over kila kona
Meli mpya
....
Niendelee Ama nisiendelee
 
Back
Top Bottom