Mangi Mashingia
New Member
- Apr 25, 2025
- 1
- 0
Salam sana wana jamvi,
Awali ya yote nawasalimu Watanzania wenzangu kwa kupitia jukwaa hili. Nikiwa ni mpenzi wa kufuatilia sisasa za Tanzania, hususani vipindi vya uchaguzi kwa kweli naona kuna mengi ambayo kila chama cha siasa kinayafanya kwa lengo la kupata madaraka/ kuunda serikali kupitia sauti za wananchi kwa njia ya kura.
Nianze kusema kwamba, nimefanikiwa kuisoma ILANI ya CCM yenye kurasa 86, kimsingi ni ilani nzuri ambayo kila mchambuzi wa sayansi ya siasa ataikubali kwa kiwango chake. Kwa kweli iwapo vipaumbele vya ILANI hii vitatekelezwa, basi TANZANIA iliyostawi zaidi itaonekana kwa miaka 5 hadi 25 ijayo kwa kuzingatia dira mpya ya Taifa- 2050.
Kwa ushauri wangu, ILANI ni nzuri, ila haitekelezwi na CHAMA, bali itatekelezwa na SERIKALIitakayoingia madarakani kwa niaba ya CCM au chama kitakachokuwa na majority votes. Hivyo ili kuhakikisha kuwa ILANI hii inaleta matokeo tarajiwa, basi ni vizuri CCM iunde kitengo maalumu kitakachokuwa na jukumu la kufuatilia utendaji wa Serikali katika kutekeleza ILANI hii.
Kitengo hiki kiitwe ' Monitoring, Accountability, Evalaution and Learnng of CCM's manifestal' Kitengo hiki kiwe na wataalumu wa kisekta, na wawe kila mkoa na wasiingiliwe na viongozi wa walichaguliwa na wananchi (Wabunge, madiwani nk), bali wapewe hadidu za rejea ambazo ndio zitakuwa msingi wa kufuatilia na kutoa taarifa za kiutendaji KUTOKA kwa Serikali itayokuwa madarakani, wabunge, madiwani nk na kutoa internal independent report kila baada ya miezi sita.
Hii itasaidia kupata taarifa sahihi za mwitikio wa uhilisia wa mtazamo wa raia kuhusu viongozi wao wa Kisiasa na hivyo kukipa chama wakati mzuri wa kurekebisha, kuonya na kujipanga kupata viongozi wawajibikaji ( responding to people's needs), msingi huu utaimarisha imani ya wananchi kupitia CCM na hivyo kuendelea kuimarika katika tasnia ya siasa, uchumi, huduma za jamii na mendeleo jumuishi.
ILANI ni nzuri sana, bado naendelea kusubiri na kusoma ilani za vyama vingine, ..
PONGEZI kwa timu iliyoandaa ilani hii.