masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Nimetembelea leo viwanja vya Saba Saba.
Naleo vilikuwa vinatembelewa na kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais Zanzibar.
Tatizo nililoliona ni lile lile la miaka yote.
Vumbi na uchafu.
Vumbi kutokana na barabara za ndani kuwa na mashimo, na vile vile vumbi kutokana na vifusi.
Cha kushangaza ni kuwa TANTRADE wanakuwa na mwaka mzima wa kujiamdaa, lakini shughuli zinaanza mwezi wa tano au sita.
Mbaya zaidi ni sehemu ya barabara inyopakana na jeshi.
Barabara ni mbaya mno na leo kulikuwa na tope kabisa, hata kupiga grader hakuna.Akili inasema hii barabara pamoja na parking yake vingewekwa lami ili hata tozo ya shillingi elfu nne iwe na maana.
Kule ndani , vibanda vingi sana wala havijakamilika, hasa mndani ya PTA, na lile banda la waonyeshaji wengi.
Hata hivyo kilichonifurahisha mwaka huu ni kuwa na exhibitors wengi wa ndani hasa bidhaa za ngozi-viatu, mikanda mabegi n.k. Hapo nimejipatia pair mbili za viatu pure leather!!
TANTRADE wanatakiwa kubadilika na kufikiri kidogo.
Maonyesho ya mwakani waanze sasa kwa kuweka lami ndani ya kiwanja kizima.
Sijui kama Waziri Kigoda analielewa hilo?