Mapendekezo: Ajira kwenye Utumishi wa Umma iwe kwa MKATABA

Mapendekezo: Ajira kwenye Utumishi wa Umma iwe kwa MKATABA

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
TUNA TATIZO KUBWA LA HUDUMA DUNI KWENYE TAASISI ZETU ZA UMMA/SERIKALI...KIINI CHA TATIZO NI MFUMO WA AJIRA ZA SO CALLED "PERMANENT AND PENSIONABLE"

Nafahamu Taasisi mbalimbali za serikali zina targets lakini hali haiko hivyo kwa watumishi wao ambao target yao ni kuishi kazini hadi kustaafu.

Tatizo la uduni wa huduma kwenye taasisi nyingi za Serikali/ umma ni MFUMO WA AJIRA kwenye Utumishi wa Umma unaompa mwajiriwa UHAKIKA kwamba akiingia TU ndani ya Utumishi wa Umma basi ni mpaka Kustaafu.

MATOKEO YAKE... hawa watumishi wa umma wamekuwa baadhi yao miunguwatu kiasi kwamba ukifika kwenye ofisi za umma unapata huduma mbovu sana mpaka unashangaa.

Tatizo la huduma mbovu si kosa la taasisi husika ni HULKA tu ya watumishi binafsi wasiojua au wanaojifanya kutojua ni KWANINI WAPO HAPO OFISINI.

Mathalani Mashirika ya Umma yasiyo na ushindani kama vile TANESCO, IDARA ZA MAJI, MAMLAKA YA MAPATO, MIFUKO YA HIFADHI kumekuwa na ujinga mwingi sana wa huduma mbovu kutoka miongoni mwa baadhi ya watumishi.

ILI KUKOMESHA TATIZO HILI SUGU....Nashauri AJIRA KWENYE UTUMISHI WA UMMA iwe kwa mikataba kuanzia mwaka mpya wa Fedha 2022/2023

NAWASILISHA

N'yadikwa
 
Sisi ndio wenye nchi ,usitupangie tutakaa ofcin mpaka tuzeeke na hakuna kitu utafanya ...!
Ila kutoa maoni NIMEFANYA huku nako ni KUFANYA. Bado unaona hakuna kitu nimefanya!?... Hata wewe umefanya kwa kukomenti hapa kwenye SLEDI niliyofanya.
 
TUNA TATIZO KUBWA LA HUDUMA DUNI KWENYE TAASISI ZETU ZA UMMA/SERIKALI...KIINI CHA TATIZO NI MFUMO WA AJIRA ZA SO CALLED "PERMANENT AND PENSIONABLE"

Nafahamu Taasisi mbalimbali za serikali zina targets lakini hali haiko hivyo kwa watumishi wao ambao target yao ni kuishi kazini hadi kustaafu.

Tatizo la uduni wa huduma kwenye taasisi nyingi za Serikali/ umma ni MFUMO WA AJIRA kwenye Utumishi wa Umma unaompa mwajiriwa UHAKIKA kwamba akiingia TU ndani ya Utumishi wa Umma basi ni mpaka Kustaafu.

MATOKEO YAKE... hawa watumishi wa umma wamekuwa baadhi yao miunguwatu kiasi kwamba ukifika kwenye ofisi za umma unapata huduma mbovu sana mpaka unashangaa.

Tatizo la huduma mbovu si kosa la taasisi husika ni HULKA tu ya watumishi binafsi wasiojua au wanaojifanya kutojua ni KWANINI WAPO HAPO OFISINI.

Mathalani Mashirika ya Umma yasiyo na ushindani kama vile TANESCO, IDARA ZA MAJI, MAMLAKA YA MAPATO, MIFUKO YA HIFADHI kumekuwa na ujinga mwingi sana wa huduma mbovu kutoka miongoni mwa baadhi ya watumishi.

ILI KUKOMESHA TATIZO HILI SUGU....Nashauri AJIRA KWENYE UTUMISHI WA UMMA iwe kwa mikataba kuanzia mwaka mpya wa Fedha 2022/2023

NAWASILISHA

N'yadikwa
Vip madeni ya mikopo utawalipia
 
Sisi ndio wenye nchi ,usitupangie tutakaa ofcin mpaka tuzeeke na hakuna kitu utafanya ...!
Mbona mliponyimwa nyongeza ya mishahara mlikuwa kimya mkaufyata. Ni wenye nchi kweli nyie. Inatakiwa mpewe Mikataba ya kazi miaka mitatu mitatu...uki underperform hakuna contract renewal ukalime mpunga kilombero.
 
Vip madeni ya mikopo utawalipia
Hilo ni suala binafsi...hata hivyo tukiwapa mikataba mabenki na taasisi za kifedha zitawakopesha kulingana na ukomo wa mikataba yao kama sie huku private sekta
 
Mi naongelea watumishi umma kupewa kazi kwa mikataba we unaleta story za gratuity...sometimes ni vema kukaa kimya ili kuficha tuujinga tudogodogo kama hutu.
 
Mtumishi wa Umma , akipewa barua ya ajira tu, kwanza anasaini Mkataba ' OVA
 
Mtumishi wa Umma , akipewa barua ya ajira tu, kwanza anasaini Mkataba ' OVA
Baada ya hapo anaenda kuendesha uber salary inaingia...Performance Review almaarufu OPRAS haitoshi kutathmini utendaji wa public servants...mikataba ya muda maalum ndo itasaidia ufanisi.
 
Tutalifanyia wazo lako kazi baada ya mwaka 2050.
 
Pambana uingie serikalini uwe huru kazini. Kama hujaingilia 18 za watu kutekenya 60 ni uhakika.

Mikataba inawahusu diwani, mbunge, rais na wenyeviti wa bodi na wajumbe wao.
 
Mathalani Mashirika ya Umma yasiyo na ushindani kama vile TANESCO, IDARA ZA MAJI, MAMLAKA YA MAPATO, MIFUKO YA HIFADHI kumekuwa na ujinga mwingi sana wa huduma mbovu kutoka miongoni mwa baadhi ya watumishi.
Upo sahihi taasisi na hasa hao wanaojiita mamlaka inapaswa wawekewe masanduku ya kupigiwa kura based on what they deliver to customers
 
Mtaalam una wazo zuri.Kuna tatizo hapa,fikiria mzee alieitumikia nchi yake kwa miaka mingi Hadi kustaafu anacheleweshewa pensheni yake.kukiwa na ajira za mikataba ni kwamba mtu akimaliza mkataba alipwe Haki zake,hapo ndipo serikali inapoogopa.pia mikataba inataka gratuity mtu akitimiza malengo aliyowekewa na mwajiri wake hivyo serikali haitaweza.mtaalam nakuomba pia unitajie nchi hapaduniani ambayo inaajiri kwa mikataba.katika utumishi wa umma kadri mfanyakazi anapo kaa miaka mingi huonekana kuwa mahiri(Bora) zaidi,hivyo wakiajiriwa kwa mikataba itasumbua kuwapata watu mahiri,mtu akimaliza mkataba analipwa mpunga anaanzisha biashara yake.ni hayo tuu kwa Sasa.
 
Tumechelewa mno kwenye hili,mfano ni hao mawakili wa serikali unakuta mwaka mzima kesi zote kashindwa tena Kwa technicalities tu ila hana hata wasiwasi.
 
Back
Top Bottom