sangu mnene
Member
- Sep 5, 2012
- 92
- 35
Akiongea kwenye kipindi cha Hoja ya Mwalimu Lwaitama kilichorushwa na SIBUKA TV leo Ijumaa 06-09-2013,Dr Lwaitema amesema kuwa wabunge wa vyama vya upinzani wanajaribu kuizuia CCM kuhodhi Bunge la katiba."CCM inao wabunge zaidi ya robo tatu kwenye Bunge la muungano,lakini tatizo lipo kwenye Bunge la wawakilishi,CCM hawafikii robo tatu ya wajumbe, kwahiyo, CCM wanataka watumie nafasi aliyopewa Raisi kuteua wajumbe 166,kuziba pengo hilo,wamepitisha apelekewe majina tisa kwa kila asasi halafu yeye atateua mmoja anayemtaka ambaye lazima akubaliane na ajenda za CCM" amesisitiza Dr Lwaitama.
Ameongeza kuwa,yapo mapendekezo mengi ya kamati ya Warioba ambayo wananchi wameyafurahia sana lakini CCM hawayaafiki kabisa.Baadhi ya mambo ambayo Dr Lwaitama amesema CCM hawataki kabisa yawemo kwenye katiba mpya ni;
Wapinzani wanajua kuwa kama Bunge la katiba litatawaliwa na wana CCM, mambo yote yaliyotajwa hapo juu na mengine wasiyoyapenda wana CCM yataondolewa kwenye rasimu ya katiba,na hivyo ndoto ya watanzania kupata katiba mpya itakuwa imeyeyuka kabisa. Katiba haitakuwa mpya tena,itakuwa ileile ya zamani kwenye jalada jipya,itakuwa sawa na kuweka divai ya zamani kwenye chupa mpya. Ndio maana wapinzani walitaka idadi ya wajumbe wasio wabunge iwe 400 na wachaguliwe na asasi husika sio Raisi.Wapinzani wamekubali kudhalilika ili kuwafumbua macho watanzania kuwa yale yote yaliyofanywa na kamati ya Warioba na kupendwa na wananchi yapo hatarini kutoweka.
Ndugu wana JF, hivi kweli kwa mswada uliopitishwa leo unaweza kuua ndoto zetu za kupata katiba mpya? Je, pendekezo lililopitishwa kuwa vipengele vya katiba vinaweza kupitishwa na wingi wa wajumbe bila kujali wanatoka wapi inaweza kuwa ni mbinu ya CCM kuhakikisha mambo hayo saba hayaingii kwenye katiba mpya? NAWASILISHA

- CCM hawataki serikali tatu,wanataka serikali mbili.
- CCM inataka mawaziri waendelee kuwa wabunge.
- CCM haitaki wabunge wanawake wachaguliwe,wanataka viti maalum viendelee ili wawaweke ndugu zao.
- CCM haitaki haki za binadamu ziingizwe kwenye katiba mpya.
- CCM inataka majaji waendelee kuteuliwa na Raisi.
- CCM hawataki madaraka ya Raisi yapunguzwe.
- CCM haitaki maadili ya viongozi yawemo kwenye katiba mpya. n.k.