Elections 2010 Mapendekezo kwa CCM kufuatia "the Walkout"...

CCM walikupa nini?
 
Badala ya CCM kutuambia wataenda lini mahakamani kuomba Mahakama iwaadhibu CHADEMA kwa kuvunja sheria za nchi(Kama zipo zilizovunjwa)kwa kusema HAWAMTAMBUI Rais JK kama Rais halali wa TZ na baadae kutoka nje alipoanza kuhutubia Bunge lkn nilichokiona ni msemaji wa CCM Chiligati akisema chama chake kitapeleka mswaada Bungeni akiomba Bunge liwafukuze CHADEMA Bungeni!

Swali langu;
Kama CHADEMA wamevunja sheria yeyote kwa maamuzi yao yote 2 kwa nini hadi sasa hawajafikshwa mahakamani na badala yake tunaambiwa CCM itapeleka mswaada wafukuzwe Bungeni

Kama hamna sheria yeyote waliyovunja;CHADEMA wanasakamwa kwa lipi?
 
Hivi wakiwafukuza Bungeni halafu majimbo yakiwa wazi wanafikiri CCM watashinda majimbo hayo; wataenda kwenye uchaguzi mdogo na Chadema watashinda tena kwa kunyanyasa na kurudi Bungeni, watawaapisha, halafu Chadema hawatomtambua tena.. na CCM itawafukuza tena, tutaenda kwenye uchaguzi mdogo, and walaaaa 2015


CCM watumie hekima badala ya nguvu.. ndicho alichoomba Solomon
 
Tofauti ilitakiwa iwepo lakini unfortunatelly kwa CCM mwenyekiti wa chama ndio mkuu wa serikali. Kwahiyo hakuna tofauti hapo, swala la kumtambua kabla ya kuanza mazungumzo haliepukiki.
Unaweza kufanya mazungumzo na mamlaka usiyoitambua. Ilishatokea Afrika kusini. ANC hawakutambua utawala wa makaburu lakini hatimaye walifikia muafaka.
 
Watanzania acheni uoga, historia inatufundisha kwamba haki upiganiwa, For those who have had an opportunity to learn Develpoment studies they will agree with me that conflict is inherent in the course of development, likewise conflict is inherent in the nature of politics. Conflict inayoongelewa hapa si lazima yawe mapigano, hata mgongano wa mawazo ni conflict ambazo zikijitokeza watu wenye busara hukaa chini na kuzungumza kufikia compromise. Inapotokea kundi moja likawa kichwa ngumu kama CCM inavyoonyesha ndo kundi la pili hufikia kushika mtutu ili kutetea haki yake.

Naona pia watu waelewe kwamba kama utajua kwamba mtu fulani anakudhulumu haki yako alafu ukakaa kimya bila kujitetea, hata siku ya kihama mungu hatakusamehe, hii ni imani ya dini zote

After all kwa wale wanojua computer watakubaliana a mimi kwamba ikiwa operating system ni mbovu usitegemee kama software zitafanya kazi vizuri. Operating system ndiyo kiungo kati ya software na hardware, kwa maana hiyo tukiwa na mfumo (operating system) - katiba, sheria, na taratibu mbovu usitegemee watendaji (software) wataweza kufanya kazi inavyotakiwa. Kwa hiyo mabadiliko yanayopiganiwa ni kwa manufaa ya watu wote wa nchi hii si wanachadema tu.

Pia ni vizuri wanaCCM wakatambua kwamba sheria mbovu zitakuja siku ya siku zitawatafuna wajukuu na vitukuu vyao na watawalaaniwa wakati wao wako makaburini. Put your country first
 

nafikiri watu bado hawajawaelewa Chadema, viongozi wake ni watu makin sana, sasa ukichukua tu propaganda za CCM utakuwa umepotea. Msimamo wwa Cahdema ni kuwa hawana shida na Kikwete kama yeye, na kuwa wanafahamu sheria kuwa NEC ikishatangaza hakuna mahali unapoweza kupinga. Sasa zingatia yafuatayo:

1. Chadema wanatambua kuwa JK ni Rais isipokuwa wanachokataa ni matokea yaliyomweka madarakani. Ni Rais kwa kuwa ametangazwa na NEC na hakuna mahakama inayoweza kubatilisha.

2. Kinachopiganiwa sasa ni kubadilisha mfumo huu unaoweza kumweka madarakani mtu ambaye hakuchaguliwa na watu. Na wanaonyesha ukweli huo kwa takwimu za kura zilizopigwa vituoni na zile zilizotangazwa na NEC

3. Kinachopiganiwa ni kuandikwa kwa katiba mpya na kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi. Hiki ni kilio ambacho wapinzani wamekilia kwa muda mrefu lakini CCM wameweka pamba masikioni. Ili hili lililotokea lisionekane katika uchaguzi ujao hili ni la lazima. Nakumbuka kuna wakati CUF waliandamana kudai tume huru lakini baada ya ndoa yao na CCM hawalisemi kabisa hili.

4. Kama CCM itajali hili na kuanza mara moja mchakato wa kuweka katiba mpya, misuguano itakuwa imekwisha, lakini kama CCM watakaidi kilio hiki wawe na uhakika kuwa matukio mengi na migawanyiko ya taifa itaendelea kulitesa taifa hili na kamwe agenda ya maendeleo haitapata nafasi kabisa.

KATIKA UMOJA WETU WATANZANIA BILA KUJALI ITIKADI ZETU ZA KISIASA TUJALI TANZANIA YA KESHO, AMBAPO WATOTO WETU WATAISHI KATIKA MAELEWANO NA UHURU NA HAKI.
 
Hawa wenzetu ( ambao sio wenzetu ) hawajaelewa somo, historia haijawafunza chochote, wasubiri waone matokeo ya ubabe wao ni nini, asifikiri watanzania ie watanganyika ni wajinga na wapole hivyo! ikifikia hatua ya enough is enough watatafuta kwa kukimbilia na hawatakuona. nawakilisha, ninahasira kuliko !!!!
 
Ipo siku historia itatuhukumu sisi wote na pia najua kuwa kuna siku watu wote tutajua kwanini CHADEMA walifanya hivyo
 


Una mawazo ya kike!
 

acha pumba wewe
 

You are right MMM kama kiongozi wa nchi atafuata maopportunist katika ushauri hakika itaonekana kuwa ni yy ndo anayekosea maana public inamwona yy zaidi. Mambo yakiwa magumu still ni yy ndiye atakayebebshwa lawama na hao maopportunist watakuwa wakwanza kumrushia mawe tena mazito ili kummaliza kabisa asipate nafasi ya kuwa expose.

Mtu anapokata tamaa yeyote anayeongea jambo linaloendana na matarajio/matamanio yake hata kama practically haliwezekani kwake yy huyo ni hero! Na baya zaidi ni pale huyo hero atakapo kuwa na yeye ni mpanda kupitia mabega ya wengine kufufil interest zake.

CCM wana somo zuri la ufisadi pale wachache wao walipoteka hii agenda from upinzani walionekana heroes; whether truly they were its a matter of discussion; and in the same way wasipo ona hii ni opportunity ya wao kujijenga kwa kufanya yanayokubalika basi wajue CCM haitabaki salama na unfortunately CCM iki yumba katika msingi ya utawala wakati huu hakuna smooth transition (Mungu epusha mbali). Kwani it is CCM and CCM only which is in a better position to bring a smooth transition kuelekea democracy ya kweli. Mwenye kuchukia na achukie mwenye kukataa na akatae 'Hiari yashinda utumwa'
 


SWALI langu dogo tu, je, hayo unayoyasema wanayajua? NIliwahi kusoma makala moja iliyokuwa inahusu kupanda kwa gharama ya kununua mkate huko UFARANSA watu wakaandamana na kupiga kelele, basi mke wa mtawala akamuuliza mumewe hivi kwa nini hao watu wanaandamana? yule mtawala akamwambia eti mkate umeadimika, Yule mama akasema kwa nini wasile keki?

sasa, huenda hayo uliyoyachambua hawayajuwi?
 

Hiyo underlined ni kauli yako wewe lakini si ya viongozi wa Chadema (with exception of Zitto Kabwe).

Mahitaji ya katiba mpya nakubaliana nayo lakini natoa angalizo kama ifuatavyo:
1. Katiba iliyopo haijaruhusu tume ya uchaguzi kumtangaza mgombea mwenye kura chache kuwa mshindi. Hivyo basi, kama hilo lilitokea, lilikuwa ni kinyume cha katiba. Hata ikija katiba mpya haitakuwa tiba ya hulka za kutokuheshimu sheria.
2. Mahitaji ya katiba mpya hayatekelezwi kwa kumdhalilisha yule unayetaka majadiliano naye. Kitendo cha kutoka wakati Rais anatoa hotuba, pamoja na kufikisha ujumbe wa kutokumtambua, pia umemdhalilisha. Je, unatarajia response gani toka kwa mtu uliyemdhalilisha? Chadema wamejiweka katika mahali ambapo ni lazima wakubali kumtambua Rais kabla mijadala mingine haijaendelea.
 

Na wewe hebu taja vifungu vya sheria na kanuni sio bla bla hapa. Nchi inaongozwa kwa sheria hii na si vinginevyo.

Kudhalilisha is a relative term, mie hapa naona unajidhalilisha tu.
 
Na wewe hebu taja vifungu vya sheria na kanuni sio bla bla hapa. Nchi inaongozwa kwa sheria hii na si vinginevyo.

Kudhalilisha is a relative term, mie hapa naona unajidhalilisha tu.

Kiongozi Chesty,
Unahitaji kipengele cha sheria cha kujustify lipi kati ya niliyoandika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…