Mapendekezo: Karibuni tupunguze ukubwa wa Serikali

Mapendekezo: Karibuni tupunguze ukubwa wa Serikali

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habari wandugu. Kwa sasa na maisha na uchumi wa dunia ni mgumu sana. Kila mtu anatakiwa kujibana. Hivyo na Serikali nayo inatakiwa kujibana. Ili kupunguza matumizi, inahitajika ukubwa wa serikali nao upungue. Leta maoni juu ya namna ya kupunguza ukubwa wa serikali. Mimi maoni yangu.

1. Cheo kimoja, kati ya waziri mkuu au makumu wa Rais kifutwe. Tumeona nchi inakuwa na waziri mkuu au makamu wa rais, si wote.

2. Unaibu waziri ufutwe. Kuna watu wengi wa kufanya kazi kutoka wizarani hadi huku chini. Hakuna haja ya hicho cheo.

3.......
 
Wabunge viti maalum wapunguzwe
Wamekua wengi sana, na hamna wanacho fanya pale mjengoni
 
FUTA wizara nyingi tu tubaki na 12 tu Wizara zilizofutwa zinakuwa idara ktk hizo wizara 12. Mfano, wizara ya muungano inakuwa idara ktk wizara ya nchi za nje etc.
 
FUTA wizara nyingi tu tubaki na 12 tu Wizara zilizofutwa zinakuwa idara ktk hizo wizara 12. Mfano, wizara ya muungano inakuwa idara ktk wizara ya nchi za nje etc.
Kabisa. Tunahitaji wizara chache tu.
 
Futa cheo cha mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya. Kua na cheo cha katibu wa mkoa au wilaya wao watafanya kazi na madiwani wa kila kata kusaidia kuleta maendeleo.

Futa cheo chote cha uwaziri na umakamu wake, kua na katibu na naibu katibu wa wizara wenye uelewa kuhusu professional. Wabunge wabaki na kazi ya kukosoa serikali na kuonya na kuhoji.
 
Habari wandugu. Kwa sasa na maisha na uchumi wa dunia ni mgumu sana. Kila mtu anatakiwa kujibana. Hivyo na serikali nayo inatakiwa kujibana. Ili kupunguza matumizi, inahitajika ukubwa wa serikali nao upungue. Leta maoni juu ya namna ya kupunguza ukubwa wa serikali. Mimi maoni yangu.

1. Cheo kimoja, kati ya waziri mkuu au makumu wa Rais kifutwe. Tumeona nchi inakuwa na waziri mkuu au makamu wa rais, si wote.
2. Unaibu waziri ufutwe. Kuna watu wengi wa kufanya kazi kutoka wizarani hadi huku chini. Hakuna haja ya hicho cheo.
3.......
Swali Kwa mleta uziunaiamini rasimu ya katiba mpya,maoni ya wananchi ya Mzee Warioba au laaa🤔
 
Back
Top Bottom