SoC02 Mapendekezo kwa Serikali yatakayobadili mfumo wa elimu

SoC02 Mapendekezo kwa Serikali yatakayobadili mfumo wa elimu

Stories of Change - 2022 Competition

tenachew

Member
Joined
May 27, 2021
Posts
10
Reaction score
11
Mfumo wa elimu inahusisha sera na Sheria zote zinazoongoza mwenendo wa uendeshaji shughuli zote za elimu nchini. Makala hii ni andiko linalotoa mapendekezo Kwa serikali na wadau wengine wa elimu yatakayobadiri na kuboresha mfumo wa uendeshaji shughuli zote za elimu Kwa ngazi zote za elimu nchini Tanzania. Andiko hili ninatoa udhaifu wa mfumo unaotumika Kwa Sasa ambao unaonekana kukosa kuwaandaa wahitimu kuyakabiri maisha ya kujiajiri Kwa kuonyesha changamoto zake na kutoa mapendekezo ya kuboresha.

Mfumo wa elimu uliopo Kwa sasa nchini ni mfumo unaoonekana kutotoa suluhisho Kwa changamoto zinazowakabili wahitimu hasa za kukosa ajira, kukosa mtaji wa kujiajiri, kukosa uwezeshwaji wa kutekeleza Kwa vitendo mawazo na ujuzi wanaoupata baada ya kuhitimu, mazingira dunu ya kufikia haduma za msingi za kuwawezesha kujiajiri, sera hafifu isiyojali mahitaji ya msingi ya wahitimu na isiyotatua changamoto zinazowakwamisha kuonyesha ujuzi waliopata na mambo mengine yatakayopendekezwa katika andiko hil Pamoja na changamoto hizo Kwa wahitimu, yafuatayo ni mapendekezo kwa serikali na wadau wa elimu ili kuleta mapinduzi katika mfumo wa elimu.

Serikali itengeneze dira ya nchi.
Dira ya nchi ni mwongozo unaotoa mwelekeo na vipaumbele vya kufanya Kama taifa kwa kipindi fulani. Hii dira ndiyo itakayoamua na kutoa mwelekeo wa kupanga na kuelekeza vipaumbele vya rasilimali na amali za nchi . Hii itasaidia watunga sera za elimu kuona mwelekeo wa vipaumbele vya nchi na kuepuka mabadiriko ya kisiasa yanayoleta athari kwa mfumo wa elimu.

Hii ni kumaanisha kuwa mfumo wa elimu usiathiriwe na utashi wa viongozi ambao huja na kupita. Tukiwa na sera moja inayofuata dira ya nchi itafanya viongozi wakiingia wasibadirishe mfumo Kwa kufuata utashi wao bali watende kufuata dira ya nchi.

Serikali iwekeze kwenye mawazo na tafiti zinazofanywa na wahitimu
Wahitimu na wadau mbalimbali wa elimu wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali wakitoa mapendekezo ya kina juu ya changamoto na mambo ya kufanya Ili kuboresha mfumo wa elimu. Tafiti hizi hufanywa kwa kuhusisha mawazo na ushauri wa wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa elimu hiyo.

Tafiti hizi ndizo zimejaa mapendekezo ya msiki, hivyo serikali na wadau wa elimu watoe kipaumbele kwa kuwekeza katika mawazo na tafiti hizi ili mfumo wa elimu uandaliwe Kwa kuhusisha mahitaji na kilenga kutatua changamoto za kukosa ajira , kukosa ujuzi wa vitendo na kubaki na elimu ya kinadharia isiyokidhi mahitaji ya jamii.

Kufanya mabadiriko katika elimu ya juu . Mabadiriko yanayopendekezwa katika elimu ya juu ni yale ya kutatua ukosefu wa ajira na ukosefu wa mtaji Kwa wahitimu. Mfumo wa sasa wa elimu unatoa mkopo Kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Hii ni kumaanisha kuwa serikali inao uwezo wa kuwahudumia wanafunzi kifedha hata Kwa kuwakopesha.

Napendekeza serikali itengeneze mfumo wa kutoa mkopo Kwa Kila mwanafunzi anaehitimu Ili anapomaliza chuo asibaki mtaani na elimu yake bali ajiajiri bila kukwamishwa na ukosefu wa mtaji. Kwa mfano serikali hutoa karibia au zaidi ya million 2 Kwa kwanafunzi Kwa mwaka kwaajili ya kujikimu Kwa maisha ya chuo . Je inashindwaje kutoa hizo million 2 au 3 siku mwanafunzi anaehitimu ili ajiajiri? Inawekekana kabisa hii ndio maana natoa pendekezo hili.

Serikali ifanyie tathimini mfumo wa elimu Kila Baada ya miaka 5 au 10. Kufanyia tathimini mfumo wa elimu Kwa Kila baada ya kipindi fulani itasaidia kujua changamoto , madhaifu na kuweza kuboresha Kwa kuzitatua changamoto hizo na kuleta mabadiriko ya kuakisi mahitaji ya watu. Kufanyia tathimini mfumo wa elimu pia itasaidia kuongeza katika mtaala vitu vya msingi vinavyogusa changamoto zinazowakabili wananchi na pia itaondoa hali ya mazoea inayosababisha watu, serikali na wadau wa elimu kujisahau na kutosheka na mfumo uliopo hata kama hautoi utosherezi wa mahitaji ya jamii.

Serikali iwekeze katika elimu ya vitendo. Hii pia imepigiwa kelele na wadau wengi hasa bungeni ambapo sauti zao bado hazisikiki vya kutosha. Mfano mzuri wa wadau hai ni mbuge wa Jimbo la kahama mweshimiwa Kishimba na Mbuge wa Jimbo la Geita V. Mweshimiwa Joseph Msukumu ambao wanapendekeza pia watoto wafundishwe Kwa vitendo kukabili changamoto zinazoikabili jamii na kukusa mahitaji ya jamii. Mfano watoto wafundishwe Kwa vitendo kutengeneza mbolea, kutengeneza lishe, kuchakata maligahafi kuwa bidhaa na kuwa elimu yote Kwa ujumla ihusishe vitendo .

Yaani mtoto afundishwe darasani mfano ukichukua caustic soda+ mafuta ya mawese = sabuni . Hii itasaidia wahitimu kuwa na ujuzi unaowapa kujiajiri kuliko elimu wanayobaki nayo tu kichwani wakishinda WhatsApp na earphone masikioni. Elimu ya vitendo itawajengea uwezo wahitimu kuitumia elimu yao kuwasaidia ndugu na jamii kwa ujumla.

Pia jamii iwekeze katika viongozi watakaoleta mabadiriko ya kivitendo.Hapa jamii pia naishauri kufanya uamuzi makini na wa busara kuhakikisha inasimamisha viongozi watakaosimama kwa ujasiri kutekeleza sera na mfumo bora utakaoandaliwa Ili kuhakikisha jamii inafikia maendeleo na matamanio yake ya kuwa na maisha bora yatokanayo na ubora wa elimu itolewayo. Serikali imara inatokana na jamii imara , hivyo mpenzi msomaji, wewe ni jamii na jamii ni wewe hivyo maamzi sahihi yanaanza na wewe .

Elimu ni kama ngao inayowangazia watu kupita njia ya giza isiyopitika bila mwanga. Hivyo naishauri serikali, Nuru pekee inayoweza kuwekeza Kwa watu wake ni elimu na elimu bora inatokana na mfumo bora wa elimu. Mfumo bora wa elimu utaisimamia elimu bora idumu kuwa bora ikiendelea kuiangazia jamii kuniona njia sahihi ya kufikia maisha bora. Pia nawasihi jamii na wadau wote wa elimu kuendelea kushirikiana na serikali katika kuleta mageuzi yatakayoboresha mfumo wa elimu na kukinusuru kizazi hiki.

Asanteni sana.

Phone: +255621282979
 
Upvote 2
Back
Top Bottom