Maonyesho ya Kibiashara-SabaSaba, viwanja bado vichafu!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Nimetembelea leo viwanja vya Saba Saba.
Naleo vilikuwa vinatembelewa na kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais Zanzibar.

Tatizo nililoliona ni lile lile la miaka yote.

Vumbi na uchafu.

Vumbi kutokana na barabara za ndani kuwa na mashimo, na vile vile vumbi kutokana na vifusi.
Cha kushangaza ni kuwa TANTRADE wanakuwa na mwaka mzima wa kujiamdaa, lakini shughuli zinaanza mwezi wa tano au sita.
Mbaya zaidi ni sehemu ya barabara inyopakana na jeshi.
Barabara ni mbaya mno na leo kulikuwa na tope kabisa, hata kupiga grader hakuna.Akili inasema hii barabara pamoja na parking yake vingewekwa lami ili hata tozo ya shillingi elfu nne iwe na maana.

Kule ndani , vibanda vingi sana wala havijakamilika, hasa mndani ya PTA, na lile banda la waonyeshaji wengi.


Hata hivyo kilichonifurahisha mwaka huu ni kuwa na exhibitors wengi wa ndani hasa bidhaa za ngozi-viatu, mikanda mabegi n.k. Hapo nimejipatia pair mbili za viatu pure leather!!

TANTRADE wanatakiwa kubadilika na kufikiri kidogo.
Maonyesho ya mwakani waanze sasa kwa kuweka lami ndani ya kiwanja kizima.
Sijui kama Waziri Kigoda analielewa hilo?
 
Hata Mh Pinda amecommt jana kuwa miundombinu ya viwanja vya Sabasaba ni minovu mno.
Heri kuahirisha maonesho kwa miaka miwili ili kushughulikia tatizo.
 
KAMA NDO HIVYO NITAENDAJE HUKO NA VEROSSA YANGU SI ITAHARIBIKA KWA HIZO BARABARA MBOVU NDAN YA UWANJA?

CC😡Ntuzu
 
Watanzania ni wazi akili zetu zimejifunga na ndio maana tumeshindwa kubadilisha jinsi ya kufikiri.
Hebu fikiria hizo enzi tangia mji una watu laki nane na kampuni zikiwa RTC na NMC, leo hii mji una wakaazi zaidi ya million tano na na uchumi wenye makampuni zaidi ya laki moja lakini kakiwanja ni kale kale na hakuna hata mwenye wazo la kusogea mbele kutafuta walau heka hamsini na kujenga maeneo mapya!
Watasema 'pesa za kufanya hayo hamna' wakati yakiteketea mabilioni ya kufanya vitu hivyo hivyo hata mara mia.
 

pinda anasema maonesho yasifanyike mwaka mmoja patengezwe, sijui wanataka kujenga shopping mall?!! btw, kama umevipenda viatu vya nyumbani ni vyema ukaongelea kidogo kuhusu kampuni inayotengeza viatu hivyo, au hata ubandike kipeperushi chao na picha za viatu hata ulivyonunua, ndiyo hasa lengo la maonesho mkuu, tuungane mkono!
 
Mkuu kwa kweli viatu nilivyoninia ni fashionable, Travolta, na ni ngozi pure.
Na hata soli siyo mbaya maana ni ile durable flexible hard plastic.
Hii nimenunua kwa 60,000/= dukani si chini ya 150,000 kwa leather.

Na pair nyingine ni ordinary executive office wear shoes.
Ina simila leather top na soli
Bei ni 40,000/=

Kuna vibanda vingi vya viatu katika hilo tenti la BMW(Benjamin William Mkapa pavillion) ila hivi nimenunua kibanda cha ROBI na wale wa TABATA.
 
Hapafai kwenda kabisa, ikiwa umeshaona Trade Fair za wenzetu wa nje ya Tanzania, hapo hurudi tena, ni kujitesa tu.

Ndiyo maana hata exhibitors wanakuwa siyo wale wa maana sana, ni hivi vikampuni uchwara tu vya nje vinavyokuja kuuza vibiashara uchwara. Weka exhibition waje akina Boeing, waje akina Raytheon, Waje akina Hyundai. Waoneshe maajabu ya dunia.

Nilienda mwaka juzi, baada ya nusu saa nikaondoka mbio. Fujo tupu, barabara mbovu, hakuna mpangilio wa maana, makelele utafikiri upo uwanja wa fisi (hata Uwanja wa Fisi siku hizi wamestaarabika).
 
Miafrika Ndivyo Tulivyo - Nyani Ngabu.

Kwa kweli inasikitisha kuona watu walioajiriwa hawajui kufikiri vitu vipya!

Na kwa bahati mwaka huu kuna mabanda ya Wamarekani, India , Indonesia ,Kenya na hata Japan.
Kwa uozo nilouona pale viwanja vya Sabasaba , yaani miundombinu mibovu sana, sidhanii kama watarudi mwakani!

Yaani ni vumbi, vumbi tupu watu wa TANTRADE utafikiri hawaendi Trade Shows nchi za nje, ukweli ni kwamba wanaenda lakini they cant themselves think outside the box.
They lack innovative ideas.
 
Mi huwa naenda kutafuta mademu niwapakaze gundi basi lakini hakuna cha maana
 

Ha ha ha !!!
Very true.
 

Ndio maana siku zote tunwaambia humu kusoma si kuelimika, hawa jamaa zetu kuelimika watachukuwa muda sana.

Usione mtu kavaa vizuri ukadhani wa maana, upeo wao unakuwa finyu kabisa. Yaani, wanaudhi mpaka unatamani kulia.
 

Nakubaliana nawe, maonyesho ya Kibiashara nchini mwetu yanahitaji marekebisho makubwa kiutendaji na sio kugeuzwa kuwa kama JAMBOREE ya uwanja wa fisi - miaka nenda rudi!! Taifa letu litajifunza mengi kwa kukaribisha Makampuni yenye hadhi ya kutoa changamoto kwa Watanzania, vijikampuni uchwara na biashara zao za Mickey Mouse visiruhusiwe kuingia ndani, badala yake viende Kidongo Chekundu wakafanye CAR bootsale.

Hivi FF baada ya kushuhudia maajabu ya MUSA pale uwanja wa Saba Saba, kwa nini hukuwavurumishia one of the Raytheon Company Tomahawk Block 4 Cruise Missiles au LockheedMartin's Longbow HELLFIRE missiles zikawatia akili watayarishaji wa maonyesho.
 
kwa hawa viongozi wetu vichwa maji.. mwakan mambo ni yale yale..
 
dar ni limji lichafu kuliko yote tanzania, najisikia kinyaa kuja huko dar wala kujiita naishi dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…