Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Kama mwezi huu nilikwenda Bujumbura, nilipofika Manyovu nikashangaa hakuna mfumo wa uhamiaji kama ukipita uwanja wa ndege au Tunduma. Nikaangalia namna wale maafisa wanavyofanya kazi, nikajiuliza tumelogwa? Wakati huo huo, TRA kwenye kituo hicho hicho, gari lazima usajili kwenye mfumo, unajiuliza uhamiaji wanashindwa kununua hata kompyuta? Mbona wanakusanya pesa lukuki kwenye visa za mtandao, hao wageni wanakaguliwaje? Haiwezi ikawa njia ya kuchepusha mapato.
Mwaka jana tena kule Rombo Tarakea, nilikutana na hii hali, serikali mnashindwa kununua hata kompyuta? Royal tour, mbona inadidimizwa na hii miundombinu yenu isiyofaa? Mdogo wangu Mwigulu ulikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, hii mianya hukuiona?
Lakini pia kimataifa, mgeni akipita pale kwa namna huduma zilivyo, anatudharau sana. Mimi ningekuwa na access au serikali ikitoa utaratibu wa kuchangia kompyuta, nipo tayari kununua hata kumi, zakuanzia kuondoa aibu.
Ila pia kiusalama, sidhani kama ni sawa. Pamoja na kiusalama, mapato yanadhibitiwaje katika mazingira yale? Mama anatangaza royal tour, ila sidhani kama anajua kwamba yapo malango ya kuingia nchini, wageni na wafanyabiashara wakubwa wanaandikishwa kwenye register kama maudhurio ya shule.
Naamini uhamiaji kama ninyi ndio mnaofunga kompyuta, mtabadilika haraka kwenye mipaka yote. Msaidieni mama, haya mambo madogo madogo si ya kusubiri tamko lake, laptop zinauzwa kuanzia milioni, mnakosa milioni hamsini, msambaze laptop kwa maafisa wenu? Waandikishe hata kujaza excel sheet kuliko kutumia madaftari ya kijima.
Kama Kigoma kwa Makamu wa Rais pako hivi, huko Rukwa na Mtwara panafananaje? Huko Kagera, ambako watu ni wengi, hali ipoje?
Badilikeni, lakini pia Mzee Mwigulu fanya mambo, peleka kompyuta faster kudhibiti mapato. Naamini ukitoa hata milioni mia, mipaka yote fedha itarudi muda wa wiki, ila kwa hali ile, hata risiti siwezi kudai.