Maparachichi ya Tanzania yanavyouzwa nje ya nchi kwa kupewa uraia mpya

Maparachichi ya Tanzania yanavyouzwa nje ya nchi kwa kupewa uraia mpya

MAPARACHICHI YA TANZANIA YANAVYOUZWA NJE YA NCHI KWA KUPEWA URAIA MPYA

Tanzania imejizolea umaarufu kwenye nchi za kiarabu kutokana na maparachichi yanayolimwa na kusafirishwa kutoka kwenye Taifa hili kuwa na ubora wa hali ya juu.

Pia Tanzania huzalisha maparachichi mengi kuliko nchi yoyote barani Afrika. Hii inatokana na juhudi nzuri za Serikali chini Hayati Dkt. Magufuli na aliyekuwa Makamu wake, Mhe. Samia Hassan (sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.)

Licha ya kuongeza uzalishaji wa maparachichi bora, chombo cha habari cha Ujerumani (DW) kinasema kwamba maparachichi yanayolimwa Tanzania hununuliwa kwa bei nafuu na wafanyabiashara wa Kenya kisha kuuzwa kwa bei ya juu huko barani Ulaya yakiwa na chapa inayosema Product of Kenya ama bidhaa iliyozalishwa Kenya, huo ni uzandiki. sio kweli.

Si hivyo tu, bali wafanyabiashara nchini Tanzania wamekuwa wakiyauza bei kubwa maparachichi bora yaliyozalishwa nchini kwa kuwadanganya raia kwamba eti maparachichi hayo yanatoka Burundi.

Hali hiyo, haijaishia kwenye parachichi tu, ukitembea kwenye Soko la Sabasaba jijini Dodoma hususan kwenye majengo mazuri, utajionea mchele mzuri wa Tanzania umeandikwa Mchele wa Zambia.

Jambo jingine, Njombe imekuwa ikizalisha matofaha (apples/peasi) bora katika miaka ya hivi karibuni lakini wafanyabiashara huyachukuwa yale yenye ubora mkubwa na kuyaweka stickers kisha huzichanganya na apples zinazotoka Afrika Kusini na kuyauza matunda hayo kwa Watanzania kwa bei kubwa. Kwa wastani apple kubwa lenye ubora mkubwa linatoka katika mkoa Mkoa wa Njombe huuzwa kwa shilingi 300-500 lakini wafanyabiashara wakishayachanganya na apples za S.A huyauza kwa shilingi 1000.

We need Magifulification in Agricultural Market! Hayati Magufuli alisimamama kidete kuhakikisha madini ya Tanzania yanauzwa kwa jina la Tanzania.

Ombi, Tunaziomba mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Kilimo, Uwekezaji na viwanda na biashara na Taasisi ya utafiti wa Kilimo (TARI) zifikirie namna bora ya kuhakikisha mazao ya kilimo yanakuwa wakala mzuri wa kuitangaza Tanzania nje ya nchi ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja kujionea kilimo bora kilichopo nchini ikiwemo Kilimo cha maparachichi.

Patrick Sanga,
Mkulima, Njombe
Umezungumza kweli tupu,Nilikuwa naangalia kwenyevgazeti moja la nje ,inaonyesha Kenya ni yavsita duniani kwa kuzalisha maparachichi huku Tanzania ikiwa haimo hata kumi bora.Wakati huo Kenya wanamakampuni yananunua nchini na kuyapeleka kenya.Wakifika huko wanayasafirisha nje kwa label yao!
 
Serikali ya Kenya walichofanya walipigania na kuwatafutia masoko ya nje wakulima wa maparachichi watu wao na walifanikiwa!
Sasa kwanini wakenya wasije nunua maparachichi tanzania?

Ova
 
Ninaunga hoja yako kwa asilimia 100. Wizara ya Kilimo ina wajibu gani?. Bidhaa za Tanzania zinasafirishwa kwenda Kenya na baadaye kusafirishwa nchi za nje zikiwa na nembo ya Kenya. Nadhani hata safari hii ya Mhe. Rais kwenda Kenya, uongozi wa kenya unaenda kumpigia magoti akubali biashara zirudi kama zamani ambapo walikuwa wanatunyonya sana. Hapa ndipo nilipompendea Mhe. hayati Magufuli. Aliweka nchi, watanzania kwanza. Wizara ya Kilimo ni muda muafaka haya yanayoelezwa mkayafanyia kazi. AMKENI WAKATI NDIYO HUU.
Hakuna kunyonywa wala nini
Bora umuzie mkenya nanasi au papai
Hela na Friday utaiona, kuliko uwauzie wazee wa chamazi na wengineo
Alafu msipende kuwalaumu wakenya wenzetu serikali yao wako vizuri kuwatafutia watu wao masoko ya nje
Hivi serikali yetu inafanya hivyo au ndiyo wanaridhika kuona mtu mmoja mmoja ndy awe ana export bidhaa

Ova
 
Umezungumza kweli tupu,Nilikuwa naangalia kwenyevgazeti moja la nje ,inaonyesha Kenya ni yavsita duniani kwa kuzalisha maparachichi huku Tanzania ikiwa haimo hata kumi bora.Wakati huo Kenya wanamakampuni yananunua nchini na kuyapeleka kenya.Wakifika huko wanayasafirisha nje kwa label yao!
Serikali yetu kupitia wizara husika wanachukua hatua gani ili wakulima maparachichi hapa wa export nje?

Ova
 
**** kweli wewe kwani kabla ya magu parachichi zilikua haziuzwi huko uarabuni......
 
Pia Tanzania huzalisha maparachichi mengi kuliko nchi yoyote barani Afrika. Hii inatokana na juhudi nzuri za Serikali chini Hayati Dkt. Magufuli na aliyekuwa Makamu wake, Mhe. Samia Hassan (sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

Hahah, kuna wakati ukidanganywa unaishia kucheka tu sababu ukweli waujua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea jambo la maana sana.Ila kunamsamiati umeutumia umepunguza uzito wa kile ulichotaka tukipate kutoka kwenye wazao lako/ habari yako.
 
Dasa nyie wakulima mtakuwa wajinga kama unataka serikali iunde chombo cha regulatory kama Korosho nk mtaanza kulia Lia

Bora ilivyo hivi hivi soko huria ,nyie hamjakatazwa kupeleka huko nje hao wanaweza kwa vile Wana mitaji na connection za soko

Imagine wasingekuwepo hao wakenya ungekula parachichi zote ?
 
Ninaunga hoja yako kwa asilimia 100. Wizara ya Kilimo ina wajibu gani?. Bidhaa za Tanzania zinasafirishwa kwenda Kenya na baadaye kusafirishwa nchi za nje zikiwa na nembo ya Kenya. Nadhani hata safari hii ya Mhe. Rais kwenda Kenya, uongozi wa kenya unaenda kumpigia magoti akubali biashara zirudi kama zamani ambapo walikuwa wanatunyonya sana. Hapa ndipo nilipompendea Mhe. hayati Magufuli. Aliweka nchi, watanzania kwanza. Wizara ya Kilimo ni muda muafaka haya yanayoelezwa mkayafanyia kazi. AMKENI WAKATI NDIYO HUU.
Unataka wizara ifanyaje,pumbavu majitu yanayotegemea salary ni hovyo Sana.

Ma viongozi yenu akiwepo marehemu kituko walishindwa kuwezesha wafanyabiashara wa ndani waweze kushindana na hao wakenya afu unaongea ujinga

Kwamba unataka serikali inunue maparachichi kama Korosho au?

Acheni upumbavu maana bila hao wakenya ungeuzia kwako au
 
Umezungumza kweli tupu,Nilikuwa naangalia kwenyevgazeti moja la nje ,inaonyesha Kenya ni yavsita duniani kwa kuzalisha maparachichi huku Tanzania ikiwa haimo hata kumi bora.Wakati huo Kenya wanamakampuni yananunua nchini na kuyapeleka kenya.Wakifika huko wanayasafirisha nje kwa label yao!
Nyie ni wajinga,kwanza hao wakenya wanasaidia wakulima kupata soko alafu wananunua kujazia pengo la kwao,kwa taarifa yako wanalima Sana tuu na ndio wamewafundisha wakulima kilimo cha parachichi.

Wasiponunua mtapeleka wapi sasa maana mpo badala ya kuchangamkia fursa mnapiga makelele na kulia Lia,hii nchi imejaa watu wajinga Sana walalamishi na wasio na suluhisho.
 
Serikali ya Kenya walichofanya walipigania na kuwatafutia masoko ya nje wakulima wa maparachichi watu wao na walifanikiwa!
Sasa kwanini wakenya wasije nunua maparachichi tanzania?

Ova
Kenya inatengeneza mazingira afu watu wao wanachangamkia fursa,kule hakuna wajamaa na wajima kama huku Tzn
 
Sabaya huyo wa marehemu alifanya fitina mpaka muwekezaji akatekeleza shamba la Miparachichi pale Kibohehe Estate- Hai. Hiyo wizara haikujigusa hata kidogo na leo shamba limekuwa pori.
 
Kama unamtaka mwendazake mfuate tutolee upimbi wako hapa
 
Ni ujinga na upumbavu uliokithiri kuamini serikali itawezesha exportation. Nitajieni bidhaa moja ya mfani imesimamiwa na serikali na kufanikiwa!
Ukifuatilia historia ya avocado, kenya wamenza kuzilima tangu miaka ya 60 , sisi tumeanza lini ?
Kenya wanamasoko mengi kuliko TZ ila hawawezi kutosheleza soko kao huko nje. Wanamkataba na China kupeleka tani zaidi ya laki moja.
Wana kampuni za kupack vizuri sisi ndio juzi Rungwe kampan tena wazungu ndio wameanza ku process na wana heka 800 tu.
BBC wamesema Nigeria na kenya ndio zina export kwa wingi na Nigeria wanataka kuongoza export in coming ten years.
BBC kuna mkulima wamemuhoji wa uganda ana hekta 1000+, ni mzawa gani Tanzania ana shamba kama hilo ? Wengi vieka viwili (subsistance farming! ), ikizi heka 100.
Kenya wakisusa kuja kununua parachichi kutatokea anguko la bei baya kabisa.
Watanzania tuache kuongea vitu kishabiki bali tutumie data.
Avocado ni biashara inayoendeshwa na makampuni serikali yetu haina mchango wowote wa maana, hivyo watu wanatakiwa waanzishe makampuni ya kusafirisha nje na si kuwazuia wakenya au wachina na wazungu.
Matajiri wa Tanzania waione avocado kama fursa na ikiwezekana waanzishe baadhi ya viwanda hapa hapa Tz ili zisafirishwe product za avocado na si avocado.
Narudia tena serikali haina mchango wowote bali demand ndio imelazimisha kukua kwa kilimo hicho, hawana msaada.
Wakulima wajitafutie masoko kama walivyofanya wakenya, hakuna mwanasiasa wa kukutafutia masoko, hayupo.
 
Back
Top Bottom