Mapambano ya sirini

Mapambano ya sirini

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
282
Reaction score
275
MAPAMBANO YA SIRINI.

Jambo la msingi sana kutambua kwenye haya maisha ni kwamba haijalishi unamuona mtu yuko vizuri ama amefanikiwa kwa kiasi gani tambua yuko na mapambano yake sirini, na mapambano ya sirini yanabaki ni siri ya mtu huenda usiyatambue kabisa kwa sababu mbele ya macho yako unaona yuko sawa, lakini ni jambo jema sana. Kujifunza kuwa wakarimu kwa kila mtu.

Hujui anapambana na kitu gani na anahitaji kutiwa moyo kwa namna gani ukarimu unaweza kuwa tiba kubwa kwake zaidi ya vile ambavyo unafikiria ama kudhania, natambua hata kwako pia bado unahitaji ukarimu wa mtu aliekaribu yako na kila mtu, hivyo jitahdi kuwa mkarimu ili upoke ukarimu.

Mfano: Ukikutana na mtu ambae anapenda kulalamika hapendwi, hapewi thamani yake,tambua kitu anachokisema ndio kimepngua kwake, akisema hapendwi tambua kiwango cha upendo kwake kimepungua sio kwa kukupenda wewe ila kwa kujipenda yeye, hivyo anahitaji mtu wa kukijaza tena kikombe chake cha upendo ili aendelee salama, jambo la kushangaza na kuogopesha akikosa mtu wa kukijaza kwa muda mrefu anageuka kuwa adui na mkali kuliko maelezo na mwisho ni matendo ya hasira ambayo yanaongozwa na majuto.

Kuwa mkarimu leo kwa ajili ya kesho bora kwako na kizazi chako, ukarimu ni TIBA YA MOYO.

Soma Pia: Acha Kuishi, Anza Kuishi

MAISHA NI HAYA HAYA WA KUBADILIKA NI WEWE.
 
Nilifikiri mimi nina madeni bwana , aisee leo kuna file nimekutana nalo la watu nawajua ambao hata sikuwadhania, aisee mimi sina deni hata 1 😂😂😂😂😂😂, kiukwel nimesikitika, sijafurahia.
 
Nilifikiri mimi nina madeni bwana , aisee leo kuna file nimekutana nalo la watu nawajua ambao hata sikuwadhania, aisee mimi sina deni hata 1 😂😂😂😂😂😂, kiukwel nimesikitika, sijafurahia.
Na ukikutana nao ni kama hawana madeni, sirini wanasumbuka ila machoni ni kama wako sawa…tujitahidi tu kuwa wakarimux
 
Back
Top Bottom