Mapendekezo ya Edwin mtei kwenye katiba mpya

Mapendekezo ya Edwin mtei kwenye katiba mpya

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
[TABLE="width: 1013"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
Edwin Mtei

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR="bgcolor: #ffffff"]
[TD]MAPENDEKEZO haya nayaandika ili niyatumie nitakapopata fursa ya kukutana na Tume ya Marekebisho ya Katiba. Endapo tume itayataka baada ya maelezo yangu, nitawaachia nakala ili wasome na kuyatafakari zaidi.


Mtiririko wa haya mapendekezo unafuata jinsi nilivyopata wazo ambalo nilidhani lingefaa kuingizwa katika Katiba Mpya, na ambalo nilihisi ningeweza kulisahau endapo halingekuwa katika kumbukumbu zangu za maandishi.

1. UPENDELEO KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kama Tanzania tunanuia kwa dhati kuwa na serikali itakayohakikisha haki kwa wananchi wote na maendeleo endelevu, amani na umoja wa kitaifa, Tume ya Marekebisho ya Katiba itabidi ipendekeze chombo ambacho kitahakikisha hakuna upendeleo katika kuajiri watumishi wa umma. Chombo hicho kiwe na jukumu la kuhakikisha watumishi wa umma ni wazalendo kweli kweli, ni waadilifu, mahiri makini na wana taaluma zinazohusika katika nafasi wanazotaka kujaza. Wawe ni watu wenye kujali maslahi ya kitaifa, wasio na uroho wa kutajirika haraka haraka, walio na huruma kwa wanyonge, wasio na ubaguzi wa kijinsia, rangi ama dini, na wenye nia ya kutatua matatizo yetu. Tukiendeleza utumishi unaojali zaidi nasaba au dini, kama dalili zinavyoonyesha sasa, tutakwama.
Hicho chombo kihusike na utumishi wote wa umma. Hapa namaanisha hata wateule wa kisiasa washughulikiwe na kuchujwa na hicho chombo kitakachohakikisha ni wazalendo wenye sifa, hususan taaluma inayohusika na uadilifu wao uchunguzwe kihadhara na uthibitishwe, kabla ya kuajiriwa.


Hapa naaminisha kwa mfano mteule wa rais, yaani waziri au mkuu wa mkoa au wilaya awe anathibitishwa na Bunge au na Halmashuri ya Wilaya, baada ya kupitia chombo hiki.
Chombo hicho mahsusi kiandae udahili (interview) ambao utazingatia na kusisitiza sifa nilizotaja hapo juu, hususan uadilifu, uzalendo na uwezo wa kitaaluma wa mhusika, kabla ya rais kumteua na kupeleka jina lake bungeni au kwa halmashauri ili athibitishwe au aidhinishwe.


Viongozi wote waandamizi wa wizara na idara, pamoja na wale wa taasisi za umma ambao sasa wanateuliwa na rais au na bodi zao, wahusishwe katika udahili na mchakato huu wa kupata ajira katika taasisi za umma.
Kutokana na umuhimu wa chombo ninachopendekeza, pamoja na hadhi ya waajiriwa watakaohusika, hicho chombo kiwe ni tume (Commission) ya watu mashuhuri, waliobobea katika fani zao; na kiwe na uhuru. Kujitegemea kwake kutakuwa kunahifadhiwa (guaranteed) kikatiba.


2. DEMOKRASIA YENYE UHAKIKA
Demokrasia ya kwelil iliyo na uhuru na haki kwa raia wote kuchagua viongozi na kuchangia mawazo bila vikwazo, ni muhimu kwa maendeleo endelevu kwa nchi yetu. Kwa hiyo Tume ya Katiba Mpya ipendekeze kwamba: Kiongozi anayeteuliwa na chama chake kugombea u-rais aruhusiwe pia kugombea u-bunge katika jimbo atakalochagua. Kwa vile mara nyingi huyu mgombea u-rais atakuwa ni kiongozi mahiri katika chama chake, endapo atashindwa kupata u-rais, anaweza kushinda u-bunge. Kwa hiyo Bunge litakuwa na viongozi wakuu wa vyama vya siasa wengi, na mijadala bungeni itasisimka zaidi kwa michango yao.
Chini ya katiba ya sasa, viongozi wa vyama mahiri, ambao wanateuliwa na vyama vyao kugombea u-rais, wakishindwa kuupata wanajikuta wako nje ya Bunge na hivyo michango yao katika chombo hiki muhimu cha kitaifa, inakosekana.


Kama tunathamini uchambuzi makini katika Bunge letu, na kwamba uchambuzi wa aina hiyo utaimarisha demokrasia na maendeleo endelevu, na kuhakikisha serikali inadhibitiwa vilivyo, basi vyama vya siasa mahiri ni vyema viwakilishwe na viongozi wao mahiri. Pendekezo hili juu ya utaratibu wa uchaguzi wa rais na wabunge utahakikisha hilo.
Nielewavyo, mfumo na utaratibu wa aina hii unafuatwa huko Kenya.


Ingawa amani na utulivu ni muhimu na ni lazima viwepo nchini kwa maendeleo na ustawi wa jamii, na sheria za polisi zinatakiwa kuhakikisha hilo, Tume ya Katika Mpya itambue pia kuwa demokrasia na uhuru wa kweli kwa raia wote ni lazima ili kuhakikisha maendeleo endelevu na matumizi stahiki ya rasilimali za umma.


Kwa hiyo uchambuzi wa kina wa sheria za polilsi na marekebisho pale zinapokingana na uhuru kamili na usalama wa raia, lazima ufanywe na tume kwa kuyaingiza marekebisho hayo katika katiba mpya au kupendekeza marekebisho stahiki katika sheria za polisi sambamba na kupendekeza katiba mpya.


Kwa maoni yangu, ni fedheha kwa wananchi kutiwa mbaroni kwa kuandamana kwa amani kudai haki au maslahi yao. Uhuru wa kusema au kuhutubia umma, kuelezea maono yao juu ya lolote lihusulo maisha yao, ni haki ya raia hata chini ya katiba ya sasa, na polisi hawawezi kuzuia hilo, bora amani idumishwe.


Dhima (role) ya polisi kuhusu mikusanyiko au maandamano ya watu ni kuhakikisha hakuna vibaka (miscreants) wanaoleta fujo kwa umma wakati wa maandamano, hotuba au maelezo ya raia huru. Kwa vile hili inaonekana halikufafanuliwa ipasavyo wakati wa kuruhusu vyama vingi vya siasa 1992, tume ichukue jukumu hilo la kueleza dhima halisi ya polisi.

3. HAKI YA KUISHI
Licha ya kwamba katiba yetu ya sasa inasisitiza hifadhi ya maisha, inaonekana kwamba vyombo vyetu vya usalama vikisitisha maisha ya binadamu hakuna hatua yoyote inayochukuliwa wazi wazi dhidi ya mwanausalama mhusika.

Kumekuwa na mauaji ya raia kwa polisi kulenga vichwa au vifua vya watu, na mambo yameishia kimya kama vile polisi kaua ndege au mbuzi.
Kuthibitisha kwamba tunajali maisha, mtu yeyote akiuawa (hata na polisi) ni lazima kuwe na public enquiry (inquest), na mhusika aonekane kihadhara kuwa anachukuliwa hatua, ili athibitishe hakutumia nguvu za ziada kudhibiti ghasia au hata uhalifu wa sheria. Hatuwezi kuendelea kuwa na viongozi wa polisi wanaotishia kutumia risasi za moto.
Nchi nyingi duniani polisi wanakuwa na virungu tu (batons), na pale inapokuwa nje lazima wawe na bunduki wanakuwa na rubber bullets au maji ya kuwasha.
Najua kunaweza kuwa na wahalifu wanaotumia silaha na ni lazima wadhibitiwe wanapotishia maisha ya walinzi wetu wa usalama. Lakini ni lazima pia tuhakikishe wanausalama wetu hawatumii nguvu za ziada, ili katiba yetu mpya ionekane imesimika na kuheshimu maisha ya mwanadamu.
Ifafanuliwe pia kwamba ni kinyume na haki za binadamu kumtesa mtuhumiwa aliye mbaroni ili akiri ametenda analotuhumiwa kutenda.


4. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Katiba ikiwa ni mpangilio na utaratibu unaoongoza mamlaka na serikali ya nchi ili wahusika watimize majukumu na wajibu wao, Tume ya Katiba Mpya ni lazima itathmini kwa kina muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwanza licha ya kwamba viongozi na sheria yenyewe inayoongoza tume imetamka kwamba wananchi wengi iwezekanavyo wajitokeze kutoa mawazo yao juu ya katiba mpya, ni pendekezo langu kwamba tume ikiishazingatia mapendekezo hayo yakiishapitishwa na Bunge Maalum kama Katiba Mpya, katiba hiyo iidhinishwe na umma wa Tanganyika na umma wa Zanzibar kwa kura ya maoni.


Mkundi haya mawili, yaani Zanzibar na Tanganyika, ni lazima yote yakubali Muungano kwa asilimia zaidi ya 50 za kura zao, la sivyo Muungano utakuwa batili.
Kutokana na uwezekano kwamba wananchi wanaweza kuikataa katiba mpya kwamba kwa sababu tu ya kipengele kimoja kinachohusu kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar, ni pendekezo langu kwamba tume ipendekeze kura ya maoni (referendum) juu ya uwepo wa muungano wa nchi hizi mbili kwanza, kabla ya kutathmini na kukamilisha masuala mengine katika katiba.
Najua kuwa pendekezo hili litaigharimu nchi zaidi. Lakini kuendelea na kukamilisha katiba mpya kabla ya kuhakikisha kwamba Muungano utakuwepo, inaweza kuwa ni balaa kubwa zaidi.


Pili, ingawa vyama vya siasa kadhaa na mahakama vimekuwa na msimamo kwamba utaratibu wa mgombea binafsi kwa nafasi ya ubunge na udiwani uruhusiwe, chama tawala na serikali yake vimekataa.
Ni pendekezo langu kwamba katiba mpya iingize mgombea binafsi kwa nafasi ya ubunge na udiwani na nafasi zote za uongozi nchini isipokuwa u-rais.
Katika hali ya Tanzania ya sasa kiuchumi, rais ni lazima awe ni mwanachama wa chama cha siasa.


Wananchi ni lazima wapige kura kwa rais anayeongoza chama chenye sera na misimamo inayofahamika. Mgombea binafsi hawezi kuwa na sera zilizo wazi kwa wananchi wote.
Rais pia ni lazima aunde serikali yake kutokana na wanasiasa wenye misimamo inayojulikana na kukubalika kwa umma. Mgombea binafsi hawezi kuwa na fursa hiyo ya kuwa na wanasiasa wajulikanao kwa sera na misimamo. Kwa hiyo kusiwe na mgombea binafsi kwa nafasi ya u-rais.


(c) Ibara ya katiba ya sasa kuhusu Uchaguzi wa Rais, inayotamka kwamba Tume ya Uchaguzi ikishatangaza kwamba mgombea ameshinda, hakuna chombo au taasisi yoyote itakayohoji au kupinga, ifutwe. Maoni yangu ni kuwa hiki kipengele kilikuwa ni sehemu ya katiba yetu tulipokuwa tunakubali chama kimoja cha siasa.
Katika mazingira ya vyama vingi vya siasa na kuongezeka kwa fursa ya rushwa na uchakachuaji, ni muhimu kuwa na kipengele kinachoruhusu uchambuzi wa matokeo kuhakikisha matakwa ya wapiga kura yametekelezwa.


(d) Pendekezo lingine ni kwamba mkuu wa nchi, yaani rais, ni lazima awe anatokana na zaidi ya asilimia 50 ya wapiga kura.Endapo katika uchaguzi matokeo ya uhesabuji wa kura yataonyesha hakuna mgombea u-rais aliyepata zaidi ya asilimia 50, basi Tume ya Uchaguzi itapanga uchaguzi urudiwe, na wagombea wawili wanaoongoza wapambane katika kipindi cha majuma manne tangu kutangazwa kwa matokeo. Mpango huo utaruhusu wapiga kura kutumia vitambulisho vile vile na vituo vya kupigia kura vile vile. Gharama zitakuwa ni kuchapisha karatasi za wagombea wawili tu na kuhakikisha wasimamizi wanakuwepo.


(e) Katika sehemu niliyozungumzia Chombo cha Kuondoa Upendeleo katika uteuzi wa watumishi wa umma, nilimaanisha kuwa rais akiteua mwananchi kushika nafasi ya kisiasa (mfano, Waziri, Mkuu wa Mkoa) atadahiliwa na hicho chombo. Lakini nifafanue kuwa napendekeza kwamba nafasi za kisiasa zote zithibitishwe na chombo cha siasa kinachosimamia huyo mteule wa rais, yaani Bunge, lithibitishe mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, na viongozi wa kisiasa katika idara za halmashauri za majiji, miji na wilaya wathibitishwe na halmashauri husika.


Pale ambapo mtumishi atakuwa amepitia mchakato wa kitaaluma kupanda ngazi katika utumishi wa umma (civil service), basi mchakato wake utakuwa ni kwa chombo cha kuondoa upendeleo tu. Yaani Permanent Secretary au Mkurugenzi wa Idara au wa Halmashauri atadahiliwa na chombo cha kuondoa upendeleo tu kuthibitisha uzalendo, umakini, umahiri na kadhalika na kulinganishwa na wenzie wanaostahili cheo chake.


h.sep3.gif

Edwin Mtei alipata kuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) na baadae Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Maelezo marefu ila hapo nilipopitia kidogo naona kama kawaida ya viongozi wa cdm, mzee anaendelea kutetea maslahi ya kundi na si watanzania. Read between line utampata.
 
mzee watanzania wanakukubali sana mungu akuongezee maisha marefu hushudie jinsi makamanda uliowachia kijiti wanavyo mtoa mkoloni ikulu
 
Ni unafiki kujifanya unazungumzia suala la udini hadharani huku unamlaumu mwenzako eti mdini kisa alisimama hadharani na kusema uchaguzi ulitawaliwa na udini.
Lakini si ndio huyuhuyu Edwin Mtei anayeendelea kumsapoti Mbowe kukiongoza chama wakati yeye aliudhihirisha udini wake kwa kiongozi mwenzake wa juu wa chama? Maneno haya kutoka kwa Mbowe kwenda kwa Zitto hayatoshi kumuona Mbowe mdini? " mh Zitto mbona una kiherehere wewe, si uende huko kwa waislamu wenzako Cuf?. Haya anayatamka mbele ya uongozi wa juu wa chama, no punishment given to him,then unazungumzia udini? Hypocracy!
 
Unapokuwa unamrekebisha mwenzako wewe mwenyewe uwe mfano.
Kwanza nakubaliana na wewe kuwa kiongozi atakaechaguliwa/kuteuliwa na Raisi na kuto/kuthibitisha na bunge na vyombo vyengine katika secta flani awe mweredi wa sekta hiyo, sasa mbona chama chako mmewapa watu wizara(mawaziri vivuli) mbalimbali na nyadhifa mbalimbali wakati elimu na uweze wao ni wa nchini sana?
Hypocracy.
 
DEMOKRASIA YA UHAKIKA,
Mzee, maoni yako ni mazuri sana ila nashindwa kukuelewa kwa sababu wewe na chama chako mmeshindwa kusimamia hilo. Mnavukuza wanachama bila kuzingatia katiba, kuzuia viongozi flani wasigombee nyadhifa za juu za chama chako.
Halafu unaposema agombea uraisi aruhusiwe kugombea ubunge, sasa akipata vyote atatekelezaje majukumu hayo mawili,Ukizingatia mb anapaswa kuwa karibu na wananchi wake wakati mwingi au sijakuelewa? Msaada tafadhari.
 
Ni unafiki kujifanya unazungumzia suala la udini hadharani huku unamlaumu mwenzako eti mdini kisa alisimama hadharani na kusema uchaguzi ulitawaliwa na udini.
Lakini si ndio huyuhuyu Edwin Mtei anayeendelea kumsapoti Mbowe kukiongoza chama wakati yeye aliudhihirisha udini wake kwa kiongozi mwenzake wa juu wa chama? Maneno haya kutoka kwa Mbowe kwenda kwa Zitto hayatoshi kumuona Mbowe mdini? " mh Zitto mbona una kiherehere wewe, si uende huko kwa waislamu wenzako Cuf?. Haya anayatamka mbele ya uongozi wa juu wa chama, no punishment given to him,then unazungumzia udini? Hypocracy!

Sasa kwenye hayo maandishi udini uko wapi? Nadhani wewe ndiye unauleta huo udini sasa
 
Polisi wanahaki pia ya kujitetea pale wananchi wanapoonyesha kuhatarisha amani yao. Virungu havitoshi ni hatari kwa usalama wao. Chama chako kina miliki jeshi la Red brigade na wanasiraha, always wanawatageti polisi na wananchi, kwahiyo hapa unataka kutengeneza mazingira ya jeshi lenu kutekeleza operation yake kirahisi. Haliwezekani na hapa nakupinga.
 
Sasa kwenye hayo maandishi udini uko wapi? Nadhani wewe ndiye unauleta huo udini sasa

Nisome tena utanielewa mkuu, Mtei anapaswa kuonyesha mfano wa kushughulikia ishu ambayo yeye leo anaipigia kampeni.
 
Kwenye muungano nakuunga mkono, ni wakati watanzania hasa wazanzibar wasikilizwe.
 
Unapokuwa unamrekebisha mwenzako wewe mwenyewe uwe mfano.
Kwanza nakubaliana na wewe kuwa kiongozi atakaechaguliwa/kuteuliwa na Raisi na kuto/kuthibitisha na bunge na vyombo vyengine katika secta flani awe mweredi wa sekta hiyo, sasa mbona chama chako mmewapa watu wizara(mawaziri vivuli) mbalimbali na nyadhifa mbalimbali wakati elimu na uweze wao ni wa nchini sana?
Hypocracy.

Angalia mazuri mkuu kama unaona yanafaa kwani yakichukuliwa hayo na kuwa incorporated kwenye katiba maana yake hata vyama vya siasa itabidi viweke watu wenye weledi, alichosema kwa hawa viongozi wa kuteuliwa ili kuondoa bias, pia kumbuka hayo maoni ni ya Edwin Mtei kama raia wa Tanzania ambae aliwahi kuwa Gavana wa BOTna haihusiani na CDM.
 
Nisome tena utanielewa mkuu, Mtei anapaswa kuonyesha mfano wa kushughulikia ishu ambayo yeye leo anaipigia kampeni.

Ishu iliyopo ni hayo mapendekezo aliyoyatoa, nimekuuliza udini hapo uko wapi kwenye hayo mapendekezo? Au ni agenda ambayo umeileta wewe mpya? Nimekusoma, na nikaona umeleta ishu ya udini ambayo unadhani yeye Mtei alikuwa nayo hapo awali wakati wa kuteua tume ya kuchukua maoni ya wananchi na kuandika rasimu ya katiba. Sawa, lakini kilicholetwa mezani kwenye huu uzi ni kuhusu mapendekezo yake kuhusu katiba mpya, je kuna udini hapo jamani? Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. By the way, sio vizuri kuendekeza udini mahali ambapo haupo. Mahali ambapo upo unatakiwa ukemewe kwa nguvu zote kabla hatujafikia nchi kama Burma, Iraq nk. tutoe hoja kulingana na kile kilicholetwa mezani.
 
Maelezo marefu ila hapo nilipopitia kidogo naona kama kawaida ya viongozi wa cdm, mzee anaendelea kutetea maslahi ya kundi na si watanzania. Read between line utampata.

si kweli , acha uvivu soma uelewe .
 
Ishu iliyopo ni hayo mapendekezo aliyoyatoa, nimekuuliza udini hapo uko wapi kwenye hayo mapendekezo? Au ni agenda ambayo umeileta wewe mpya? Nimekusoma, na nikaona umeleta ishu ya udini ambayo unadhani yeye Mtei alikuwa nayo hapo awali wakati wa kuteua tume ya kuchukua maoni ya wananchi na kuandika rasimu ya katiba. Sawa, lakini kilicholetwa mezani kwenye huu uzi ni kuhusu mapendekezo yake kuhusu katiba mpya, je kuna udini hapo jamani? Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. By the way, sio vizuri kuendekeza udini mahali ambapo haupo. Mahali ambapo upo unatakiwa ukemewe kwa nguvu zote kabla hatujafikia nchi kama Burma, Iraq nk. tutoe hoja kulingana na kile kilicholetwa mezani.

Msiishambulie viongozi wetu wa ccm kwa malengo ya kujijenga wakati udini umejaa chumbani kwenu huko.
 
Msiishambulie viongozi wetu wa ccm kwa malengo ya kujijenga wakati udini umejaa chumbani kwenu huko.

Rudi kwenye mada. BY THE WAY ==> Clip ya Profesa wa CUF uliisikiliza wewe? Si alisema wazi wazi kuwa walijadiliana na JK Waachiane kwa misingi ya mfanano wa imani/
 
Back
Top Bottom