Mapendekezo: Serikali ibadilishe madaraka ya mkuu wa mkoa na yasiingiliane kabisa na Jeshi la Polisi

Mapendekezo: Serikali ibadilishe madaraka ya mkuu wa mkoa na yasiingiliane kabisa na Jeshi la Polisi

Vyeo vya RC havitumiki tena Duniani ni vyeo vilivyopitwa na wakati hata hapo nchi jirani ya kenya wamepiga hatua kimarndeleo kwa sababu hawatumii mfumo wa kuwa na wakuu wa mikoa, Nchi nyingi Duniani hutumia mfumo wa kuwa na Gavana kwenye majimbo yaani zile kanda kubwa na ktk mikoa huwa na Meya wa kuchaguliwa pia wilaya huwa na meya wa kuchaguliwa hata South Africa wanatumia huo mfumo ni aina Fulani ya utawala bora na wenye nafuu kuliko kuwa na wakuu wa mikoa kibao wanaligharimu Taifa mapesa kibao kwa kazi ambazo ni rahisi zingeweza kufanywa na mamea wa kuchaguliwa.
 
Habari wakuu.

Nafikiri umefika muda wa Serikali yetu kuliangalia hili suala la wakuu wa Mikoa kuwa wenyeviti wa kamati za ulinzi za mikoa, haya ni madaraka yanayoingiliana moja kwa moja na Jeshi la Polisi, na wote tunajua ya kuwa wateule hawa wengi wao hawana mafunzo ya kijeshi, hata kwenye maamuzi na vikao vya Jeshi la Polisi hawatakiwa kabisa kuhudhuria sababu ya itikadi zao za kisiasa, hii ni moja ya sababu kuu inayofanya jeshi letu tukufu kudharauliwa na kushushiwa heshima yake.

Nawasilisha hoja, niko tayari kurekebishwa kwa mwenye ufahamu wowote kuhusu hili .
Polisi wanahusika na usalama tu kumbuka
 
Aisee...! Kazi ipo
Kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wakati mwingine DC au RC hujenga Urafiki na Watu wa usalama na pia wale wa Takukuru, matokeo yake humlinda kwa kila baya na madhambi yake yote, ni mfumo ambao unahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu kwani umewafanya usalama wa taifa mkoa na wilaya kukosa uhuru wa kufanya kazi zao ipasavyo wakihofia kujenga chuki toka kwa wakuu wa wilaya na mikoa
 
Serikali ipo kikatiba na mabadiliko makubwa maana yake ni mabadiliko ya katiba. Msimamo rasmi wa serikali ni katiba (mpya) sio kipaumbele chake.
Katiba mpya kwa awamu hii ya tano ni ndoto ni vigumu mtukufu akubali kuunda katiba mpya
 
Back
Top Bottom