Mapendekezo: Serikali ibadilishe madaraka ya mkuu wa mkoa na yasiingiliane kabisa na Jeshi la Polisi

Vyeo vya RC havitumiki tena Duniani ni vyeo vilivyopitwa na wakati hata hapo nchi jirani ya kenya wamepiga hatua kimarndeleo kwa sababu hawatumii mfumo wa kuwa na wakuu wa mikoa, Nchi nyingi Duniani hutumia mfumo wa kuwa na Gavana kwenye majimbo yaani zile kanda kubwa na ktk mikoa huwa na Meya wa kuchaguliwa pia wilaya huwa na meya wa kuchaguliwa hata South Africa wanatumia huo mfumo ni aina Fulani ya utawala bora na wenye nafuu kuliko kuwa na wakuu wa mikoa kibao wanaligharimu Taifa mapesa kibao kwa kazi ambazo ni rahisi zingeweza kufanywa na mamea wa kuchaguliwa.
 
Polisi wanahusika na usalama tu kumbuka
 
Aisee...! Kazi ipo
Kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wakati mwingine DC au RC hujenga Urafiki na Watu wa usalama na pia wale wa Takukuru, matokeo yake humlinda kwa kila baya na madhambi yake yote, ni mfumo ambao unahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu kwani umewafanya usalama wa taifa mkoa na wilaya kukosa uhuru wa kufanya kazi zao ipasavyo wakihofia kujenga chuki toka kwa wakuu wa wilaya na mikoa
 
Serikali ipo kikatiba na mabadiliko makubwa maana yake ni mabadiliko ya katiba. Msimamo rasmi wa serikali ni katiba (mpya) sio kipaumbele chake.
Katiba mpya kwa awamu hii ya tano ni ndoto ni vigumu mtukufu akubali kuunda katiba mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…