Maparachichi ya Tanzania yanavyouzwa nje ya nchi kwa kupewa uraia mpya

Maparachichi ya Tanzania yanavyouzwa nje ya nchi kwa kupewa uraia mpya

blix22

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
213
Reaction score
645
MAPARACHICHI YA TANZANIA YANAVYOUZWA NJE YA NCHI KWA KUPEWA URAIA MPYA

Tanzania imejizolea umaarufu kwenye nchi za kiarabu kutokana na maparachichi yanayolimwa na kusafirishwa kutoka kwenye Taifa hili kuwa na ubora wa hali ya juu.

Pia Tanzania huzalisha maparachichi mengi kuliko nchi yoyote barani Afrika. Hii inatokana na juhudi nzuri za Serikali chini Hayati Dkt. Magufuli na aliyekuwa Makamu wake, Mhe. Samia Hassan (sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

Licha ya kuongeza uzalishaji wa maparachichi bora, chombo cha habari cha Ujerumani (DW) kinasema kwamba maparachichi yanayolimwa Tanzania hununuliwa kwa bei nafuu na wafanyabiashara wa Kenya kisha kuuzwa kwa bei ya juu huko barani Ulaya yakiwa na chapa inayosema Product of Kenya ama bidhaa iliyozalishwa Kenya, huo ni uzandiki. sio kweli.

Si hivyo tu, bali wafanyabiashara nchini Tanzania wamekuwa wakiyauza bei kubwa maparachichi bora yaliyozalishwa nchini kwa kuwadanganya raia kwamba eti maparachichi hayo yanatoka Burundi.

Hali hiyo, haijaishia kwenye parachichi tu, ukitembea kwenye Soko la Sabasaba jijini Dodoma hususan kwenye majengo mazuri, utajionea mchele mzuri wa Tanzania umeandikwa Mchele wa Zambia.

Jambo jingine, Njombe imekuwa ikizalisha matofaha (apples/peasi) bora katika miaka ya hivi karibuni lakini wafanyabiashara huyachukuwa yale yenye ubora mkubwa na kuyaweka stickers kisha huzichanganya na apples zinazotoka Afrika Kusini na kuyauza matunda hayo kwa Watanzania kwa bei kubwa. Kwa wastani apple kubwa lenye ubora mkubwa linatoka katika mkoa Mkoa wa Njombe huuzwa kwa shilingi 300-500 lakini wafanyabiashara wakishayachanganya na apples za S.A huyauza kwa shilingi 1000.

We need Magifulification in Agricultural Market! Hayati Magufuli alisimamama kidete kuhakikisha madini ya Tanzania yanauzwa kwa jina la Tanzania.

Ombi, Tunaziomba mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Kilimo, Uwekezaji na viwanda na biashara na Taasisi ya utafiti wa Kilimo (TARI) zifikirie namna bora ya kuhakikisha mazao ya kilimo yanakuwa wakala mzuri wa kuitangaza Tanzania nje ya nchi ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja kujionea kilimo bora kilichopo nchini ikiwemo Kilimo cha maparachichi.

Patrick Sanga,
Mkulima, Njombe
 
Ninaunga hoja yako kwa asilimia 100. Wizara ya Kilimo ina wajibu gani?. Bidhaa za Tanzania zinasafirishwa kwenda Kenya na baadaye kusafirishwa nchi za nje zikiwa na nembo ya Kenya. Nadhani hata safari hii ya Mhe. Rais kwenda Kenya, uongozi wa kenya unaenda kumpigia magoti akubali biashara zirudi kama zamani ambapo walikuwa wanatunyonya sana. Hapa ndipo nilipompendea Mhe. hayati Magufuli. Aliweka nchi, watanzania kwanza. Wizara ya Kilimo ni muda muafaka haya yanayoelezwa mkayafanyia kazi. AMKENI WAKATI NDIYO HUU.
 
Kuweka habari ya mwendazake kwenye hii thread yako ni sawa na umemwaga mafuta ya taa kwenye mchuzi alafu watu wako mezani wana njaa balaa.

Magufuli hayupo watu waelewe na hakua na sera nzuri kwenye uchumi wa nchi hii na alikua muongo uchumi unaku 8% leo siku ya arobaini na tano hivi tunaambiwa uchumi wetu umeshuka hadi 4.7 jamaa alikua muongomuongo sana
 
Anajaribu kuleta hoja kama wabunge wa 'kijani' Bungeni asijue wale ni wanasiasa wana maslahi yao binafsi

Siku nyingine ndugu mkulima zingatia hadhira uliyopo unapotoa hoja ya msingi kama hii.. hapo umeonekana umewataja kinafiki tu hao uliowataja usijue wamefanya nini hasa.
Mie sijaacha kusoma Kwa sababu namchukia mtajwa Bali kubumbabumba story anafikiri wote ni vilaza kama Jobu.
 
Back
Top Bottom