Mapendekezo ya CCM kuhusu kwa tume ya katiba haya hapa ....

Mapendekezo ya CCM kuhusu kwa tume ya katiba haya hapa ....

Naomba kuwaletea baadhi ya vipengele ambavyo CCM wametoa mapendekezo yao kwenye tume ya Warioba ...makubwa yaliyopo ni kuhakikisha kuwa status quo inaendelea kuwepo kama hali ya sasa kuanzia kwenye Muungano na madaraka ya Rais .

katika kifungu 25(2)...wao wanasema kuwa kusafirisha binadamu sio kosa kisheria , hivyo lisping we maarufuku na katiba

kifungu, 62 Znz iruhusiwe kujiunga na Jumuiya za Kimataifa kama UN, FIFA .nk , kuwa ni ili kupungua kero za Muungano, ila hawataki Tanganyika iwepo

kifungu, 69 (4) kinachohusiana Rais kujinasibisha na chama chake wanasema kifutwe kwani mara nyingi Marais huwa ndio wenyeviti wa Chama .......

Kifungu, 93(2), idadi ya Mawaziri wanasema iwe 20 .......

kifungu, 94(2), kinachokatwa mgombea urais walau awe na shahada ya kwanza , wanasema kifutwe kwani sio lazima kuwa na elimu ili uwe Rais boboar kifungu,

kifungu 107 , kinachotoa fursa kwa Bunge kuithinisha mikataba mikubwa kuhusu rasilimali za taifa , wanasema kifutwe kwani hilo sio jukumu la Bunge bali la Serikali....

kifungu, 105 , wanasema wabunge wa Muungano wawe 360 na kwa suala wa 50/50 wanaume na wanawake ......where on Earth ........

kifungu, 106 (2), wabunge waendelee kulipwa mishahara hata baada ya Bunge kuvunja na kulipwa vinu a mhongo vyao .....eti mpaka Bunge jipya lipatikane......

kifungu, 122(1)(d) ...kuhusu mtu kukosa sifa ya kuendelea kuwa mbunge endpoint amepangiwa na matatizo ya akili , wanasema kifutwe kwani huo ni ugonjwa kama mwingine.

Kifungu 124, wananchi wasiwe na haki ya kuwawajibisha wabunge , hivyo kifutwe na kisiwepo

kifungu, 133(1) ,katibu wa Bunge aendelee kuteuliwa na Rais na sio kamisheni ya Bunge.....eti awe huru katika utendaji na kama atateuliwa na kamisheni ya Bunge hata kuwa huru , .....mbona Rais anateua katibu mkuu kiongozi .....kwanini huyo wanaona atakuwa huru?

Vifungu vya 224-229-234 , uteuzi wa wakuu wa vyombo vya usalama wateuliwe na Rais kama ilivyo leo.

kuhusu Muungano.
wanataka Muungano wa Serikali mbili na hoja zao ni kama ifuatavyo;
1. Kisheria , kwa kuwa hati za Muungano zimekuwa rejea ya rasimu
2. Serikali 3 zitakuwa na utata katika kusimamia na kuendesha Uchumi n hivyo kuleta mgongano
3. Tanganyika itachangia zaidi kuendesha serikali tatu kutokana na uchumi wake na hivyo kuivuruga Zanzibar .....vipi kuhusu serikali mbili........
4. Jamii imepanga na sana kwa kuoleana na kuishi pamoja .......so

haya ndio sehemu ya mapendekezo ya CCM yalivyowasilishwa na Asha Rose Migiro Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu rasmu ya katiba .

Katibu Mkuu wa UN hakufanya makosa kumtimua huyu Mpare kabla ya muda wake. Kumbe ni mtupu kiasi hiki??? Yaani anapewa UTUMBO ulio jaa kinyesi aupeleke sokoni naye bila kutafakari anakubali? Ni huo Urais anao taka apigiwe chapuo!!!

Heri ametusaidia kumjua jinsi alivyo mtupu!!
 
:Cry:
clip_image002.jpg
:disapointed:
 
Mapendekezo haya ndio yanafanywa CCM na wabunge wake kuhakikisha kuwa wana control ya Bunge la katiba ili kama wakina warioba hawatapitisha haya mapendekezo yao basi wayarejeshe kwa njia ya amendments kwenye Bunge la katiba.
 
Haki sawa na wengine
Ikiwa kuna mtu anaweza kutuwekea mapendekezo yote ya CCM na CHADEMA hapa jukwaani itatusaidia sana kuchambua na kutupa uwezo wa kuwelewa ni yapi yatachukuliwa na yapi yataachwa
 
...'kifungu, 62 Znz iruhusiwe kujiunga na Jumuiya za Kimataifa kama UN, FIFA .nk , kuwa ni ili kupungua kero za Muungano, ila hawataki Tanganyika iwepo'...
Pendekezo hili linatia wasiwasi wa kudumu kwa muungano. Kwa maana rahisi ni kuwa kuwe na nchi mbili huru (sovereign); moja ikiitwa Zanzibar yenye kiti Umoja wa Mataifa na mipaka inayoeleweka; ingine inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo mipaka yake haijulikani (kwa sababu Zanzibar haiwezi kuwemo). Sijui kama hii JMT itaruhusiwa kuwa na kiti Umoja wa Mataifa!
 
Mapendekezo haya yanaonesha jinsi CCM walivyo "emptyheaded" hivi suala la kuoana ni hoja, mbona kuna wazungu alioolewa na watanzania au wazambia mimi nina wasiwasi na vyeti vyao naomba NECTA ifanye uchunguzi, VIONGOZI BOGAZI HAWATAKIWI KUONGOZA NCHI, kweli nimeamini kuwa 50 yearz hatujawahi kuwa na viongozi. KWELI CCM kichwa cha wendawazimu, wamechanganyikiwa hadi hawana point! lo! nawahurumia. POLENI CCM.
 
Back
Top Bottom