rushwa hasa zile ndogondogo...
Ulikuwa sahihi kabisa uliposema rushwa imekuwa utamaduni. Na lugha ni sehemu ya msingi kabisa ya utamaduni. Huu utamaduni wa kusema kuna rushwa ndogondogo ndio unajenga nafsi za kifisadi. Rushwa ni rushwa tu na fisadi ni fisadi tu hata umuite fisadi papa, nyangumi, kamongo, kibua, perege, changu au dagaa!
Siku Watanzania watakapokuwa tayari kusema kwa maneno na matendo kuwa "rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa rushwa" ndipo tutashinda kwenye haya mapambano dhidi ya ufisadi. Pambano linaanzia nafsini. Lazini tuzikane nafsi zetu za kifisadi!
Umesikika ndugu ila.. why dont u walk the talk by sharing your own experience on how you have been corrupt? This will break the ice....
Umenihukumu kuwa nimejitenga kwa kutumia lugha ya " wengine" je hiyo lugha ya nyekundu hapo juu unasemaje?....wewe siyo Mtanzania?
Anyway.. back to the issue.
Ni maneno, malalamiko, manung'uniko, shutuma tu kila kukicha kulikoni? Tanzania haijawahi kupungukiwa na taasisi za kupambana na Rushwa. Wakati wa uhuru, Tanzania ilirithi Sheria ya wakoloni ya kupambana na Rushwa ya 1958, hadi 1971 wakati sheria ya Anti-corruption ilipopitishwa. Pia Permanent Commission of Enquiry ilianzishwa 1966 kuchunguza mienendo ya Rushwa iliyokuwa inafanywa na Viongozi wa juu wa Serikali na Siasa na kulalamikiwa na wananchi.Kutokana na kukuwa kwa tatizo la rushwa, mwaka 1975 serikali ikaanzisha kikosi cha kupambana na rushwa (Anti-Corruption Squad). Katikati ya miaka ya 1980, kikosi hiki kilionekana dhahiri kuwa hakifanyi kazi yake kikamilifu na hata watu kukibatiza Corruption Squad.
1983 jitihada nyingine zilifanyika Mahakama ya wahujumu Uchumi ilianzishwa (National Anti-Economic Sabotage Tribunal) ili kushughulikia washtakiwa waliokuwa wanatuhumiwa kuhujumu uchumi. Mwaka wa kwanza tu, kati ya watuhumiwa 4,216 waliofikishwa kwenye tribunal hiyo iliyoongozwa na Jaji Mrosso, washtakiwa 424 walionekana na hatia, 2,155 wakaachiwa baada ya kuonekana hawana hatia. Hata hivyo ilikuja kudhihirika kuwa wengi wa waliokamatwa kwa uhujumu walikuwa ni watu wa kawaida mno na hakukuwemo na watu wazito au mapapa na manyangumi wa Ufisadi kama wanavyojulikana leo.
Miaka ya 1990 ilishuhudia hatua zaidi zikichukuliwa ambapo mwaka 1991 yakafanyika mabadiliko ya Kikatiba, na kubadilisha Anti-Corruption Squad kuwa the Prevention of Corruption Bureau (PCB). Mwaka 1995, ikaundwa Sheria ya maadili ya viongozi- the Public Leadership Code of Ethics kuwamulika viongozi wenye kutumia vibaya madaraka. Pia Sheria hii ikaunda Sekretariat iliyoongozwa na Commisioner wa Maadili.
Pamoja na kuundwa kwa utitiri huu wa taasisi na Sheria, hadi kufikia katikati ya miaka ya 1990, hali ya Rushwa ilionekana kutisha ikiwa imeingia kila nyanja ya maisha ya Mtanzania. Ndipo Rais wa awamu ya Tatu Bwana William Mkapa alipotangaza kupambana na rushwa kuwa ni kipaumbele katika utawala wake. Alianza kwa kuunda Tume iliyojulikana kama Tume ya Warioba (the Presidential Commission of Inquiry Against Corruption) mwaka 1996. Mwenyekiti akiwa ni Jaji Joseph Warioba. Tume hii ilifanya kazi yake kwa kuchambua na kutafiti tatizo la rushwa nchini na kuandika taarifa iliyojulikana kama Warioba Report.Humo walionyesha visababishi vya rushwa kwa kirefu sana, na kupendekeza nini kifanyike. Aidha ilibainisha kuwa rushwa imeenea kila mahali na imesababishwa na uzembe na kukosekana kwa uwajibikaji katika taasisi za umma, ukosefu wa huduma muhimu, mishahara midogo kwa watumishi wa umma ukilinganisha na hali ya maisha inavyozidi kupanda siku hadi siku, mmomonyoko wa maadili/uadilifu kwa
Ripoti ya Warioba ilipendekeza mambo kadhaa ambayo utekelezaji wake ulizaa urekebishwaji wa taasisi na mifumo mbalimbali ndani ya Serikali.Baadhi ya mapendekezo ni pamoja na kusafisha safu ya juu ya uongozi na kuweka watu waadilifu, Rais kutoa Maagizo kwa viongozi wote kupambana na rushwa maeneo wanayoongoza, elimu kwa umma kufahamisha kuhusu haki zao, kuwaadhibu vikali wale wote walioonekana na makosa ya rushwa, ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zao kisheria.
Serikali ilichukua hatua kadhaa kama utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo hayo kama kuweka mpango mkakati wa kupambana na Rushwa (Nation Anti-Corruption Strategic Action Plan (NACSAP) wa mwaka 1999. Hii ilifuatiwa na kuanzishwa kwa Kitengo cha kuratibu Utawala bora - Good Governance Coordinating Unit mwaka 2000 ili kiwe kinasimamia utekelezwaji wa NACSAP pamoja na mambo mengine.Sanjari na hili pia ikaanzishwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora - the Commission for Human Rights and Good Governance mnamo mwaka 2001. Kulifuatiwa na maboresho mengine kadhaa pamoja na kupitishwa kwa Sheria kadhaa ikiwa ni pamoja na Finance Act na Public Procurement Act (2001) iliyorekebishwa 2004, sheria iliyolenga kuongeza uwazi na uwajibikaji (transparency and accountability). Hii ni kwa uchache tu.Sheria hii imeshafanyiwa marekebisho zaidi.
Nitaendelea kuwaletea mengine zaidi ila hadi wakati huo..tuchangie katika yafuatayo?
Ni wapi tunakosea katika vita dhidi ya rushwa kwa maana Rushwa imekuwepo toka ukoloni ndio maana sheria ilikuwepo; baada ya uhuru tunaona jitihada chungu nzima lakini rushwa bado inaibuka kidedea.
Kwa hivyo ukweli wenyewe ni msamaha wa yaliyopita na kuanza upya kuvipa vyombo vinavyohusika unlimited power na access hili wafanye kazi ya kweli vinginevyo ni mchezo its a fact.
Come on, hivi hao wananchi unaosema wataelimishwa na nani? na hao hao wala rushwa, na sisi M, na vyama vya upinzani, au na malaika special toka sayari ingine?Tuache ulimbukeni wa kukimbilia kuilaumu CCM, hili suala halihusu siasa wala chama fulani. Ni suala la kitaifa linalomuhusu kila Mtanzania.
Rushwa: wananchi hawako tayari kupambana na rushwa.!! Why? kwa sababu sheria zilizopo zinatosha kuwapa shida wala rushwa wachache hazitumiwi na wananchi. Wananchi wanakata tamaa badala ya kulalamika na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria wanaona hakuna la kufanya, wanaona ni afadhali na wao wale rushwa kuliko kuhangaika kupambana na rushwa.
Wananchi wanatakiwa kubadilika (kama ni kwa kuelimishwa au kwa wao wenyewe kuchoka) wawe wakali dhidi ya wala rushwa popote pale walipo. Rushwa isionewe aibu kuanzia majumbani hadi maofisini ndipo Taifa litafanikiwa kupambana na Rushwa. Vita ya rushwa inafaa ipiganwe kama au sambamba na AIDS, kila mmoja ajione ana jukumu la kupambana na rushwa pale alipo kwa vitendo na sio kulaumu kwa maneno matupu.
Nakubaliana na wewe mama, maana kila mmoja hata mafisadi wakisimama jukwaani ulia kilio hicho hicho na sometimes unaweza usijue fisadi ni nani hasa.Rushwa imeshageuka utamaduni..njia ya maisha kwa watanzania.Pamoja na kuwa watu "wanachukia" rushwa, bado wanaiendekeza.....wanashiriki..kutoa na kupokea..kuanzia wasio na kitu hadi wenye vitu.
Haya mambo siyo personal ndugu yangu.Ukiniuliza maswali kama haya yenye kunilenga mimi na maisha yangu binafsi... nitakupa majibu yafuatayo tena very frankly:
1.Cheti cha kuzaliwa - sikukishughulikia mimi bali wazazi wangu
2.Vyeti vya shule - kila nilipohitimu nilipata cheti changu kihalali bila kutoa KK yotote kwa maana nilifaulu kihalali..sikuhitaji kuiba cheti cha mtu au kubadili chochote kwenye cheti
3.Passport niliiipata zamanni mno kupitia wazazi wangu sijahonga mtu hata kwenye ku renew mara zote nafuata utaratibu.Sijaenda kutafuta passport bila kuwa na safari yenye uthibitisho.
4.Kiwanja - nilinunua kwa mtu wa pili na hapo ni transaction ya kibiashara hivyo rushwa ya nini? ( kununua kwa maana ya compensation for unexhausted improvements)
5.Kazi niliyonayo - sijahonga bali nilipambana thru due process
6.ile naniii - ipi?
Kutokana na hayo hapo juu ndugu utaona kuwa siyo lazima kutumia rushwa kupata huduma.Ila inatakiwa ujue wapi, nani, muda gani.INFORMATION IS POWER.
Rushwa imeshageuka utamaduni..njia ya maisha kwa watanzania.Pamoja na kuwa watu "wanachukia" rushwa, bado wanaiendekeza.....wanashiriki..kutoa na kupokea..kuanzia wasio na kitu hadi wenye vitu.
The reality ni kuwa rushwa ni rafiki wa haki....
Field Marshall Es,
Mkuu, kwa mtu mwenye kufahamu unazungumzia upande mmoja tu, ama kweli nyani huwa haoini kundule...Hii ikiwa na maana wewe unawaona watu kama Waislaam tu kuwa wao ndio wenye makosa, inawezekana kabisa ktk fikra zako hata Kikwete unafikiria makosa yake yanatokana na kuwa Muislaam...Ya Ufisadi yameshakuwa ya Waislaam, duh! nina hakika hizi ndizo mbinu za kanisa tunazishtukia tayari mkuu wangu tunajua kinachoendelea...
Now, vita imegeuka sio against mafisadi tena ila waislaam - heeee!...mkuu, hatutafika mkuu wangu, ya Nigeria yatakuja wala sii muda, kwani waislaam sii watu wa kutiwa vidole vya macho wakanyamaza..Diversity ni pamoja na wewe kukubali ya wengine sio sisi tukubali na kuvumilia yako tu.
Kaazi kweli kweli ..ndio Maana nakubali kabisa maneno ya Nyani Ngabu - NDIVYO TULIVYO..
Jirani maneno mazuri sana hayo. Wako Watanzania wengi sana ambao wanafuata sheria bila kutaka kupindisha sheria ili wapate upendeleo wa aina moja au nyingine na wala hawajawahi kufaidika hata indirectly na utoaji au upokeaji wa rushwa.
Nimekutana na Watanzania mbali mbali ndani na nje ya nchi ambao walikuwa hawana hata godfather au godmother wa kuwasaidia wapate upendeleo wa kufika pale walipo leo hii kimaisha. Wengi ni juhudi za binafsi na wala hawakutoka katika familia za kuwawezesha hata kutoa hiyo hongo. Wengi wa hawa ni wa miaka ile ya Mwalimu Nyerere ambapo rushwa ilikuwa ni ndogo sana kulinganisha na sasa ambapo imeshamiri kila kona na Kikwete na Serikali yake wameifumbia macho.
Modern Tanzania
- Unfortunately in 1967 Nyerere adopted a policy of socialism. He made the Arusha declaration in which he outlined his vision of a socialist Tanzania.
- However in Tanzania, as in other countries, socialism proved to a complete failure.
- The cornerstone of that policy was called Ujamaa (family hood). Nyerere planned to create huge collective farms. The people were encouraged to move into large villages in which food and other goods would be produced collectively for the whole community.
- However the policy proved disastrous. Agricultural production slumped and the Tanzanian economy was wrecked.
Furthermore by 1973 only about 20% of the population had moved to Ujamaa villages. So Nyerere forced people to move and by 1977 about 80% of the population had been resettled.
- Meanwhile in 1977 Tanzania became a one-party state.
At that time Uganda was ruled by the tyrant Idi Amin. In October 1978 Amin invaded the Kagera region on Tanzania. In January 1979 a Tanzanian force counterattacked and rapidly overran Uganda. The Tanzanians withdrew in 1981.
- Meanwhile Nyerere was re-elected president in 1980. However the Tanzanian economy was in tatters and corruption was endemic. Furthermore Tanzania sank heavily into debt. International donors demanded reform in return for help but Nyerere was unwilling to change his policies. So in 1985 he resigned.
- He was replaced by Ali Hassan Mwinyi. He spent the next 10 years trying to repair the Tanzanian economy. Mwiyini privatised business and tried to purge corruption. He also encouraged foreign investment. As a result the Tanzanian economy began to grow steadily.
- In 1992 Tanzania became a multi-party democracy and in 1995 Benjamin Mkapa became president.
In 2005 Jakaya Kikwete was elected president.
Today Tanzania is still very poor. However the government is making strenuous efforts to reduce poverty. In 2001 school fees were abolished and as a result attendance at school greatly increased.