#COVID19 Maonyesho ya Sabasaba kipindi hiki cha Corona yana umuhimu gani?

Kama yatafanyika itabidi wawe strict kwenye matumizi ya barakoa na vitakasa mikono.....tatizo wabongo tunapenda tuanze kushuhudia ndo tuamini. Kwa magonjwa ya kuambukiza kwa kasi kama korona hakunaga huo muda wa kuanza kushuhudia, ukiona umeshuhudia basi hiyo hali iashakuwa si hali tena...
 
Wabongo bhana eti mnaaminishana hakuna corona na ni propaganda za kimagharibi sawa sawa...

Waache tu, watakuja kusimulia hapa.. ..watu kama hawa wanahitaji elimu ya ziada.. ..eti anakuuliza "Corona we mbona hujafa, kwenu wamekufa wangapi? Kuna sehemu wamekufa mji mzima hapa Tanzania?" Mtu kama huyu utamwambia nini akuelewe mkuu 😀


Mimi nina watu wa karibu yangu washapoteza maisha kutokana na janga hili.
 
Kuna haja ya kuepusha misongamano ili kukinga wananchi na korona.
 
Aisee kama Corona huyo yupo nafikiri Bongo ingekuwa 70% ya wananchi wake tumefariki kwa wimbi la 1&2 lile! Na hivi hatuna tahadhari zozote aaah ingekuwa tumeisha lakini bora sisi kuliko wavaa barakoa na wanalockdown
 
Kuna haja ya kuepusha misongamano ili kukinga wananchi na korona.
Njoo kariakoo mzee nyomi kama kawaida alafu uje utuambie sasahivi eti msiwe mnakaa pamoja sijui aaah mbona Magufuli alitufanya tuwe na akili za kufikiri wenyewe na sio kukaririshwa..!!
 

Bado bongo zilizooshwa tokea awamu ile zingalipo.

Mama itabidi atoe karipio kali kurejesha busara kutamalaki.

Hata yale ya mwenge nayo ni hayo hayo.
 
Aisee kama Corona huyo yupo nafikiri Bongo ingekuwa 70% ya wananchi wake tumefariki kwa wimbi la 1&2 lile! Na hivi hatuna tahadhari zozote aaah ingekuwa tumeisha lakini bora sisi kuliko wavaa barakoa na wanalockdown
Huwezi jua watu wangapi wamepoteza/wanapoteza maisha kwa covid bila ya kutolewa statistics.
..watu wangu wa kalibu wamechomoka, nani katoa statistics!!! Wewe huko ulipo umepata taarifa hizi!! Hujui sio, ndio maana huamini corona ipo.. ..

Lockdown pia inachangia maambukizi kuongezeka.. ..hapa kinachotakiwa wapige marufuku mikusanyiko, kumbi za starehe,ma harusi, bar, miziki, mipira n.k ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…