Mapendekezo kwa TBS ili kuzuia matumizi ya kemikali ya Ethylene katika kuivisha ndizi kwa muda mfupi na kuokoa afya za walaji

Mapendekezo kwa TBS ili kuzuia matumizi ya kemikali ya Ethylene katika kuivisha ndizi kwa muda mfupi na kuokoa afya za walaji

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Kwa yeyote anayefuatilia vyombo vya habari nchini Tanzania bila shaka atagundua kuwa siku chache nyuma kumekuwa na taarifa kwamba kuna baadhi ya wafanyabiashara wanatumia gesi ya Ethylene kuivisha ndizi zao.

Sasa kama kuna mamlaka ambayo inahusika ina jukumu muhimu katika kuhakikisha usalama na ubora wa chakula nchini Tanzania ni Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS)

Katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na mjadala kuhusu matumizi ya gesi ya ethylene ili kuivisha ndizi kwa haraka mjini Dar es Salaam ni wazi kuwa TBS inatakiwa kuchukua hatua madhubuti kushughulikia suala hilo.

Kwa wanaofahamu, Ethylene ni homoni ya mimea inayotumika sana katika kilimo. Ingawa TBS imehakikishia umma kuhusu usalama wa ethylene, ni muhimu sana kwa taasisi hiyo kufanya mapitio ya kina kuhusu matumizi ya Ethylene ili kuboresha viwango vya usalama wa chakula.

Soma pia:
Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

Kwanza kabisa TBS inapaswa kuanzisha kanuni za kueleweka ambazo zitahakikisha kuwa ethylene iliyothibitishwa pekee ndiyo inatumika katika upandaji ndizi.

Hii itasaidia kuondoa hatari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi ya ethylene isiyo na ubora, ambayo inaweza kuleta madhara. Ili kufanikisha hili TBS inaweza kufanya kazi na watengenezaji pamoja na wasambazaji wa Ethylene.

Aidha TBS inaweza kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vituo vya uzalishaji Ethylene ili kuhakikisha kuwa sheria za uzalishaji zinazingatiwa. Ukaguzi huu unapaswa kuhusisha uchambuzi wa sampuli mbalimbali za ethylene ili kuhakikisha kuwa gesi hiyo inakidhi viwango vya usafi vilivyowekwa.

Kufanya hivyo kutasaidia kubaini mapema matatizo yoyote yanayoweza kuathiri ubora wa ndizi na afya ya walaji.

Pia ni muhimu kwa TBS kuanzisha miongozo ya wazi itakayozuia matumizi ya ethylene iliyozidi kiwango cha chakula. TBS inapaswa kufanya upimaji wa mara kwa mara wa sampuli za ethylene, kitu ambacho kitasaidia kupunguza hatari za kiafya zinazohusiana na matumizi ya kemikali zisizo salama, ambazo zinaweza kuathiri afya ya walaji.

Soma pia:
Kemikali ya ethylene hutumika kwenye kuivisha ndizi

Njia nyingine ni kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara na wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia ethylene safi. Kuelewa athari za uchafuzi wa kemikali kwenye ndizi kutawasaidia wafanyabiashara kufanya maamuzi sahihi. Mafunzo haya yanaweza kujumuisha warsha na semina zinazohusisha wataalam wa afya na usalama wa chakula.

Ndz.png

Kwa kufuata mapendekezo haya na mengine mengi ambayo sijayataja hapa, TBS inaweza kuboresha viwango vya usalama wa chakula na kuhakikisha walaji wanapata ndizi zenye ubora na salama.
 
Mkuu, by nature mimea huzalisha ethylene ambayo huivisha matunda na hata usipoweka by default mmea wenyewe utazalisha. Si ndizi tu, apples, papai, maembe n.k yote hutumia kemikali hii kuivisha matunda.

So binafsi sioni kama kuna shida. Si kila kemikali ni sumu.
 
Back
Top Bottom