kilio
Member
- Jan 24, 2014
- 29
- 36
Tusipo jiandaa mapema, Watanzania wanaweza wakatumbukia kwenye dimbwi kubwa la migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha kuongezeka kwa kasi kwa matukio yenye uhusiano na magonjwa ya akili. Hii ni kutokana na madhara yatakayosababishwa na program za Akili Bandia zenye uwezo wa kutengeneza taarifa chonganisha. Kunaongezeko kubwa la programu za akili bandia zinazotengenezwa kwa shughuli mbalimbali . Kuna wataalamu wengine wanatengeneza programu hizo na kusambaza taarifa chonganisha zinaweza kusababisha vurugu katika ngazi zote za kijamii. Kwahiyo tunatakiwa tuanze kufanya maandlizi wezeshi katika wizara husika mpaka katika ngazi ya kijamii, kuhusu program hizo za akili bandia kupambana na taarifa chonganishi.
Kwasasa, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum(WMJJWM ), katika upande wa taarifa chonganishi inasumbuliwa haswa na tatizo la ramli chonganishi na taarifa zinazohusiana na imani za kishirikina ili kuweza kujipatia utajiri. Hivyo vyote vinafanywa na baadhi ya waganga wa jadi kwa kushirikiana na wateja wao. Taarifa hizo chonganishi zimesababisha matukio yenye vitendo vya ukatili katika jamii, kama vile Mauaji,ubakaji, kumsabaishia mtu ulemavu , Watu kuchukiana, na tukio kubwa ni kuongeza kwa hali inayohusiana na magonjwa ya akili. Pia taarifa chonganishi zimekuwa tatizo kubwa kwenye mahusihano ya kimapenzi.
Wizara ya Maendeleo ya jamii imesema kunaongezeko kubwa la vitendo vya ukatili vinavyosabishwa na taarifa chonganishi zinazopatika katika simu za mkononi za wapendanao (watu wenye mahusiaho ya kimapenzi). Wapendanao wamekuwa na tabia ya kuzikagua simu zao, wakiamin kujenga uaminifu baina yao. Changamoto inakuja pale wanapokutana na taarifa tata ndani ya simu zao. Zinazopelekea kutokea vitendo vya ukatili kama mauji, kusababishiana ulemavu au kuvunjika kwa ndoa. Wanandoa au wapenzi walioishi pamoja wanapoachana wanaoathirika ni watoto, kukosa malezi ya pande mbili. Tusisahau kunaongezeko la “Single Mothers”
Programu za akili bandia “Generative AI” zikitumika kutengeneza taarifa chonganisha zinakuja kuongeza matukio ya chuki, uhasama wa kimampenzi, ongezeko la vitendo vya ukatili katika jamii. Programu hizi zinapatikana katika simu janja , tukumbuke idadi ya watanzania wanotumia simu janja inaongezeka kwa kasi sana siku hadi siku. Kwahiyo usambaaji wa taarifa chonganishi utakuwa rahisi.
Programu za akili bandia zinauwezo mkubwa wa kutengeneza picha, kutengeneza sauti na kutengeneza video. Kwahiyo kunauwezekano mkubwa watu wakatumia vibaya kutengeza video chonganishi, picha chonganishi na kutengeneza sauti chonganishi ili mradi kuleta taharuki baina ya watu. Kwa kipindi kifupi tangu programu ya akili bandia ya CHATGPT kutengenezwa , kuna malalamiko katika taasisi za elimu, kwamba wanafunzi wanatumia program hiyo kupata urahisi kufanya majukumu yaho. CHATGPT ina mchango mkubwa katika kujifunza vitu, pia inatumiwa vibaya na wanafunzi kufanya udanganyifu katika majukumu yao ya kila siku. Hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa haina hizi za program za akili bandia “Generative AI” zikatatumiwa vibaya kutengeza picha,video na sauti kuchafua taswira ya mtu fulani.

SULUHISHO: Kupambana na changamoto zinazoletwa na programu za akili bandia katika usambazaji wa taarifa chonganishi.
Wizara ya maendeleo ya jamii
Lazima katika wizara ya maendeleo ya jamii na taasisi zake ndogo ndogo, mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi katika maswala ya kijamii kuwekeza katika elimu wezeshi na ngazi mbali mbal za kijamii. Malengo ni kutoa mafunzo ya kutosha kwa watendaji katika wizara husika kuhusu haina ya program za akili bandia zinazochochea vitendo vihovu . Pia kutumia nja rahisi za kuwafikia jamii kutoa elimu, Kwa mfano Mtandao ya kijamii na mikutano; Uwezekano wa kutumia video, sauti na picha zilizotengenezwa na kutumwa katika mitandao ya kijamii kuleta uchonganishi. Jamii inatakiwa kuelezewa madhara ya program hizo kiafya. Kwa mfano, Muhusika aliyetendewa kunauwezekano akapata changamoto zitazopelekea kupata magonjwa ya akili. Muhusika anaweza kuwa na msongo wa mawazo, na kupelekea kufanya maamuzi magumu au ya ukatili. Kwahiyo jamii inatakiwa kuwa waangalifu katika kujihusisha na vitendo vihovu vya kutengeneza taarifa chonganishi.
Wizara ya mambo ya ndani kupitia Jeshi la polisi
Pia jeshi la polisi lazima lipewe elimu hii kuweza kupambana watumiaji wa taarifa chonganishi. Jeshi la polisi linatumika kupambana na vitendo vya wizi wa mtandao, ni fursa nzuri kuunganishwa katika progrmu hii kuweza kutatua migogoro inapotokea katika jamii. Jeshi la polisi liko katika wizara ya mambo ya ndani , liko karibu na jamii ya watanzania wanasikiliza mashtaka mbalimbali kabla ya kwenda mahakamani.
Wizara ya katiba na sheria kupitia taasisi zake na washirika wake na watunga sera “Policy Makers”
Taasisi za sheria za zilizo chini ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania na washirika wake lazima zipate elimu wezeshi kupambana makosa haya ya kimtandao. Teknolojia inakua kwa kasi, na kuna programu nyingi zinatengenezwa za Akili Bandia, ambazo zinahusiano mkubwa na makosa ya kimtandao, kama usambazaji wa taarifa chonganishi kupotosha jamii. Wizara hii ndiyo kuna muhimili wa Serikali unaoitwa mahakama ndiyo wenye maamuzi katika mahakama zetu.
Ya mwisho ni kuwafikia watunga sera katika serikali ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania, wanatakiwa kuwezeshwa kielimu kuhusu madhara ya program hizi za akili bandia. Itawezesha kuja na sera mbadala kupambana na hizi changamoto zitazopelekea migogoro mikubwa katika jamii yetu ya watanzania.

Hitimisho, Tanzania salama inawezekana, kupitia elimu wezeshi zidi ya taarifa chonganishi zinazotengenezwa kupitia programu za Akili Bandia.
Upvote
1