Mapacha kwetu ni kawaida sana.hii imekaaje wadau

Mapacha kwetu ni kawaida sana.hii imekaaje wadau

J putin

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2018
Posts
1,263
Reaction score
1,206
Ukoo wetu wote ni mapacha.
Kwenye familia yetu tuko nane.
Wakike ni wa NNE
Wa kiume pia tuko wa NNE
Dada zangu wote wana mapacha tena kila wakipata mimba ni watoto wawili mpaka tatu.
Kaka zangu pia hali ni hivyohivyo watoto wawili ,watatu.
Na tunafanana sana,sana,sana kutofautisha watoto wa dada na wa kaka zangu ni vigumu sana .

Cha ajabu dada zangu wote ni mapacha wa kike.

Kaka zangu nao wana mapacha wa kiume wote. Ila wote tunatumia jina moja LA ukoo hata dada zangu pia ni hivyo hivyo japo wameolewa lkn haina shida kwa waume wao na wamekubali kutumia jina uko wetu.

Hata mimi najua njia ni moja tu kuja kupata mapacha.

Watalaam hii inakuwaje?
 
Ukoo wetu wote ni mapacha.
Kwenye familia yetu tuko nane.
Wakike ni wa NNE
Wa kiume pia tuko wa NNE
Dada zangu wote wana mapacha tena kila wakipata mimba ni watoto wawili mpaka tatu.
Kaka zangu pia hali ni hivyohivyo watoto wawili ,watatu.
Na tunafanana sana,sana,sana kutofautisha watoto wa dada na wa kaka zangu ni vigumu sana .

Cha ajabu dada zangu wote ni mapacha wa kike.

Kaka zangu nao wana mapacha wa kiume wote. Ila wote tunatumia jina moja LA ukoo hata dada zangu pia ni hivyo hivyo japo wameolewa lkn haina shida kwa waume wao na wamekubali kutumia jina uko wetu.

Hata mimi najua njia ni moja tu kuja kupata mapacha.

Watalaam hii inakuwaje?
Japo mi pia nina nina fani ya afya ila nimesoma sana ila hii ya nyumbani ni shida
 
Nimesoma tu kichwa cha habari na ninakujibu kama ifuatavyo.

Takwimu zinasema katika kila mimba 84 kwa mwanamke 1 ni mapacha. Usijali, yaani nyinyi katika mimba 84 zote ni mapacha basi inamaanisha, umekava 84 ya kwanza, ya pili, ya tatu na kuendelea.
 
Acha kunitukana chief,unaweza kumuoa mamako
Nimekujibu kisomi , wanawake ndio wana determine mapacha kutokana na kugawanyika kwa mayai au kutoa mayai tofauti kurutubishwa wakati mmoja genes hiyo inaelekea sisters wako na mama yako wanayo hapo sishangai sababu hao.ni wanawake lakini unaposema na brother zako nao wanamapacha napata shida sana ina maana brother zako watakua na wanawake ndani ya ukoo wenu ndio maana hako ka abnormality kanaendelea kwenye ukoo ,
 
Pia ndugu kusema kwamba watoto wa dada zako wanatumia jina la ukoo wenu , hii inaonesha mnatabia ya kuoana ndugu wa ukoo , mwanaume gani anayeruhusu mwanae aitwe jina la ukoo wa mwanamke , hii huweza kitokea endapo mwanamke na mwanaume wanatoka ukoo mmoja , kama ni kweli mnatabia ya kuoana wenyewe kwenye ukoo mnajipa nafasi ya magonjwa makubwa ya genetics endapo kuna ka genes kabaya kwenye ukoo kuoana wenyewe genes hii hukua kutokana na wote kuwa carries kunafanya mzae watoto wenye mapungufu au tabia fulani ambayo kama muhusika angeoa njee tabia hii au ulemavu huo wa genes ungepotea kabisa
 
Sawa mapacha wametawala
Tutajie jina la ukoo wenu,maana kwa hilo tu mtakuwa maarufu hivyo ni rahisi kuwajua na kubaini IQ zenu ili wadogo zetu walete posa ktk ukoo huo waendeleze mapacha

Hilo la watoto wa dada zako wote 4 kutumia jina la ukoo wenu(upande wa wanawake) kuna tatizo kubwa.
Inawezekana dada hao wamepata wanaume wenye shida katika kufikiria kwao au kutokana na makuzi/maadili ya familia yenu,kuna hali ya utemi ambayo mnataka kuiabukiza hata huko walikooewa.
HAMUWATENDEI HAKI WANAUME HAO.

Kuhusu kaka zako kuzaa mapacha wote hilo silizungumzii sana maaa post #9 ya geniusMe imejieleza vizuri.

Otherwise unataka kuwanasa akina mama wanaolilia mapacha kila siku,hivyo unawafanyia tricks ili waje wenyewe.

HONGERENI UKOO WA MAPACHA
 
Wanaume hawawezi sababisha mapacha .. Ni genetic za mwanamke na mpaka Leo haijulikani kitu kinachosababisha mapacha ingawa process inajulikana
 
Back
Top Bottom