SoC01 Mapendekezo: Jinsi Chama cha Mapinduzi kinavyoweza kuwaandaa viongozi waadilifu

SoC01 Mapendekezo: Jinsi Chama cha Mapinduzi kinavyoweza kuwaandaa viongozi waadilifu

Stories of Change - 2021 Competition

Collee

New Member
Joined
Jul 22, 2021
Posts
2
Reaction score
1
CHAMA CHA MAPINDUZI UONGOZI ONLINE COURSE

Chama cha mapinduzi ni chama cha kisiasa nchini Tanzania kilichoundwa mwaka 1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kutoka Tanganyika na Afro Shiraz Party kutoka Zanzibar,chama cha mapinduzi ndio chama tawala nchini Tanzania na chama tawala cha muda mrefu zaidi barani Africa.Tangu kurejeshwa kwa siasa za vyama vingi nchini Tanzania ccm imezidi kuwa maarufu nchini Tanzania na imeshinda chaguzi zote sita 1995,2000,2005,2010,2015,2020,uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 katika nafasi za ubunge ccm ilishinda kwa zaidi ya 90% hivo kuendelea na kuwa na udhibiti wa bunge la taifa.

Chama cha mapinduzi ni moja ya taasisi kongwe, yenye ushawishi na kuheshimika barani Afrika,ushiriki wake katika harakati za ukombozi wa nchi za Afrika kama Zimbabwe,Afrika kusini,Namibia,Msumbiji imeifanya taasisi hii kuwa maarufu na kueshimika sana ndani na nje ya mipaka ya Afrika.

Nchini Tanzania chama cha mapinduzi ndiyo kimekuwa mzalishaji mkuu wa viongozi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya nyumba kumi hadi viongozi wakuu wa kitaifa,hii inatokana na utaratibu mzuri na madhubuti iliyojiwekea taasisi hii katika kupika na kuwaendeleza viongozi kuanzia ngazi ya chipukizi,jumuiya ya vijana,na jumuiya nyinginezo,maandalizi mazuri ya viongozi kupitia taasisi hii kumeifanya nchi ya Tanzania kuwa imara yenye umoja,amani na mshikamano mkubwa hivo kupelekea wananchi kufanya shughuli zao za kijimii,kiuchumi na kisiasa pasipo buguza yoyote kwasababu ya uimara wa viongozi wanaotokana na chama cha mapinduzi.Uongozi ni mamlaka au karama ya kuwaonyesha watu njia kwa vitendo, kiongozi bora ni yule ambaye matendo yake yanawahamisha wengine kupata ndoto zaidi,kujifunza zaidi na kukuwa zaidi,kiongozi anatakiwa kuwa muwazi,mwenye maono,mwadilifu,muwajibikaji, mwenye nidhamu, na anayekubalika na watu anaowaongoza. Katiba ya chama cha mapinduzi imemuelezea sifa za kiongozi kuwa ni mtu mwenye kutosheka asiye na tamaa na anayependa kueneza matunda ya uhuru kwa wananchi wote kwa ajili ya manufaa ya maendeleo kwa taifa kwa ujumla.

Pamoja na katiba ya chama cha mapinduzi kuelezea sifa za kiongozi, katika miaka ya hivi karibuni kumeanza kuzuka kwa baadhi ya viongozi wasio na maadili na miiko ya kiuongozi hivo kuchafua taswira na kuondoa imani ya chama cha mapinduzi kwa wananchi,kuwepo kwa vitendo vya rushwa, ubinafsi,wizi,uvivu na mengineyo ni baadhi ya matendo yanayozidi kushamiri katika baadhi ya viongozi wanaotokana na chama cha mapinduzi jambo ambalo siyo jema kwa ustawi wa chama hiki kikubwa barani Afrika.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na viongozi wanaotokana na chama cha mapinduzi wasiokuwa na mafunzo ya kutosha kuhusiana na chama kwa maana ya historia ya chama cha mapinduzi,imani na madhumuni ya ccm,muundo wa ccm, katiba ya ccm, katiba ya nchi, kanuni za maadili ya viongozi wa uma,na mengineyo hivo kuwapelekea viongozi hawa kufanya mambo ambayo nikinyume na matakwa ya katiba ya chama na katiba ya nchi inayosababisha imani ya chama cha mapinduzi kwa uma wa watanzania kuanza kupungua.

Chama cha mapinduzi Uongozi online course ni mafunzo maalumu yatakayotolewa kwa njia ya mtandao yenye malengo yafuatayo;

Lengo kuu
Kuandaa viongozi waadilifu wanaokijua vema chama cha mapinduzi.

Malengo mengineyo
Kukiwezesha chama kujipatia mapato kwa kupitia ada za mafunzo, matangazo na ada za uanachama.

Kuyachangamsha majukwaa ya kimtandao ya chama cha mapinduzi kama tovuti ya chama cha mapinduzi, ccm app n.k

Lengo kuu
Kuaandaa viongozi waadilifu wanaokijua vema chama cha mapinduzi.

Katika katiba ya chama mapinduzi lengo namba moja ya uanzishwaji wa chama hiki ni kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa na serikali kuui ili kuunda na kushika serikali kuu na serikali za mitaa katika jamuhuri ya muungano wa Tanzania na upande wa Zanzibar,kufanikisha lengo hili linahitaji viongozi waadilifu,wenye maono,nidhamu,ujasiri,kujituma,wenye kupenda maendeleo kwa sababu kiongozi yeyote anayetokana na chama awe mwenyekiti wa Serikali za mitaa, diwani,mbunge n.k ndiyo anakisemea chama kwa wananchi kutokana na matendo yake na mienendo yake,kama kiongozi mzuri,picha wanaipata wananchi kuhusu chama ni kwamba chama ni kizuri pia hivo kurahisisha lengo namba moja la kuanzishwa kwa chama cha mapinduzi la kushika dola, kama kiongozi ni mwizi picha inayojengeka kwa wananchi ni CCM ni chama cha wezi hivo kukwamisha lengo namba moja kuanzishwa kwa chama cha mapinduzi la kushika dola,kumekuwa na changamoto wa uwepo wa baadhi ya viongozi kutofata miiko na maadili ya uongozi yaliyoainishwa katika katiba ya chama cha mapinduzi na kanuni za maadili ya uongozi wa uma,hii inatokana na hahiba ya viongozi wenyewe pia maandalizi hafifu katika kuwaandaa vyema viongozi, hadi sasa hakuna jukwaa lolote rasmi ambalo lipo kwa ajili kuwaandaa na kuwapatia maarifa viongozi wanaotokana na chama cha mapinduzi,wapo baadhi ya viongozi wanaopata nafasi lakini hawakijui vema chama cha mapinduzi kwa maana ya historia, itikadi,madhumuni,katiba n.k chama cha mapinduzi kina amini kuwa binadamu wote ni lakini ni jambo lililozoeleka kwa baadhi ya viongozi wa sasa wa chama cha mapinduzi kudharau nakubagua watu kitu ambacho ni kinyume na imani ya chama cha mapinduzi,hii inatokana na viongozi hawa kutokijua vema chama cha mapinduzi hivo kupelekea kuchafuka kwa taswira nzuri ya chama cha mapinduzi kwa wananchi hivo ccm uongozi online course ni mafunzo yaliyolenga kuwaandaa viongozi wanaokijua vema chama cha mapinduzi wenye nidhamu,uadilifu wanaoziishi fikra za waasisi wa chama hiki

Malengo mengineyo

Kukiwezesha chama kujipatia mapato kwa kupitia ada,matangazo,na ada za uanachama

Chama cha mapinduzi kimekuwa ndiyo daraja kubwa kwa watanzania wenye ndoto za kuwa viongozi,hii inasababishwa na tabia ya chama hiki ya kutoa nafasi za uongozi pasipo kuangalia jinsia, hali,rangi,kabila hivo kuwavutia watu wengi wenye ndoto za uongozi kukitumia chama hiki kama daraja la kutimiza ndoto zao,kwa kutumia faida iliyonayo ya kuaminika na kutumika kama daraja ya watu wenye ndoto ya kuwa viongozi uanzishwaji wa mafunzo haya utawavutia watu wengi kama mafunzo haya yakiwekewa mazingira mazuri hivo kukiwezesha chama kujipatia mapato kwa kupitia ada za mafunzo, kwa mfano katika uchaguzi wa 2020 watanzania waliojitokeza kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya ubunge walikuwa 10367, kwa wabunge hawa kama gharama za mafunzo ni shilingi laki moja chama kingeweza kupata zaidi ya bilioni moja kama ikiwekwa ulazima wa mafunzo haya na hii bilioni moja ni kwa wabunge tu achana na madiwani na wenye viti wa serikali za mitaa. Pia kuna fursa nyingine ya mapato yatokanayo na matangazo kwa kuwa mafunzo haya yatatolewa kwa njia ya mtandao itaongeza idadi ya watu wanaofatilia tovuti ya chama na CCM app hivo kuwavutia wafanyabiashara kutangaza bidhaa zao mbalimbali kwa kupitia tovuti na CCM app. Moja ya kigezo cha kupata mafunzo haya ni lazima uwe mwanachama wa chama cha mapinduzi na usiyodaiwa ada ya uanachama mfumo wa mafunzo utawakubali wanachama waliolipia ada zao za uanachama hivo kusaidia wanachama kulipia ada zao za uanachama.

Kuyachangamsha majukwaa mengineyo ya chama cha mapinduzi kama vile tovuti na CCM app.

Kwakuwa mafunzo haya mafunzo haya yatatolewa kwa kutumia tovuti ya chama na c.c.m app itasaidia kuyachangamsha majukwaa haya nakuyafanya yawe yanatembelewa mara kwa mara hivo kuwawezesha watanzania kupata taarifa nyingine muhimu zinazopatikana kwenye majukwaa haya kama utekelezaji miradi mbalimbali,nafasi za tenda na kazi n.k

JINSI MAFUNZO HAYA YATAKAVYOTOLEWA

Yatatolewa kwa njia mtandao kwa kupitia tovuti ya chama cha mapinduzi na c.c.m app ili kutoa fursa ya wana c.c.m waishio ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kujipatia mafunzo haya.

Mafunzo haya yatatolewa kwa njia ya video pia mwanafunzi wa mafunzo haya atalazimika kudownload baadhi ya notes.

Maafisa waandamizi wa chama waliopo na wastaafu ndio watakuwa waalimu wa mafunzo haya.

Mafunzo haya yatakuwa ya miezi minne na muhitimu atalazimika kufanya mtihani kupitia ofisi za wilaya za chama anapoishi na kutakuwa na cheti kitachotolewa baada ya kuhitimu mafunzo haya.

Kutokana na umuhimu wa mafunzo haya kwa mustakabali wa ustawi wa chama na nchi kwa ujumla chama kinaweza kuweka mazingira ya ulazima wa mafunzo haya, kwa mfano 2030 mwana CCM hasiyekuwa na cheti cha mafunzo haya hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote pia kupata uteuzi kwa kupitia chama cha mapinduzi.


FAIDA ZA CCM UONGOZI ONLINE COURSE

Chama cha Mapinduzi kupata viongozi waadilifu na wenye nidhamu watakaosaidia maendeleo ya chama na nchi kwa ujumla.

Wanachama wa chama cha mapinduzi kupata nafasi ya kukijua vema chama chao kwa maana ya historia,itikadi,imani,katiba n.k

Chama cha mapinduzi kujipatia mapato yatakaotokana na ada za wanafunzi, matangazo na ada za uanachama.

Kutoa fursa kwa wana c.c.m wanaishi nje ya mipaka ya Tanzania wenye ndoto za kuwa viongozi kupata mafunzo haya muhimu!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

COLLINS AUDAX,0788947141,audaxc@yahoo.com

August 2021
 
Upvote 1
Back
Top Bottom