Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Maonyesho haya maalum kwa ajili ya wakulima na wafugaji ambayo hufanyika kila mwaka yanaendelea kupoteza mvuto wake tofauti na ile miaka ya uanzishwaji wake Yan 95,96 na kuendelea. Lakini kuanzia miaka hii ya 2000 katikati hali ni tofauti na miaka ya nyuma.
Wamachinga kwenye maonyesho wanaomwaga bidhaa zao chini ni wengi kuliko hata hao wakulima na wafugaji ambao ni sikukuu yao.
Wachezezeshaji kamari ni wengi na wenyewe, hawa hawana mtaji wa pesa wa bidhaa, wala mazao yoyote yale bali mitaji yao na bidhaa zao ni akili tu. Hili pia nimelishuhudia kwa wingi mwaka huu., nimeshuhudia idadi Kubwa ya wacheza kamari mwaka huu kuliko kipindi kingine.
Wafanyabiashara wa nguo za mitumba. Vyombo vya ndani hutumia nafasi hiyo kufanya biashara zao zaidi ya mkulima mwenyewe.
Hakuna mabadiliko yoyote ya teknolojia ya kilimo, mambo yote ni yale yale tu kama vile bustani ya mboga za majani, nyanya, kuku. Sungura nk. Wananchi na wenyewe wamechoka kuona mtindo ni ule ule waoujua miaka yote.
Nimeshudia aina moja ya ng'ombe akiwa na mtoto wake, tofauti na wakati mwingine kunakuwa na aina tofauti za ng'ombe wa kienyeji na wa kisasa.
Mabanda mengi yalikuwa matupu kwa kile kinachodawaida ni ukubwa wa kodi ya pango hivyo watu kushindwa kumudu gharama za uendeshaji kulinganisha na siku zenyewe ni chache.
Wakulima na wafugaji mabanda yao ni madogo kulinganisha na wafanyabiashara wakubwa kama vile makampuni ya simu, makampuni ya gesi na vinywaji.,hapo tunaona kabisa mfanyabiasha amekuwa mkubwa kwenye maonyesho ya wakulima na wafugaji kuliko wakulima na wafugaji wenyewe ambao ni sikukuu yao.
Serikali ijitafakari upya kuhusu sikukuu hizi za wakulima. Zinaenda kupoteza mwamko wake.
Huu uonyeshaji wa bustani za mboga mboga kila mwaka hakuna mabadiliko yoyote wala mboga mpya zilizoingia mbona karibu kila mtu anajua kulima mboga, hili somo lipo tangu shule ya msingi.
Viongozi wengi wanapenda kubeba waandishi ile siku ya kelele tena kwenye mabanda ambayo yatakuwa yameandaliwa vyema ajili ya upigaji picha na kuonekana kwenye tv