Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,467
- 3,687
Baada ya kuwaza na kuwazua yule Mwasi mkuu yaani Shetani akaja na wazo ili kudumisha wazo lake la kutokufa hakika (Mwanzo 3:4),alitunga Uongo mwingine ili kulinda uongo wake wa awali.
Wazo lake likawa hivi: MTU AKIFA ROHO YAKE HAIFI,ITAENDELEA KUISHI MAHALI PENGINE.
Katika uongo huu ameilevya dunia yote,baadhi ya jamii kila mwaka hufukua makaburi ili kuwatoa watu na kuwabadilishia mavazi yao, Wengine huenda makaburini kila siku kufanya usafi kwa kudhani kuwa Marehemu anachukia uchafu, Wengine huenda makaburini na kuomba baraka za wafu, Wengine huita majina ya ndugu zao waliokufa ili kuwafurahisha wafu hao,Wengine hupeleka vyakula makaburini kila siku wakiamini Marehemu watakula/atakula chakula kile! Wengine huweka fedha zao juu ya kaburi Kama zawadi kwa Marehemu nk nk...Mambo yote haya hufanyika kwa kusudio moja tu kuwakumbuka wafu na kutowachukiza wasije wakatulaani.Kuwakumbuka wafu ni Jambo zuri tu, na kusafisha sehemu ya makaburini ni jambo jema kabisa maana uchafu huzalisha magonjwa hatari Kama kipindupindu na hatari nyingine nyingi.
Hivyo kusafisha makaburi ni sawa tu,kuyatunza ni sawa tu Ila likija Jambo la kufanya Hayo kwa sababu et marehemu atafurahi au atatubariki Hilo ni jambo jingine kabisa tena ni chukizo kwa BWANA Maana yeye si Mungu wa wafu bali wa walio hai.
Lakini ukweli ni kuwa mtu akifa hajui Jambo lolote,hata Kama alikuwa akichukia kitu fulani au kupenda kitu fulani ndio hawezi tena kufanya hivyo maana hana ufahamu wowote,haoni chochote,maana ufahamu wake umeondoka, hesabu zake zimefungwa kabisa (Mhubiri 9:5,6, Zaburi 6:5).
Mtu = Mwili wa mavumbi/udongo Kujumlisha(+) Pumzi ya Mungu
Kwahiyo ukiondoa Pumzi ya Mungu kinachobaki ni mwili wa mavumbi/udongo ambao kimsingi hauna ufahamu wowote, ile Pumzi ya Mungu ndiyo yenye kuutia nuru mwili,na kuupa ufahamu mwili na kuupa hisia zote mwili,hivyo Pumzi hiyo ikitoka mwili ule hubaki mtupu usio na hisia yoyote Wala ufahamu Wala nguvu.
Ile roho hutoka,Biblia haitwambii kwamba roho hiyo ikitoka kuna mahali inahifadhiwa,maana pumzi haishikiki na hakuna mahali itahifadhiwa.
Kwa mantiki hii mtu akifa haendi Mbinguni bali mtu huyo huenda kaburini,gizani,kwenye kimya, hakuna kazi yoyote inafanyika kaburini.
Haijalishi ni mtakatifu au mtu muovu sana wote wakifa huzikwa, wanangojea ufufuo wa Yesu Kristo,Mwili huu hauwezi kufanya lolote bila pumzi ya Uhai ya Mungu, hivyo ili uhuike Inabidi upokee tena nguvu ya Uhai kutoka kwa Mungu na huo ndio ufufuo.
Swali jingine,Je,roho za hawa wanyama wanaokufa au tunaowachinja roho zao huenda wapi?
Sote tunajua tukichinja mnyama kama ng'ombe au mbuzi au kuku tunakula nyama yake yote
Je, huwa tunawaza kuhusu pumzi yake huenda wapi? Jibu ni moja kama ilivyo kwa mtu ndivyo ilivyo kwa mnyama au ndege au kiumbe chochote chenye Uhai;pumzi hutoka na hakuna store ya pumzi ya watu au wanyama
. (Soma Mhubiri 3:19-21)
Mtu akifa haendi mbinguni Wala motoni Wala toharani wala hageuki kuwa muzimu.Mtu akifa hurudi mavumbini -shimoni ambako hakuna ufahamu wowote,Wala hakai hewani au angani kama baadhi wanavyoamini
Hakika,aliyekufa hatarudi nyumbani kwake( Ayubu 7 :10) kusumbua watoto wake,arudi usiku kuwatisha au kupambana na wanaonyanyasa watoto wake? Hapana, maana mtu aliyekufa hawezi kufanya jambo lolote hana ufahamu wowote,Wala hageuki kuwa mzimu wa kulinda familia na kutatua migogoro ya jamii yake.
Na Yesu Mwenyewe alisema atakaporudi katika dunia hii Wafu wote waliomo makaburini (Hasemi walioko Mbinguni au motoni au hewani au angani, Anasema wafu waliomo makaburini) wataisikia sauti yake nao watatoka humo makaburini walimokuwa ili wapate ujira wao kadri ya matendo yao yalivyo (Yohana 5:28,29) Yesu alikuwa wazi sana alitaja wazi wafu wamo makaburini,wamefukiwa na saa ya kutoka ikifika watatoka humo.
Hata yule Lazaro wa Bethania Kaka wa Martha na Mariamu alipokufa Yesu alimwita kutoka Kaburini na alitoka akiwa amefungwa sanda bado (Yohana 11:1-45)
Manabii wote na mitume waliokufa wamo makaburini hata Mfalme Daudi ambaye kiti cha Ufalme wake kinatajwa kuwa cha milele yeye Daudi yumo Kaburini hata Leo hii(Matendo 2:29).
Mpendwa, Mkatae Shetani na Mambo yake yote na Mwamini Mungu ili upate Uzima wa milele.