DOKEZO Mapato yanapotea, Uhamiaji Manyovu na Tarakea kwa kutumia madaftari kurekodi wageni wa kimataifa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kama mwezi huu nilikwenda Bujumbura, nilipofika Manyovu nikashangaa hakuna mfumo wa uhamiaji kama ukipita uwanja wa ndege au Tunduma. Nikaangalia namna wale maafisa wanavyofanya kazi, nikajiuliza tumelogwa? Wakati huo huo, TRA kwenye kituo hicho hicho, gari lazima usajili kwenye mfumo, unajiuliza uhamiaji wanashindwa kununua hata kompyuta? Mbona wanakusanya pesa lukuki kwenye visa za mtandao, hao wageni wanakaguliwaje? Haiwezi ikawa njia ya kuchepusha mapato.

Mwaka jana tena kule Rombo Tarakea, nilikutana na hii hali, serikali mnashindwa kununua hata kompyuta? Royal tour, mbona inadidimizwa na hii miundombinu yenu isiyofaa? Mdogo wangu Mwigulu ulikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, hii mianya hukuiona?

Lakini pia kimataifa, mgeni akipita pale kwa namna huduma zilivyo, anatudharau sana. Mimi ningekuwa na access au serikali ikitoa utaratibu wa kuchangia kompyuta, nipo tayari kununua hata kumi, zakuanzia kuondoa aibu.

Ila pia kiusalama, sidhani kama ni sawa. Pamoja na kiusalama, mapato yanadhibitiwaje katika mazingira yale? Mama anatangaza royal tour, ila sidhani kama anajua kwamba yapo malango ya kuingia nchini, wageni na wafanyabiashara wakubwa wanaandikishwa kwenye register kama maudhurio ya shule.

Naamini uhamiaji kama ninyi ndio mnaofunga kompyuta, mtabadilika haraka kwenye mipaka yote. Msaidieni mama, haya mambo madogo madogo si ya kusubiri tamko lake, laptop zinauzwa kuanzia milioni, mnakosa milioni hamsini, msambaze laptop kwa maafisa wenu? Waandikishe hata kujaza excel sheet kuliko kutumia madaftari ya kijima.

Kama Kigoma kwa Makamu wa Rais pako hivi, huko Rukwa na Mtwara panafananaje? Huko Kagera, ambako watu ni wengi, hali ipoje?

Badilikeni, lakini pia Mzee Mwigulu fanya mambo, peleka kompyuta faster kudhibiti mapato. Naamini ukitoa hata milioni mia, mipaka yote fedha itarudi muda wa wiki, ila kwa hali ile, hata risiti siwezi kudai.
 
Lakini pia kimataifa mgeni akipita pale Kwa namna huduma zilivyo anatudharau Sana. Mimi ningekuwa na access au serikali ikitoa utaratibu wa kuchangia computer nipo tayari kununua hata Kumi zakuanzia kuondoa aibu .
Wewe ndio mzalendo sana
 
Siyo suala la uzalendo nikubadili mindset tu, lakini pia unaweza kukuta anayetakiwa kupeleka kompyuta kule hata hajawahi kusafiri nje ya nchi.

Mimi naamini kwa ukubwa wa Ofisi za Uhamiaji, haya makompyuta ukifanyika ukaguzi wa kushtukiza utayakuta yapo mengine yamefungiwa kwa mabosi hayana kazi, lakini watu wanaumia.

Maafisa Uhamiaji wana huduma nzuri sana, na nadhani kwa kuwa wanatoa huduma nzuri, mapungufu hatuyaoni sisi tunao safiri. Ila huduma nzuri ziendane na miundombinu mizuri.

Mnawafanya watoto wetu wanaotoa huduma huko mipakani waingie tamaa, mnaanza kuwakamata kwa rushwa, kumbe shida ipo kwa kiongozi mwenye dhamana.

Wapeni fedha wanunue kompyuta, nchi hii siyo ya kukosa pesa. Kwanza majirani zetu wanatuonea wivu; msipofunga mitambo mizuri wataingiza wahalifu na tutaanza kuumizana ndani au kutuumiza ndugu zetu na kukimbiza wawekezaji.

Kongo tunaona na Msumbiji tunaona yanayoendelea, kimbizaneni mfunge mifumo imara, achaneni na akaunti book.
 
Kama mwezi huu nilikwenda Bujumbura, nilipofika Manyovu nikashangaa hakuna mfumo wa uhamiaji kama ukipita uwanja wa ndege au Tunduma. Nikaangalia namna wale maafisa wanavyofanya kazi, nikajiuliza timelogwa? Wakati huo huo, TRA kwenye kituo hicho hicho, gari lazima usajili kwenye mfumo, unajiuliza uhamiaji wanashindwa kununua hata kompyuta? Mbona wanakusanya pesa lukuki kwenye visa za mtandao, hao wageni wanakaguliwaje? Haiwezi ikawa njia ya kuchepusha mapato.

Mwaka jana tena kule Rombo Tarakea, nilikutana na hii hali, serikali mnashindwa kununua hata kompyuta? Royal tour, mbona inadidimizwa na hii miundombinu yenu isiyofaa? Mdogo wangu Mwigulu ulikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, hii mianya hukuiona?

Lakini pia kimataifa, mgeni akipita pale kwa namna huduma zilivyo, anatudharau sana. Mimi ningekuwa na access au serikali ikitoa utaratibu wa kuchangia kompyuta, nipo tayari kununua hata kumi, zakuanzia kuondoa aibu.

Ila pia kiusalama, sidhani kama ni sawa. Pamoja na kiusalama, mapato yanadhibitiwaje katika mazingira yale? Mama anatangaza royal tour, ila sidhani kama anajua kwamba yapo malango ya kuingia nchini, wageni na wafanyabiashara wakubwa wanaandikishwa kwenye register kama maudhurio ya shule.

Naamini uhamiaji kama ninyi ndio mnaofunga kompyuta, mtabadilika haraka kwenye mipaka yote. Msaidieni mama, haya mambo madogo madogo si ya kusubiri tamko lake, laptop zinauzwa kuanzia milioni, mnakosa milioni hamsini, msambaze laptop kwa maafisa wenu? Waandikishe hata kujaza excel sheet kuliko kutumia madaftari ya kijima.

Kama Kigoma kwa Makamu wa Rais pako hivi, huko Rukwa na Mtwara panafananaje? Huko Kagera, ambako watu ni wengi, hali ipoje?

Badilikeni, lakini pia Mzee Mwigulu fanya mambo, peleka kompyuta faster kudhibiti mapato. Naamini ukitoa hata milioni mia, mipaka yote fedha itarudi muda wa wiki, ila kwa hali ile, hata risiti siwezi kudai.
TAIFA LA WAPIGAJI
 
Visa haitolewi na uhamiaji kiongozi
 
Back
Top Bottom