Katika maonyesho haya ya wakulima kipindi hiki imekuwa na utofauti mkubwa sana Zaidi ya mwaka Jana.
Tofauti ni Kuwa wamachinga wa nguo ,wamachinga wa vyombo na mama ntilie,wauzaji wa dawa za asili wamekuwa wengi kuliko wakulima na wafugaji.
Mabanda ya ng'ombe, mbuzi, na kuku hayazidi matano, lakini Kwa upande wa machinga wameteka eneo lote la uwanjan na hivyo kufanya maonyesho hayo kuwa ya wafanyabiashara na si ya wakulima na wafugaji.
Wananchi wengi wamekuwa wakionekana Kwa wamachinga wa vyombo vya ndani, nguo za mitumba, na dawa za asili lakini Kwa upande wa kwenye mifugo na wakulima hamna kitu.