Maonyesho ya Mwami Tereza Ntare II Jumba la Kumbukumbu ya Taifa

Maonyesho ya Mwami Tereza Ntare II Jumba la Kumbukumbu ya Taifa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MAONYESHO YA MWAMI TEREZA NTARE II JUMBA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA
Ukiingia lango kuu la Makumbusho ya Taifa sasa unaelekea kwenye ukumbi wa Maonyesho ya Mwami Tereza Ntare imewekwa picha kubwa inayowaonyesha wanawake mashuhuri katika historia ya Tanzania.

Nimesimama hapa kwa muda naziangalia picha hizi moja baada ya nyingine, jicho linakwenda picha nyingine na nyingine na nyingine hadi nimefika mwisho.

Nimeondoka pale kwenye hizi picha kuingia ukumbini.
Moyo wangu mzito sana.

Nina masikitiko makubwa.

Najiambia.
Najiuliza.

Hivi kweli, ndiyo kweli hasa mama zetu waliopigania uhuru wa Tanganyika historia yao imefutwa kabisa?

Haitambuliwi.

Wazalendo hawa mashujaa mama na shangazi zetu hawana tena thamani?

Najiuliza kwa nini haijawekwa picha ya Khadija Mkomanile aliyepigana katika Vita Vya Maji Maji na akanyongwa na Wajerumani?

Lakini kabla hajanyongwa akaja Mmeshionari Fr. Yohannes Hafliger kutoka Peramiho kufuta imani yake akambatiza na kumpa jina jipya la Yasintha kwa ahadi kuwa akikubali kuukana Uislam hatanyongwa.

Inakuwaje hakuna picha ya Chiku bint Said Kisusa, Tatu bint Mzee, Hawa bint Maftah, Halima Khamis, Khadija Kamba, Sharifa bint Mzee, Fatma Matola, Halima Selengia, Amina Kinabo, Mama bint Mwalimu, Nyange bint Chande, Zarula bint Abdulrahman na wengine wengi ambao bado hawajafahamika?

Hakika inasikitisha.
Nani aliyewafuta wazalendo hawa katika historia ya kupigania uhuru?

Picha ya kwanza Mwami Tereza Ntare.
Picha ya pili picha ya wanawake mashuhuri.


1713030969209.png


1713031035809.png
 
Labda kwa makusudi au kwa kudhamiria historia ya Tanzania haijawahi kuandikwa popote kwa usahii. Mashuleni tunafundishwa kuhusu wakoloni na kuacha kujua vyema historia yetu. Kama taifa inabidi tuwe na mjadala mpana kuhusu historia yetu. Historia yenye vipande vipande si historia.
 
Back
Top Bottom